Back

ⓘ RikshoRiksho
                                     

ⓘ Riksho

Riksho ni chombo cha usafiri ambacho kiasili kilikuwa gari dogo lenye kiti lililovutwa na mtu, ilhali abiria amekalia nyuma.

                                     

1. Historia

Riksho ya kwanza ilitengenezwa mwaka wa 1869 nchini Japani. Taarifa zinatofautiana kama mvumbuzi alikuwa mwenyeji wa Japani au mgeni kutoka Ulaya au Marekani.

Zilienea haraka katika nchi za Asia. Riksha za kuvutwa zilipokelewa vizuri mno na watu wa Asia katika karne ya 19 huku vijana wengi wakijitosa katika ajira za kuvuta riksha hizi. Mnamo mwaka 1920 kulikuwa na riksha 60.000 mjini Beijing China na takriban mmoja kati ya wanaume sita katika mji huu alifanya kazi ya kuvuta chombo hiki.

Baadaye riksho ziliendelea kuunganishwa na baisikeli ilhali dereva moja anaendesha baisikeli ya magurudumu matatu ambako abiria hukalia ama mbele ama nyuma ya dereva. Tangu kuenea kwa pikipiki mfumo huu ulibadilishwa kuwa pia na injini ya petroli. Riksho za pikipiki ziliendelea kupata chumba kidogo cha abiria na hivyo zinajulikana kwa jina la tuk-tuk katika sehemu kadhaa za Asia, pia kwa jina la bajaj nchini Uhindi na kutoka huko zilifika kama "bajaji" katika Afrika ya Mashariki.

Riksho asilia za kuvutwa zinapatikana bado katika miji michache lakini idadi inapungua haraka.

                                     

2. Marejeo

  • William E. Lewis. Through the Heartland on U.S. 20: Massachusetts: Volume I: A Historical Travel Guide. PublishAmerica. ISBN 1462624596 kupitia google books
  • David Strand, Rickshaw Beijing: City People and Politics in the 1920s
  • Chi Ming Fung, Reluctant Heroes: Rickshaw Pullers in Hong Kong and Canton, 1874-1954, Hong Kong University Press, 2005 kupitia google books
Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →