Back

ⓘ Dini
                                               

Dini nchini Urusi

Dini nchini Urusi zimepata uhai mpya na kustawi tena tangu Ukomunisti uanguke mwaka 1989. Wafuasi wa dini hawahesabiwi katika sensa, hivyo kuna makadirio tu. Kwa jumla Waslavi mara nyingi ni Wakristo wa Kiorthodoksi, wasemaji wa lugha za Kiturki ni zaidi Waislamu, na wenye lugha za Kimongolia mara nyingi hufuata Ubuddha. Mnamo Agosti 2012 kulikuwa na kadirio la asilimia 46.8 za Warusi kuwa Wakristo na asilimia 25 waliamini uwepo wa Mungu lakini bila kufuata dini yoyote. Makadirio mengine yalitaja asilimia 76 za Warusi kuwa Wakristo au asilimia 65.

                                               

Uyahudi

Uyahudi ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, lakini jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu wa kabila la Yuda tu. Uyahudi Yuda ni pia jina la kihistoria la sehemu ya kusini ya nchi ya Palestina au Israel. Kwa jumla kuna namna mbili za kuangalia Uyahudi: kama dini au kama taifa. Namna zote mbili huchanganyikana na kutumiwa pamoja mara kwa mara. Kuna Wayahudi wanaojitazama raia wa nchi fulani na Uyahudi wao ni katika imani tu. Kuna Wayahudi wengine wanaosema hawafuati dini ya Kiyahudi wala hawaamini lakini wanajisikia kuwa Wayahudi k ...

                                               

Dini barani Afrika

Dini barani Afrika inaheshimika sana na imeathiri sana utamaduni, falsafa na sanaa zake. Kwa sasa wakazi wengi ni wafuasi wa Ukristo na Uislamu, lakini bado wapo wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika. Pamoja na hayo hizo dini za jadi zinaathiri imani na maisha ya Wakristo na Waislamu wengi vilevile.

                                               

Dini ya miungu mingi

Mifano mashuhuri ni dini za kale kama zile za Misri ya Kale, Ugiriki ya Kale na Roma ya Kale. Leo hii dini zinazoamini umoja wa Mungu, kama vile Ukristo na Uislamu, huwa na wafuasi wengi duniani. Lakini kuna pia wafuasi wengi wa dini zinazosadiki miungu mingi kama vile Uhindu India na Shinto Japani.

                                               

Wakaodai

Wakaoda ni wafuasi wa dini ya Vietnam inayomuamini Mungu mmoja. Jina lake rasmi ni Dai Dao Tam Kỳ Phổ Do Ilianzishwa katika mji wa Tay Ninh mwaka 1926 kwa kuchanganya imani mbalimbali. Wafuasi wanakadiriwa kuwa milioni 4-6.

                                               

Wamormoni

Wamormoni ni kundi la watu wanaohusiana na dini ya Mormoni, iliyoanzishwa na Joseph Smith huko New York, Marekani, katika miaka ya 1820 akidai alipata njozi na kuonyeshwa kitabu kitakatifu. Baada ya kifo chake 1844, Wamormoni walimfuata Brigham Young hadi eneo la Utah. Leo wengi wao ni waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku ya Mwisho kifupisho cha Kiingereza LDS Church. Kiini cha utamaduni wao ni jimbo la Utah, ambapo wao ndio wengi kati ya wakazi wote, lakini siku hizi Wamormoni wanaoishi nchini Marekani ni wachache kuliko wanaoishi nje kutokana na umisionari mkubwa wanaou ...

                                               

Sinkretisimo

Sinkretisimo ni tabia ya kuchanganya falsafa au dini tofauti. Katika mazingira ya Afrika kusini kwa Sahara, mara nyingi imani na desturi za dini za jadi zinajitokeza katika maisha ya Mkristo au Mwislamu, hata kinyume cha misingi au maadili ya dini hizo. Pengine sinkretisimo inafuatwa kwa makusudi mazima ili kurahisisha ushirikiano wa watu tofauti.

