Back

ⓘ Lidia wa Thiatira
Lidia wa Thiatira
                                     

ⓘ Lidia wa Thiatira

Lidia wa Thiatira alikuwa mwanamke mfanyabiashara wa karne ya 1 ambaye kwanza aliongokea dini ya Uyahudi.

Mwinjili Luka katika Matendo ya Mitume kitabu cha Agano Jipya la Biblia ya Kikristo alisimulia habari zake; hivyo amekuwa mtu wa kwanza wa Ulaya ambaye anajulikana kwa jina kuwa aliongokea Ukristo. Ni tunda ambalo Mtume Paulo alilichuma huko Filipi Ugiriki Kaskazini.

Madhehebu mengi yanamheshimu kama mtakatifu katika tarehe tofautitofauti. Kwa Wakatoliki wa Kanisa la Kilatini sikukuu yake ni tarehe 20 Mei awali 3 Agosti.

                                     

1. Katika Matendo ya Mitume

16:11 Basi tukang’oa nanga kutoka Troa, tukafika Samothrake kwa tanga moja, na siku ya pili tukafika Neapoli; 12 na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha. 13 Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. 14 Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo. 15 Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatushurutisha.

Ndio ubatizo pekee katika Matendo ya Mitume ambao uliweza kufanyika katika maji mengi kutokana na mazingira ujirani wa mto.

                                     
  • watakatifu Bernardino wa Siena, Lidia wa Thiatira Aurea wa Ostia, Baudeli, Talalei, Austregesili, Anastasi wa Brescia, Theodori wa Pavia, Protasi Chong
  • waliokutana pale. 14 Mwanamke mmoja, jina lake Lidia mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake
  • waliokutana pale. 14 Mwanamke mmoja, jina lake Lidia mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake