Back

ⓘ Mauzo
Mauzo
                                     

ⓘ Mauzo

Mauzo ni shughuli inayohusiana na kuuza au kiasi cha bidhaa au huduma zinazouzwa katika muda fulani.

Muuzaji humaliza kitendo cha uuzaji baada ya kujibu mwito wa ununuzi. Kuna kupitisha umiliki wa bidhaa na kulipa, ambapo kuna makubaliano ya bei ambayo italipiwa bidhaa ile. Muuzaji ndiye anayefanya tendo lile la uuzaji na uzo lile laweza kumalizika kabla ya mnunuzi kumaliza kulipa.

                                     

1. Ufafanuzi

Mtu au shirika linaloonyesha nia ya kupata bidhaa ya thamani inayotolewa linajulikana kama mnunuzi au mteja mtarajiwa. Kununua na kuuza ni lile tendo la kubadilishana umiliki. Kununua ni kupokea umiliki wa kinachouzwa ilhali kuuza ni kupitisha umiliki kwa mnunuzi baada ya malipo. Muuzaji na mnunuzi huafikiana ili kukamilisha ubadilishaji wa thamani.

Katika mauzo kunaweza kuwa na kujadiliana bei au bei inaweza kuwa isiyobadilika. Sanasana bei ya bidhaa au huduma hukuliwa na haja ya wanunuzi na wingi wake sokoni. Kwa biashara zinazolenga wanunuzi fulani, hasa matajiri, muuzaji anaweza kuiweka bei ya bidhaa bila kuzingatia bei ya ile bidhaa au huduma sokoni.

                                     

2. Mbinu

Mauzo yanaweza kuwa:

 • Ya kielektroniki
 • Ombi la pendekezo
 • Ya moja kwa moja
 • Biashara kwa biashara
 • Yasiyo ya moja kwa moja
 • Ya rejareja
 • Ya kupitia mawakala

Mawakala wa mauzo

Mawakala katika mchakato wa mauzo wanaweza kuwakilisha upande wowote; kwa mfano:

 • Wakala wa kuangalia shughuli tu
 • Msimamizi wa mauzo wa kutekeleza mikakati ya mauzo na kuratibu idara ya mauzo
 • Wakala wa mauzo kama vile kupitia mauzo shirikishi
 • Wataalamu wa mauzo mtandaoni
 • Wakala mnunuzi
 • Mfanyabiashara muuzaji
 • Wakala anayewakilisha pande zote mbili
 • Uwakilishi wa nje wa mambo ya mauzo

Aina za uuzaji

 • uso kwa uso P2P
 • uso kwa biashara P2B
 • biashara kwa biashara B2B

Aina za mauzo kijiografia

 • mauzo ya ndani
 • mauzo ya kimataifa
 • mauzo ya nchi
 • mauzo ya serikali