Back

ⓘ Kutubu
Kutubu
                                     

ⓘ Kutubu

Kutubu ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Dubu Mdogo. Nyota hii iko karibu sana na nukta ya ncha ya kaskazini ya angani na kabla ya kupatikana kwa teknolojia ya kisasa ilikuwa nyota muhimu kwa ajili ya mabaharia waliotazama angakaskazi. Haionekani kwenye nusutufe ya kusini ya Dunia.

                                     

1. Jina

Kutubu ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini upande wa kaskazini wa ikweta wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema القطب al-qutub inayomaanisha "nyota ya ncha ya kaskazini".

Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kilatini na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Polaris".

Alfa Ursae Minoris ni jina la Bayer ikiwa ni nyota angavu zaidi katika Dubu Mdogo na Alfa ni herufi ya kwanza katika Alfabeti ya Kigiriki.

                                     

2. Tabia

Kutubu iko kwa umbali wa miaka nuru takriban 323 - 433 kutoka Jua letu, tofauti ya namba inatokana na vipimo vinavyoofautiana hadi sasa bila kupata usuluhisho. Mwangaza unaoonekana ni mag 1.98.

Kutubu ni nyota maradufu yenye sehemu tatu: nyota kuu inayojulikana kama α Umi Aa au A 1 inayozungukwa na msindikaji mdogo α Umi Ab au A 2 na hizi mbili zinazungukana na nyota ya tatu α Umi B kitovu cha graviti cha pamoja.

Kutubu ilitambuliwa kwenye mwaka 1780 na William Herschel kwa darubini kuwa nyota maradufu yaani mfumo wa nyota mbili za α Umi na α Umi B. Wakati ule darubini ya Herschel ilikuwa kati ya vifaa bora duniani. Kwa kutumia Darubini ya Angani ya Hubble ilitambuliwa kwenye mwaka 2006 ya kwamba pia nyota ya A yenyewe ni nyota maradufu na sasa Polaris yote inajulikana kama mfumo wa nyota tatu zinazoitwa α Umi A 1, α Umi A 2 na α Umi B.

Nyota kuu ni Kutubu A 1 Polaris Aa ambayo ni nyota badilifu yenye masi ya Jua mara 5 iking’mara 1200 kuliko Jua letu. Kutokana na mng’aro mkubwa inapangwa katika kundi la nyota jitu kuu. Mwangaza wa α Umi Aa ulibadilikabadilika kati ya mag 1.86 hadi 2.13 wakati wa kurekodiwa kama miaka 100 iliyopita. Baadaye kiwango hiki kilipungua kwa muda mrefu lakini kwa miaka ya nyuma kimeanza kuongezeka tena

                                     

3. Kutubu kama Nyota ya Ncha ya Kaskazini

Mtazamaji kwenye nusutufe ya kazkazini ya Dunia anaona nyota ya Kutubu inakaa mahali pake ilhali nyota zote zingine zinazunguka wakati wa usiku. Hali halisi inazunguka pia kidogo lakini haitambuliki na mtazamaji maana haiko kikamilifu kwenye ncha ya anga bali kwa umbali wa nyuzi 0.7°.

Katika kumbukumbu za kale si Kutubu iliyoangaliwa kuwa nyota ya kuonyesha mwelekeo wa kaskazini. Ptolemaio aliitaja kama "kwenye mkia wa Dubu Mdogo" Miaka 2000 iliyopita nyota iliyokuwa karibu zaidi na ncha ya kaskazini ya anga ilikuwa Kochab β Ursae Minoris. Kutokana na kusogea kwa mhimili wa mzunguko ing. en:precession pia Kutubu imefika katika nafasi hii takriban miaka 400 iliyopita na bado inaendelea kukaribia hadi mwaka 2100; baadaye itaendelea polepole kusogea tena mbali na ncha ya kaskazini ya anga. Baada ya miaka 12.000, nyota ya Vega katika Kinubi itakuwa nyota ya ncha ya kaskazini jinsi ilivyowahi kuwa miaka 14.000 iliyopita.

                                     

4. Viungo vya Nje

 • Constellation Guide:Ursa Minor
 • Ursa Minor, kwenye tovuti ya Ian Ridpath, Star Tales, iliangaliwa Oktoba 2017
 • Polaris Alfa Ursae Minoris, kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
                                     

5. Marejeo

 • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
 • Lee, B. C.; Mkrtichian, D. E.; Han, I.; Park, M. G.; Kim, K. M. 2008. "Precise Radial Velocities of Polaris: Detection of Amplitude Growth". The Astronomical Journal. 135 6: 2240 online hapa
 • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 437 online kwenye archive.org
 • Turner, D. G.; Kovtyukh, V. V.; Usenko, I. A.; Gorlova, N. I. 2013. "The Pulsation Mode of the Cepheid Polaris". The Astrophysical Journal Letters. 762: L8 online hapa
 • Ptolemys Almagest, translated and annotated by G.J. Toomer, London 1984, ISBN 0-7156-1588-2 online hapa
                                     
 • wengi waliopo Ulaya au Marekani hawawezi kuona kamwe nyota mashuhuri ya Kutubu Polaris Mtazamaji katika Afrika ya Mashariki yupo karibu na ikweta, kwa
 • ncha ya anga. Kwenye nusutufe ya kaskazini ya Dunia kuna nyota angavu ya Kutubu en: Polaris iliyopo karibu sana kwenye ncha ya anga ya kaskazini. Kwenye
 • zinazoonekana vema upande wa kaskazini. Kwa hiyo hawezi kuona kamwe nyota ya Kutubu Polaris iliyopo kwenye ncha - anga ya kaskazini. Kinyume chake watu wengi
 • kundinyota kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia yetu. Nyota angavu zaidi ni Kutubu en: Polaris iliyotumiwa sana na mabaharia kwa sababu inaonyesha daima upande
 • nyota ya 11.0 mag. Mwanzoni nyota ya Kutubu Polaris ilifafanuliwa kuwa na mag 2. Baada ya kutambua ya kuwa Kutubu ni nyota badilifusasa ni Vega inayotumiwa
 • kusamehewa dhambi ya kukataa neema ambayo Roho Mtakatifu anatusukuma tuamini na kutubu kwa sababu pasipo imani na toba hapana msamaha. Kila dhambi na kila neno
 • 421 hivi alikuwa mwanamke aliyeishi peke yake jangwani miaka 47 baada ya kutubu maisha yake ya dhambi miaka 17 ya ukahaba mjini Aleksandria Tangu kale
 • ikituondolea adhabu nyingi na kutuletea huruma ya Mungu, yaani nafasi na neema ya kutubu Tito 2: 11 - 14 Hatimaye kutakuwa na hukumu itakayobagua waadilifu na waovu
 • wa mag 5.47 hivyo ni dhaifu mno na si msaada kwa mabaharia kama mwenzake Kutubu Polaris kwenye nusutufe ya kaskazini. Thumni ni kati ya makundinyota yaliyobuniwa
 • angakaskazi ya Dunia nyota hii ni moja kati ya mbili zinazosaidia kuikuta Kutubu Polaris ambayo ni nyota ya ncha ya kaskazini. Mtazamaji anaweza kufuata
 • Kwenye angakaskazi nyota hii ni moja kati ya mbili zinazosaidia kukuta Kutubu Polaris ambayo ni nyota ya ncha ya kaskazini. Mtazamaji anaweza kufuata
 • watu hao. Kumbe kwa Yesu lilikuwa dokezo la kwamba Mungu anawaalika wote kutubu na kuingia raha ya ufalme wake. Wakati huohuo aliita baadhi kumfuata kama