Back

ⓘ Mtihani
                                     

ⓘ Mtihani

Mtihani ni njia ambayo mtu anapimwa kutokana na alichokisoma au alichofundishwa ili atambuliwe kwamba alielewa au hakuelewa. Au ni kipimo cha maisha kutokana na ulichojifunza.

Katika shule mwanafunzi hupimwa na walimu wake juu ya kile walichomfundisha ili kumjua kama anaelewa au haelewi. Ili tufaulu mitihani tunatakiwa tusome sana na kwa bidii kubwa.

Hivyo mitihani yaweza kuwa migumu au rahisi kutokana na mwanafunzi mwenyewe: kama huwa hajisomei ataiona migumu na kama anajisomea ataiona rahisi hata kama mwalimu alitunga migumu kiasi gani. Kama tujuavyo, lengo la mtihani kwa mwanafunzi ni kumpima kile alichojifunza kutoka chanzo cha mafunzo yake, baada ya kipimo hicho ndipo mwanafunzi anaweza kufanyiwa tathmini ya kumjua kama anafaa kwa lipi na hafai kwa lipi.

                                     

1. Aina za mitihani shuleni

Kitaaluma, hasa katika masuala ya shule, mwanafunzi anaweza kupimwa katika vipindi vikuu vitatu:

 • Katikati ya masomo au mafunzo: Mara nyingi katikati ya masomo au mafunzo husika mwanafunzi hutahiniwa ili kupima uwezo wake wa kile au yale anayojifunza. Mitihani ya namna hiyo huweza kutolewa kwa ratiba za shule au taasisi husika au mwalimu wa somo anaweza kutoa mitihani ili kupima uwezo wa wanafunzi wake. Mitihani ya namna hiyo ni muhimu sana, kwani humsaidia mwalimu kuelewa uwezo wa mwanafunzi wake na hata mwanafunzi mwenyewe kujitathmini kiwango cha uelewa wake. Katika mitihani asilimia kubwa ya wanafunzi huwa na woga, ndiyo maana hupewa mitihani shuleni ili waizoee. Katika shule huwa na mashindano ya wanafunzi ili waweze kumpata wa kwanza kati yao. Mitihani hutungwa na walimu wenyewe. Huwa na mtihani wa wiki, mwezi, robo mhula, nusu mhula na mtihani wa mwisho.
 • Kabla ya kujiunga na shule au taasisi: Hiki ni kipindi ambacho mtahiniwa hupimwa kwa kutolewa mtihani ili kutambuliwa uwezo wake wa kujiunga na shule au taasisi hiyo. Mara nyingi kila shule ina utaratibu wa kumchukua mwanafunzi kutokana na kiwango cha uelewa kwa kutumia alama za maswali zilizowekwa na shule au taasisi hiyo. Ikiwa mtahiniwa atafanikiwa kupata alama zilizowekwa na shule au taasisi husika mtahiniwa huyo ataruhusiwa kujiunga nayo. Mitihani ya namna hiyo wengi huiita usaili.
 • Mwisho wa masomo/mafunzo: Mara baada ya kumaliza masomo au mafunzo mwanafunzi hupewa mtihani ili kumpima juu ya yale yote aliyojifunza. Kwa baadhi ya nchi au nchi nyingi duniani hutumia mitihani ya mwisho kama ni upimaji utakaomwezesha mwanafunzi kupata cheti cha kuhitimu mafunzo yake. Mara nyingi, kushindwa kwa mtihani wa mwisho ni kushindwa kwa masomo yake. Mitihani ya namna hiyo hutolewa na taasisi maalumu kama vile Baraza la Mitihani la Taifa kwa nchi ya Tanzania na taasisi nyingine zenye dhamana ya kufanya hivyo. Nchini Tanzania kuna mtihani wa taifa: mtihani huo humvusha mwanafunzi katika daraja alilopo na kwenda katika hatua nyingine kutoka shule ya msingi kwenda sekondari, kutoka sekondari kwenda chuo kikuu na hatimaye kufaulu na kutimiza malengo yake.
                                     

2. Sifa za mwanafunzi

 • Mwanafunzi anatakiwa afanye kazi alizopewa kwa muda aliopangiwa bila kuchelewa.
 • Ajenge ushirikiano na wenzake katika kufanya kazi walizopewa
 • Kama amepewa mtihani asimsaidie/asisaidiwe maana ni kipimo cha uelewa wao
 • Anatakiwa kuwaheshimu walimuj na wanafunzi wenzake ili ajenge upendo baina yao
 • Mwanafunzi kama hajaelewa anatakiwa kuuliza bila ya kuogopa kupigwa

Mwanafunzi akifaulu mtihani tunasema kuwa alielewa na hupewa zawadi na walimu na wazazi nyumbani kama pongezi, hivyo basi mwanafunzi anapopewa zawadi hujijengea kwamba ili apewe zawadi inambidi asome kwa bidii sana.

                                     
 • ya maksi kwenye mtihani ni 250. Sheria inasema ya kwamba 65  ni sharti kwa kupita. Je, maksi ngapi zinahitajika ila kupita mtihani huu? Jibu: Jumla
 • nchini Kenya. Baadhi ya mitihani inayopeana ni: Mtihani wa Kitaifa wa Shule za Msingi KCPE Huu ni mtihani ambao hufanywa baada ya mwnanafunzi kumaliza
 • shahada ambayo huchukuliwa baada ya mtu kukamilisha elimu ya sekondari. Mtihani wa kwanza ulifanyika mwaka wa 1989 wakati uo huo ukiwa mwisho wa Kenya
 • QT au qt ni kifupi cha: Qualifying Test Mtihani wa maarifa Kodi ya IATA ya Tampa Cargo, Kolumbia
 • Alikuwa mtoto wa mkulima aliyeendelea kusoma uhandisi akafaulu kupita mtihani kwa shule ya wanaanga mwaka 1962. Tar. 16 Juni 1963 alirushwa kwa chombo
 • jina la jaribio linalofanywa ili kupima ujuzi wa mtu katika jambo fulani na kumuandaa kufanya vizuri zaidi mtihani wa siku za mbele. Mazoezi ya mwili
 • imepata matokeo bora kwenye mtihani wa KCSE. Mara nyingi shule hii huwa kati ya shule kumi ambazo zinaongoza nchi katika mtihani huu. Wasichana wa Precious
 • ya Taifa ya Kiingereza na wanafunzi kufanya mtihani wa N.C. wakiwa na umri wa miaka 7, 11 na 14, na mtihani wa IGCSE wakiwa na umri wa 16 na A Level
 • shule za nchi mbalimbali E ni maksi ya duni inayoonyesha mtu ameshindwa mtihani katika muziki E ni noti. Kwa magari E ni alama ya kimataifa ya gari kutoka
 • na uwezo wa wanafunzi. Ngazi ya juu inayopatikana katika mfumo huu ni mtihani unaoandaa kwa kuingia katika ngazi ya juu ya elimu kwenye vyuo na Chuo
 • kutokana na usawasaji kutolewa kwa baadhi za alama katika kila somo Mtihani huu hutumiwa kuamua shule ya sekondari ambayo kila mwanafunzi atajiunga