Back

ⓘ Forbes
Forbes
                                     

ⓘ Forbes

Forbes ni gazeti la kibiashara la Marekani ambalo huchapishwa mara mbili kwa wiki, huku likiangazia masuala ya fedha, viwanda, uwekezaji na masoko. Forbes pia humulika mambo yanayoendana na hayo, yakiwamo masuala ya teknolojia, mawasiliano, sayansi, siasa na sheria. Washindani wao katika biashara ya magazeti kitaifa ni pamoja na Fortune na Bloomberg Businessweek.

Gazeti hili hujulikana sana kwa kutoa takwimu, orodha na madaraja ya vitu/mambo mbalimbali kama vile takwimu ya Orodha ya watu tajiri zaidi nchini Marekani the Forbes 400 na madaraja ya makampuni makubwa zaidi duniani the Forbes Global 2000. Orodha nyingine maarufu iliyowahi kufanywa na Forbes ni orodha ya mabilionea wakubwa zaidi duniani The Worlds Billionaires.

Kaulimbiu ya gazeti la Forbes ni The Capitalist Tool na mhariri mkuu chief editor wake ni Steve Forbes, na mkurugenzi Chief executive officer wake ni Mike Perlis.

Makao makuu yake yapo katika jiji la Jersey City, New Jersey, lakini ilitangazwa mnamo 18 Julai 2014 kwamba wanahisa wakubwa wa gazeti hilo ni kutoka Hong Kong, China.