Back

ⓘ Ufunguo
Ufunguo
                                     

ⓘ Ufunguo

Ufunguo ni kifaa kinachotumika kufungulia au kufungia mlango, kufuli n.k.

Kwa sababu hiyo, mara nyingi huchukuliwa kama ishara ya kumiliki nyumba, sanduku n.k. Mwambatanisho wa kufuli na ufunguo huchangia katika ulinzi kwa maana ni mwenye ufunguo peke yake anayeweza kufungua kitasa au kufuli.

                                     

1. Historia ya ufunguo

Historia ya ufunguo inafanana na ile ya kufuli maana zote zilitengenezwa kwa pamoja. Kufuli na ufunguo wa kwanza zilipatikana kule Ninawi, Assyria. Baadaye, mwambatanisho huo ulipatikana nchini Misri.

Baada ya mfumo huu wa ulinzi kuitikiwa na wote, uvumbuzi uliendelezwa na teknolojia pia kutumika katika kuboresha kufuli na funguo.

Leo, funguo za kisasa zahitilafiana sana na zile za zamani. Hata hivyo, minajili ni ilele: ulinzi.

                                     

2. Funguo za kisasa

Funguo za leo zina ulinzi mwingi kuliko ule wa zamani. Wezi waliweza kufungua na kuingia kwenye nyumba za kufuli za kitambo maana zilitengenezwa kwa teknolojia dhaifu.

Hivi leo, teknolojia ni nzuri na ni vigumu hata kama bado itafanyika kufungua kufuli kwa ufunguo usiodhaminiwa kufanya hivyo. Pia kuna teknolojia ambayo inazuia mtu kutengeneza nakala ya ufunguo bila ruhusa ya mwenye ufunguo.

Pia kumekuwa na kufuli zisizohitaji ufunguo wa kawaida bali tu kubofya nambari. Milango hii ni kama ile ya karakana za gari, ya milango ya nyumba na kampuni.

Kuna milango pia ambayo hufunguliwa kwa njia ya kieletroniki baada ya kutambua anayejaribu kufungua.

                                     

3. Funguo na taaluma ya lokismithi

Upotevu wa funguo au kuvunjika kwa funguo hufanya mtu ateseke sana akijaribu kuufungua au hata kuuvunja mlango. Kwa kuepuka hii shida, watu wengi huona heri waende kwa walio na taaluma ya lokismithiambayo ni taaluma ya kutengeneza funguo, kufuli na usalama wote wa kinyumbani. Lokismithi hawa huweza kuifungua ile milango kwa kutengeneza funguo badala au kuikata kufuli.

                                     
 • Katika utarakilishi, ufunguo programu kwa Kiingereza: product key au software key ni neno la siri linalotumika ili kuamilisha programu moja. Kahigi
 • kali na pia kuibwa. Kufuli za karakana huweza kufunguliwa bila kutumia ufunguo wa kawaida. Kufuli hizi hufunguliwa kwa kubofya nambari kwa kibodi au hata
 • Misemo huunganisha dhana au mawazo mawili kuwa moja. Mifano: Elimu ni ufunguo wa maisha Mtu ni afya Heshima ya mtu ni utu Mtu kwao Maji ni uhai Hasara
 • ndogo ya kampaundi ya kemikali ambayo bado ina sifa za kampaundi maalum. Kuelewa muundo wa atomu ni ufunguo wa masomo kama fizikia, kemia, biolojia n.k.
 • zilipatikana baadaye nchini Misri ambazo zilikuwa na komeleo, kipande cha mbao na ufunguo wa kufungulia kufuli. Kufuli ya kwanza ya chuma ilitengenezwa na mvumbuzi
 • maskini serikali zinatakiwa kuongeza mikopo kwa wanafunzi wa vyuoni ili waweze kupata elimu hiyo na kusonga mbele, kwa kuwa elimu ni ufunguo wa maisha.
 • watoto, vijana, watu wazima hata wazee. Pia unaweza ukasema kwamba elimu ni ufunguo wa maisha ukimaanisha kuwa elimu ndiyo kila kitu kwenye maisha ya mwanadamu
 • kulingana na spishi. Kichwa kina umbo wa mshale na mboni zina umbo wa tundu la ufunguo Rangi yao ni kijivu au kahawia lakini kichwa ni kijani kabisa au juu yake
 • Konklevu kutoka Kilatini cum clave yaani kwa ufunguo kupitia Kiingereza conclave ni mkutano maalumu ya makardinali wote wenye umri chini ya
 • kitasa linalopatikana katika jengo la posta. Linakodiwa na mteja anayepokea ufunguo wa sanduku. Kila sanduku huwa na namba yake na namba hiyo ni anwani yake
 • muhtasari wa uhusiano wa Lorenzo na sanaa. Peter Barenboim, Michoro ya Michelangelo - Ufunguo wa Tafsiri ya Medici Chapel Moscow, Letny Sad, 2006
 • ajifunze kuishi kama mama mwenye VVU. Mpango wa uzazi unaonyeshwa kama ufunguo wa afya na maendeleo ya jamii. Ila, kwa kawaida, mwanamke hawezi kujadili