                                               

Aga Khan

Aga Khan ni cheo cha imamu au kiongozi wa Wanizari ambao ni kundi kubwa la pili ndani ya Waislamu Washia wakihesabiwa katika dhehebu la Waismaili. Maimamu wa Wanizari walianza kutumia cheo cha Aga Khan wakati wa karne ya 19 ambako Hasan Ali Shah aliyehesabiwa kama imamu wa 46 wa Kiismaili alipewa cheo hiki na mfalme au shah wa Uajemi. MaAga Khan hadi sasa ni wafuatao: Aga Khan I - Hasan Ali Shah Mehalatee 1800–1881, Imamu wa 46 wa Kiismaili 1817–1881 Aga Khan IV - Prince Karim Al Husseini b. 1936,Imamu wa 49 wa Kiismaili tangu 11 Julai 1957 Aga Khan II - Ali Shah ~1830–1885, Imamu wa 47 wa ...

                                               

Agano

Agano ni neno lenye maana nzito katika dini mbalimbali, hasa zile zinazofuata imani ya Abrahamu kwa Mungu mmoja. Upekee wake ni kwamba agano hilo si kati ya pande mbili zilizo sawa, kama yale kati ya watu, bali ni Mungu anayelianzisha na kupanga masharti, akimhimiza binadamu kukubali na kuwa mwaminifu.

                                               

Ahera

Ahera ni neno linalotegemea imani ya kwamba baada ya mtu kufariki dunia anaendelea kuishi kwa namna nyingine, si kwamba anakoma kabisa. Imani hiyo inaweza kutokana na hoja za falsafa lakini zaidi na mafundisho ya dini. Ili mtu aweze kukubali, ni lazima aone kwamba yeye si mwili tu, kwa sababu ni wazi kwamba kifo ni mwisho wa uhai wake duniani na kinaleta uharibifu wa mwili huo. Wengi wanakubali ubora wa binadamu kati ya wanyama ni uwemo wa roho ndani yake, na kwamba ndiyo inayoweza kuendelea kuishi baada ya kutengana na mwili wake. Hali hiyo ni ile ya mzimu na makazi yake yanaitwa kuzimu, ...

                                               

Madhabahu ya Komarock

Madhabahu ya Komarock ni sehemu ya ibada iliyopo mjini Nairobi, Kenya. Anwani yake ni Kangundo Road nje mwa jiji la Nairobi. Eneo hilo linatumiwa na dini la wakatoliki na linaaminika kuwa kuliwahi onekana Maria mtakatifu katika sehemu hii.

Mazishi
                                               

Mazishi

Mazishi ni taratibu za kuheshimu na kuzika maiti ya mtu au mabaki yake. Taratibu hizo zinategemea dini na mila za wahusika, hivyo zinatofautiana sana. Mara nyingi mazishi yanaendana na sala kwa ajili ya marehemu. Kama sivyo kuna kumkumbuka na kukumlilia pamoja na kufariji wafiwa. Mazishi ni ya zamani sana, inawezekana yalikuwepo kabla ya Homo sapiens kutokea, miaka 300.000 iliyopita.

Mimbari
                                               

Mimbari

Mimbari ni mahali pa kutangazia Neno la Mungu katika maabadi ya dini mbalimbali. Umuhimu wake unatofautiana kadiri ya dini na ya madhehebu husika. Kwa mfano, upande wa Ukristo, katika Uprotestanti inashika nafasi ya kwanza ndani ya kanisa, wakati Ukatoliki unapendelea altare inapotolewa sadaka ya ekaristi, ingawa unataka sehemu hizo mbili zilingane kwa kuwa ni meza mbili ambapo Mungu anawalisha wanae kwanza Neno, halafu Mwili na Damu ya Kristo.

                                               

Mizimu

Mizimu inamaanisha roho zilizoishi katika mwili kabla ya kuiaga dunia. Katika baadhi ya dini na mila inaaminika kuwa mizimu inaweza kuwa na faida kwa watu waliopo duniani ina uwezo wa kuwasiliana nao kwa kutumia njia mbalimbali kufuatana na mazingira au utamaduni. Katika Kanisa Katoliki na baadhi ya madhehebu mengine, mizimu inaweza kuwa ya watakatifu. Kuna tofauti kati ya mizimu; pengine ni roho za binadamu ambao hawakutimiza majukumu yao au walifanya kinyume wakati wapo duniani.

                                               

Msiba

Msiba ni hali au tukio lolote la kusikitisha au la kuleta majonzi linalompata mtu binafsi au jamii, kama vile kifo cha ndugu, ajali, kufilisika n.k. Dini mbalimbali zinasaidia kukabili misiba inayoweza ikatokea maishani. Mara nyingi utamaduni kuhusu misiba unategemea dini.

Muujiza
                                               

Muujiza

Muujiza ni tukio lisiloelezeka kisayansi kufuatana na sheria za maumbile. Matukio hayo yanaweza kufikiriwa yamesababishwa ama na Mungu au miungu, hata kupitia mtu wa dini, ama na nguvu nyingine zinazohusiana na ushirikina. Wanateolojia Wakristo wanasema Mungu kwa kawaida anaacha sheria za maumbile zifuate mkondo wake, lakini anabaki huru kuziingilia anavyotaka kwa mipango yake. Injili zinasimulia aina nyingi za miujiza ya Yesu.

Nabii wa uongo
                                               

Nabii wa uongo

Katika dini, nabii wa uongo ni mtu anayejidai kuwa na karama ya unabii lakini hakubaliwi na wale wanaomuita hivyo. Anaweza kuwa nabii kweli, au kujidanganya au kudanganya kwa makusudi ili kujipatia sifa na mali. Nje ya dini, mtu anaitwa hivyo kwa kutetea hoja au mpango ambao msemaji anaona ni mbaya.

                                               

Neno la Mungu

Neno la Mungu ni namna ambayo wafuasi wa dini kadhaa wanavyotazama misahafu yao ili kusisitiza imani yao ya kuwa hiyo iliandikwa kadiri ya Mungu na kuleta kwa usahihi ufunuo wake. Kwa namna ya pekee Uyahudi na Ukristo vinaita hivyo Biblia. Zaidi ya hayo, katika Agano Jipya Mtume Yohane anamwita hivyo Yesu Kristo ili kueleza asili yake ya Kimungu kabla ya kuzaliwa binadamu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kutokana na Bikira Maria.

Njozi
                                               

Njozi

Njozi ni istilahi inayotumika hasa katika maisha ya kiroho kama njia ya mtu kupata taarifa ya mambo yaliyopita, yaliyopo, na yale yajayo. Neno hilo hutumiwa pia kwa maana ya ndoto, ambayo ni ya kawaida pale mtu anapokuwa amepumzisha akili na mwili. Upande wa dini huaminiwa kuwa Mungu hutumia njozi kuwasilisha ujumbe kwa mtu, kama habari juu ya kazi yake au tukio linalotaka kutukia. Kwa kifupi tu Njozi ni tukio lolote la ndoto inaweza kuwa nzuri au mbaya

Patakatifu
                                               

Patakatifu

Patakatifu ni mahali panapoheshimiwa na waumini wa dini fulani kwa sababu mbalimbali, kama vile umuhimu wake katika historia ya dini hiyo. Mara nyingi mahali hapo watu wanakwenda kwa hija. Katika Ukristo ni patakatifu hasa pale Yesu Kristo anaposadikiwa kuwa alikufa akafufuka mjini Yerusalemu. Katika Uislamu ni patakatifu hasa Kaaba mjini Maka.

Pepo
                                               

Pepo

Pepo ni roho wachafu au wabaya wenye nguvu za Kishetani wanaoweza kumshawishi mtu atende mabaya na hata kumwingilia kwa lengo la kumharibia maisha yake kiroho na kimwili. Roho hizo huweza kufikia hatua ya kumpagaa mtu ili kumwendesha afanye mambo mbalimbali kwa kutojielewa kuliko kwa kulewa sana, kama vile kuropoka, kupiga, kurukaruka, kufanya uasherati n.k.