Back

ⓘ Elimu
                                               

Shule ya msingi

Shule ya msingi ni hatua ya kwanza katika mfululizo wa masomo katika nchi nyingi. Masomo ya msingi huchukua kati ya miaka 5 hadi 8 ya kwanza ya elimu rasmi. Kwa jumla elimu ya juu hujumulisha miaka 6-8 ya masomo kuanzia mwaka wa tano au sita, lakini hutofautiana kati ya nchi na nchi. Asilimia 70 ya watoto waliotimu umri wa kujiunga na shule hujiandikisha katika masomo ya msingi kote ulimwenguni na viwango hivi vinaongezeka. Chini ya mipango ya Elimu kwa wote inayoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, nchi nyingi zina nia ya kufanikisha uandikishaji ...

                                               

Elimu nchini Tanzania

Elimu nchini Tanzania hutolewa na sekta zote mbili, yaani, sekta za serikali na binafsi. Muundo wake kiujumla ni kama ifuatavyo: Miaka 3 zaidi elimu ya Chuo Kikuu Miaka 2 elimu ya juu ya sekondari hutolewa kati ya umri wa miaka 18–19 Fom 5 na 6 Miaka 2 elimu ya vidudu/cheke-chea hutolewa kwa wanafunzi wenye umri kati ya miaka 5–6 miaka 2, lakini hii watoto sehemu kubwa wanaanza wakiwa na umri wa miaka 3, ili kuwa na mazoea ya shule. Miaka 4 elimu ya sekondari hutolewa kati ya umri wa miaka 14–17 Fomu 1-4 Miaka 7 elimu ya msingi ambayo hutolewa kwa watoto walio na umri wa miaka 7–13 Darasa ...

                                               

Wizara ya Elimu

Nchi kadhaa zina idara za serikali zinazoitwa Wizara ya Elimu au Wizara ya Elimu ya Umma. Wizara ya kwanza kabisa inafikiriwa kuwa Tume ya Taifa ya Elimu na ilianzishwa mwaka wa 1773 katika Madola ya Kipolishi-Kilithuania. Wizara ya Elimu Jamaika Wizara ya Elimu na Utafiti Uswidi Wizara ya Elimu Bahrain Wizara ya Elimu Jamhuri ya China Wizara ya Elimu India Shirika la Kitaifa ya Elimu ya Kifini Wizara ya Elimu Uingereza Wizara ya Elimu Bangladesh Wizara ya Elimu Urusi Wizara ya Elimu Finland Sekretarieti ya Elimu ya Umma Mexico Wizara ya Elimu Misri Wizara ya Elimu Namibia Shirikisho ya Ni ...

                                               

Elimu mbadala

Elimu mbadala, ambayo pia hujulikana kama elimu isiyo rasmi, ni dhana yenye maana pana na inayoweza kutumiwa kurejelea aina zote za elimu zilizo nje ya elimu ya kawaida. Hujumuisha si tu mitindo ya elimu inayokusudiwa wanafunzi wenye mahitaji ya pekee lakini pia mitindo inayolenga hadhira ya jumla na kutumia mitindo na falsafa badala ya elimu. Elimu mbadala mara nyingi huwa matokeo ya mabadiliko katika elimu yaliyotokea katika misingi mbalimbali ya falsafa ambayo kwa kawaida ni tofauti na elimu ya jadi ya lazima. Mabadiliko mengine yana misingi ya kisasa, kiutafiti au kifalsafa, ilhali men ...

                                               

Falsafa ya elimu

Falsafa ya elimu ni utafiti wa kifalsafa juu ya kusudi, utaratibu na ubora wa elimu, kwa kuchunguza ufafanuzi, malengo na maana ya elimu kwa jumla au ya mtazamo mmojawapo juu yake. Falsafa ya elimu kwa kawaida huonwa kama tawi la falsafa na la elimu vilevile.

                                               

Mwalimu

Mwalimu ni mtu anayesaidia wengine kupata ujuzi, maarifa na tunu. Kazi hiyo inaweza kufanywa na yeyote katika nafasi maalumu, kwa mfano mzazi au ndugu akimfundisha mtoto nyumbani, lakini kwa wengine ndiyo njia ya kupata riziki inayomdai karibu kila siku kwa miaka mingi, kwa mfano shuleni. Huko mwalimu anatakiwa kuwa na shahada au stashahada, kadiri ya sheria za nchi na ya ngazi ya elimu inayotolewa.

