Back

ⓘ Kuanguka kwa Soko la Hisa la Marekani 1929
Kuanguka kwa Soko la Hisa la Marekani 1929
                                     

ⓘ Kuanguka kwa Soko la Hisa la Marekani 1929

Kuanguka kwa Soko la Hisa la Marekani 1929 ndilo tukio la awali la Mdororo Mkuu wa uchumi wa Marekani na sehemu nyingine za dunia, kipindi kibaya sana kwa watu wengi kwa kuwa walipoteza kazi zao, wakawa maskini na kutokuwa na makazi.

Bei za hisa za makampuni mengi katika Soko la Hisa la Marekani zilianguka ghafla kuanzia tarehe 24 Oktoba hadi 29 Oktoba 1929. Mshtuko huo ulifuatwa na kufilisika kwa theluthi moja ya benki za Marekani.

Ile siku ambayo imesemwa kuwa mwanzo wa Mdororo Mkuu inaitwa "Black Tuesday". Ndiyo iliyomaliza utajiri wa Roaring Twenties.