Back

ⓘ Hoteli
Hoteli
                                     

ⓘ Hoteli

Hoteli ni jengo kubwa lenye vyumba vingi, ambapo watu wanaweza kulala wakati hawapo nyumbani.

Wenye sehemu hizo wanakodisha chumba kwa siku yoyote. Wanatoa vyumba vya kulala, na kwa kawaida hata chakula, hatimaye kwa ajili ya huduma hizo hutaka pesa, ambazo kiasi chake hutegemea ubora wa jengo.

Pia kuna hoteli ambapo mikutano hufanyika.

                                     

1. Aina za hoteli

Aina za hoteli hulinganishwa na wingi wa vyumba na eneo ambalo hoteli hupatikana.

  • Airport hotel ni aina ya hoteli ambazo hupatikana karibu kabisa na viwanja vya ndege na mara nyingi hutoa huduma zake kwa wasafiri wa ndege.
  • Inn hotel ni aina ya hoteli ambazo mara nyingi hutoa huduma za malazi na kifunguakinywa.
  • Motel hotel ni aina ya hoteli ambazo hupatikana karibu na barabara kubwa na huwa na vyumba vichache kutoa huduma sana kwa madereva wa magari ya watalii.
  • Resort hotel ni aina ya hoteli ambazo hupatikana karibu na mito, maziwa, milima, pembezoni mwa bahari au katika kisiwa,
                                     

2. Aina za vyumba vya hoteli

Aina za vyumba hutazamwa kulingana na aina au idadi ya vitanda vilivyomo ndani yake.

  • Double room ni aina ya chumba maalumu kwa ajili ya watu wawili na huwa na kitanda kimoja kikubwa.
  • Suite room ni aina ya chumba kikubwa kilicho na sehemu ya kulala pamoja na sebule.
  • Single room ni aina ya chumba maalumu kwa ajili ya kulala mtu mmoja tu
  • Twin bed ni aina ya chumba chenye vitanda viwili vilivyo karibu, wakati mwingine anaweza kulala mtu mmoja katika aina hii.