                                               

Akademia

Akademia ni shule au chuo kinachotoa elimu au taaluma maalumu, k.v. lugha, muziki, michezo au sanaa. Jina linarejelea taasisi iliyoundwa na Plato kwenye mwaka 385 KK ilikuwa chuo chake cha falsafa mjini Athens iliyokuwepo ndani ya hekalu ya Athena, mungu wa hekima na elimu. Pia inaweza kuwa kundi la wasomi wenye ujuzi mkubwa katika taaluma fulani, k.v. siasa, uchumi au masuala ya jamii. Tena inaweza kuwa taasisi rasmi inayohamasisha maendeleo ya fasihi, sayansi n.k. Nchi nyingi huwa na "Akademia ya Sayansi" ambayo ni shirika za wataalamu au pia taasisi za wataalamu. Zinalenga kujenga na ku ...

                                               

Alumni

Alumni ni neno la kutaja watu waliokuwa wanafunzi wa chuo kikuu fulani. Asili ya neno ni lugha ya Kilatini ni uwingi wa alumnus inayomaanisha "anayelelewa, anayelishwa". Desturi ya kuunda umoja wa wanafunzi wa kale wachuo fulani ilianzishwa huko Marekani kwa shabaha ya kupata msaada wa watu wenye kazi njema na mapato mema walio tayari kusaidia chuo chao cha zamani. Alumni wanajitolea kwa hali na mali, kwa kukipa chuo chao pesa, kwa kutumia athira yao katika siasa kwa ajili ya sheria za kusaidia elimu, kwa kuwapa wanafunzi wachuo chao nafasi za ajira na kadhalika. Siku hizi kuna vyama vingi ...

                                               

Alumniportal Deutschland

Alumniportal Deutschland ni ukurasa kwenye mtandao. Madhumuni yake ni kuwaunganisha Alumni wa Ujerumani. Alumni-Ujerumani ni watu wote duniani ambao walisomea, waliofanya kazi, utafiti, waliosoma lugha ama kwa kusafiri kwenda Ujerumani ama katika chuo chochote cha Ujerumani kwenye nchi za kigeni. Ukurasa huu watumika bila malipo na sio wa kibiashara. Huu ni mradi wa mashirika matano ya Ujerumani ya ushirikiano wa kimataifa. Fedha za mradi huu zinatoka katika Wizara ya ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo.

                                               

Andalio la somo

Andalio la somo ni mpangilio au hatua zinazofuatwa na mwalimu wakati wa kufundisha somo fulani darasani. Mwalimu anapaswa kuandaa andalio la somo kabla na hata wakati wa mchakato mzima wa kufundisha.

                                               

Taasisi ya Wahandisi Tanzania

Taasisi ya Wahandisi Tanzania ni taasisi isiyolenga faida ambayo dhamira yake ni kukuza taaluma ya uhandisi nchini Tanzania na zaidi. Baadhi ya vitu vyake ni kukuza maendeleo ya jumla ya sayansi na mazoezi ya uhandisi na matumizi yake, na kuwezesha kubadilishana kwa habari na maoni juu ya masomo hayo miongoni mwa wanachama wa Taasisi.

                                               

Tamsya

Tanzania Muslimu Student and Youth Association ni asasi isiyo ya kiserikali ya wanafunzi na vijana wa Kiislamu iliyosajiliwa mwaka 2010. Asasi hiyo hapo mwanzo ilikuwa ikijulikana kama TAMSA wakati ikianzishwa mwaka 1993 kwa malengo ya kuwaunganisha wanafunzi wa Kiislamu pamoja na vijana wa Kiislamu huku malengo yake makuu ikiwa ni kutoa msaada wa kiroho na wa kijamii.

Usomaji
                                               

Usomaji

Usomaji ni hali ya kusoma maandishi, hasa ya vitabu vilivyoandikwa na wanadamu wengine. Maarifa hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kupelekea mwanadamu kutafuta maarifa naye mwenyewe kuandika vitabu mbalimbali.

                                               

Utabiri

Utabiri au ubashiri ni uoteaji au ukisiaji wa mambo yatakayotokea muda ujao. Mtu mwenye uwezo wa kutabiri huitwa mtabiri. Mara nyingine utabiri unatokana na uchunguzi wa kisayansi, kwa mfano utabiri wa hali ya hewa. Katika dini mbalimbali utabiri unatokana na karama maalumu ambayo mtu anajaliwa na Mwenyezi Mungu.

                                               

Uzamili

Uzamili ni shahada ya pili inayotolewa na vyuo vikuu baada ya digrii ya bachelor na kabla ya shahada ya uzamivu. Shahada hiyo ya pili inamruhusu msomi aliyeipata afundishe katika taasisi za elimu ya juu.