Back

ⓘ Gharama
Gharama
                                     

ⓘ Gharama

Gharama ni thamani ya pesa ambayo imetumiwa ili kupata kitu au kutoa huduma, na hivyo haipatikani kwa matumizi tena.

Katika biashara, gharama inaweza kuwa ile ya ununuzi: katika kesi hiyo kiasi cha fedha kilichotumiwa kupata kitu huhesabiwa kama gharama. Katika kesi hii, pesa ni pembejeo ambayo imekwenda ili kupata kitu.

Gharama ya upatikanaji inaweza kuwa jumla ya gharama za uzalishaji kama inavyotokana na mtayarishaji wa awali, na gharama zaidi za manunuzi ya malighafi.

Kwa kawaida bei ya kuuzia inalenga faida juu ya gharama za uzalishaji.