Back

ⓘ Historia
                                               

Historia ya Moroko

Habari za kimaandishi za kwanza ni kutoka karne za kwanza KK. Wafinisia walijenga miji yao pwani lakini eneo la ndani lilibaki nchi ya Waberber waliounda ufalme wa Mauretania ya Kale usiuchanganye na nchi ya kisasa Mauretania uliounganisha sehemu kubwa ya Moroko ya kaskazini. Wamauretania wa kale walishirikiana na Dola la Roma hadi kuwa jimbo la dola hili kwa jina la "Mauretania Tingitana". Wakati wa kudhoofika kwa Dola la Roma kuanzia mwaka 400 BK kukawa na uvamizi wa Wavandali.

                                               

Historia ya Denmark

Utafiti wa akiolojia umeonyesha ya kwamba Denmark iliwahi kuwa na vikundi vya wawindaji tangu muda mrefu sana. Lakini katika nyakati za kupanuka kwa barafuto za Skandinavia walipaswa kundoka tena. Eneo la Denmark lilifunikwa kabisa na barafu hadi takriban miaka 13.000 hadi 15.000 iliyopita. Tangu mwaka 4000 K wakulima walianza kupatikana nchini. Hakuna uhakika kama Denmark ilikaliwa na Wakelti; kuna mabaki ya kiakolojia ya kuonyesha athira ya Kikelti, lakini haijulikani kama ni kutokana na biashara na maeneo ya Wakelti walioendelea zaidi au kama Wakelti wenyewe walikaa hapa.

                                               

Historia ya Kirgizia

Historia ya Kirgizia inahusu eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya Kirgizia. Hadi mwaka 1991 Kirgizia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyet, ikijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kikirgizi". Ilipata uhuru wake katika mwendo wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti. Kabla ya uhuru yalitokea mabadiliko katika uongozi wa chama cha kikomunisti. Viongozi wapya waliotafuta njia bila udikteta mkali walishika uongozi na rais Askar Akayev alirudishwa madarakani katika uchaguzi wa kwanza na wa pili. Lakini uchaguzi wa mwaka 2005 ulionekana haukuwa huru, hivyo hasira ya wananchi ikalipuka katika m ...

                                               

Historia ya Eswatini

Historia ya Eswatini inahusu eneo la Kusini mwa Afrika ambalo wakazi wake leo wanaunda Ufalme wa Eswatini. Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani. Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi. Waswati walianzisha ufalme wao katikati ya karne ya 18 chini ya Ngwane III; mipaka ya sasa ilikubalika mwaka 1881. Baada ya vita kati ya Waingereza na Makaburu, Swaziland ilukuwa nchi lindwa ya Uingereza tangu mwaka 1903 hadi 1967. Chini ya mfalme Sobhuza II aliyetawala kwa muda mrefu sana 1921-1982, Swaziland ilipata uhuru tarehe 6 Septem ...

                                               

Lango: Historia

                                               

Akiolojia

Akiolojia ni somo linalohusu mabaki ya tamaduni za watu wa nyakati zilizopita. Wanaakiolojia wanatafuta vitu vilivyobaki, kwa mfano kwa kuchimba ardhi na kutafuta mabaki ya majengo, makaburi, silaha, vifaa, vyombo na mifupa ya watu.

                                               

Anno Domini

Anno Domini ni namna ya kutaja miaka katika kalenda ama Kalenda ya Gregori au Kalenda ya Juliasi. Jina kamili ni "Anno Domini Nostri Jesu Christi" Mwaka wa Bwana wetu Yesu Kristo likirejea idadi ya miaka tangu kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Katika lugha ya Kiingereza ni njia ya kawaida ya kutaja miaka kama "AD" ambayo ni sawa na matumizi ya BK au "BC" yaani "before Christ" tazama KK; ni pia kawaida katika maandiko ya kihistoria yanayotumia lugha ya Kilatini.

                                               

Anthropolojia

Anthropolojia ni fani ya elimu inayochunguza pande zote binadamu kuanzia wale wa kale. Matawi yake mbalimbali yanachunguza maisha ya jamii, utamaduni pamoja na taratibu na tunu, athari ya lugha, mabadiliko ya kimwili n.k. Kwa vyovyote, anthropolojia inahitaji ushirikiano wa sayansi mbalimbali, ikiwemo teolojia. Akiolojia inaweza kutazamwa kama sehemu ya anthropolojia k.mf. Marekani au ya historia, lakini pia kama fani ya pekee k.mf. Ulaya.

                                               

Baada ya Kristo

Baada ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo ni namna ya kutaja miaka ambayo imekuwa njia ya kuhesabu miaka inayotumika zaidi duniani. Kila mwaka huhesabiwa kuanzia ule uliodhaniwa kuwa mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Miaka iliyotangulia kuzaliwa kwake Yesu huitwa Kabla ya Kuzaliwa kwake Yesu Kristo au kifupi: KK.

                                               

Chimbuko la mwanadamu

Chimbuko la mwanadamu ni suala linalochochea utafiti mwingi wa akiolojia, ili kuelewa wapi walitokea watu wa kwanza. \ Suala hilo ni muhimu kwa fani mbalimbali, dini ikiwemo. Kwa sasa wataalamu karibu wote wanakubaliana kwamba chimbuko la mwanadamu lilikuwa barani Afrika, lakini wanaleta ushahidi tofauti ili kupendekeza Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika, Afrika Magharibi au Afrika Kaskazini. Sehemu ya bonde la Ufa lijulikanalo kama bonde la Oltupai lililoko ndani ya Hifadhi ya Serengeti nchini Tanzania ndiko kulikogunduliwa masalia ya kale kuliko yote yanayojulikana hivi sasa kati ya viu ...