Back

ⓘ Towashi
Towashi
                                     

ⓘ Towashi

Towashi ni mwanamume asiyeweza tendo la ndoa, kwa mfano yule aliyehasiwa.

Katika historia ilitokea mara nyingi na kwa sababu mbalimbali kwamba watu wa namna hiyo walihitajiwa, kwa mfano ili kutunza wake wa mfalme, kufanya kazi kama mtumwa bila kuzaa watoto, kubaki na sauti ndogo ya kabla ya ubalehe ili kuimba vizuri, n.k.

Siku hizi watu wanakubaliana katika kulaani upasuaji kama huo kwa kuwa ni kinyume cha hadhi ya binadamu ambaye ni haki yake ya msingi kuwa na mwili mtimilifu na kutofanywa chombo cha wengine.

Katika Injili Math 19:12, Yesu alifananisha watu ambao kama yeye kwa ajili ya ufalme wa Mungu wanajinyima kwa hiari ndoa na uzazi na matowashi waliozaliwa na ubovu katika viungo vya uzazi na wale waliohasiwa. Sababu ni kwamba uamuzi wao wa moja kwa moja unawanyima tunu hizo, hivyo ni sadaka ambayo wanamtolea Mungu ili kueneza zaidi utawala wake.

Ingawa katika Agano la Kale matowashi hawakuruhusiwa kujiunga na dini ya Israeli, Isaya wa Tatu alitabiri kwamba siku za mbele hali yao itakuwa tofauti.

Hivyo katika Matendo ya Mitume sura ya 8 inasimuliwa jinsi Towashi Mwethiopia alivyobatizwa na Filipo mwinjilisti.

Nukuu kutoka katika Mathayo 19:12

"Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee." Mathayo 19:12 SUV

                                     

1. Marejeo

 • Keay, John 2010. China: A History. HarperCollins UK. ISBN 0007372086. Retrieved on 5 September 2013.
 • Tsai, Shih-Shan Henry 1996. The Eunuchs in the Ming Dynasty Ming Tai Huan Kuan, illustrated, SUNY Press. ISBN 0791426874. Retrieved on 5 January 2013.
 • Tuotuo. Liaoshi Archived Septemba 25, 2018 at the Wayback Machine.
 • 2011 The Tongking Gulf Through History, illustrated, University of Pennsylvania Press. ISBN 0812243366. Retrieved on 4 January 2013.
 • Lary, Diana 2007. in Diana Lary: The Chinese State at the Borders, illustrated, UBC Press. ISBN 0774813334. Retrieved on 4 January 2013.
 • 2000 Notable Women of China: Shang Dynasty to the Early Twentieth Century, illustrated, M.E. Sharpe. ISBN 0765619296. Retrieved on 5 September 2013.
 • English translation of Rudople Guillands essay on Byzantine eunuchs "Les Eunuques dans lEmpire Byzantin: Étude de titulature et de prosopographie byzantines", in Études Byzantines, Vol. I 1943, pp. 197–238 with many examples
 • Bauer, Susan Wise 2010. The History of the Medieval World: From the Conversion of Constantine to the First Crusade, illustrated, W. W. Norton & Company. ISBN 0393078175. Retrieved on 5 September 2013.
 • McMahon, Keith 2013. Women Shall Not Rule: Imperial Wives and Concubines in China from Han to Liao. Rowman & Littlefield Publishers. ISBN 1442222905. Retrieved on 5 September 2013.
                                     

2. Viungo vya nje

 • 38 rare pictures of eunuchs during Qing Dynasty
 • The Eunuch Archive
 • The Ancient Roman and Talmudic Definition of Natural Eunuchs
 • Long-Term Consequences of Castration in Men: Lessons from the Skoptzy and the Eunuchs of the Chinese and Ottoman Courts, The Journal of Clinical Endocrinology & Metabolism December 1, 1999 vol. 84 no. 12 4324-4331 Archived Septemba 6, 2012 at the Wayback Machine.
 • The Perfect Servant: Eunuchs and the Social Construction of Gender in Byzantium
 • "Born Eunuchs" Home Page and Library
 • Eunuchs in Pharaonic Egypt
 • Hidden Power: The Palace Eunuchs of Imperial China Archived Julai 27, 2008 at the Wayback Machine.
 • The Eunuchs of Ming Dynasty China