Back

ⓘ Chuo
                                               

Chuo Kikuu cha Maastricht

Chuo
                                     

ⓘ Chuo

Chuo ni taasisi ya elimu ya pekee. Inatoa mafunzo ya kazi fulani. Mifano ni chuo cha ufundi, chuo cha kilimo au chuo cha ualimu. Kwa kila namna chuo kinaanza kufundisha watu baada ya kumaliza ngazi fulani ya shule.

                                     

1. Asili na maana ya neno "chuo"

Kiasili maana ya neno "chuo" ilikuwa sawa na "kitabu". Kwa maana hiyo linatumiwa kwa mfano katika tafsiri za Biblia kama vile Injili ya Luka 4:17 "Yesu akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo".

Kutokana na maana hii asilia "chuo" kimekuwa pia neno la kutaja mahali pa kujifunza kusoma, kwa hiyo katika Kiswahili cha miaka iliyopita kiliweza kutaja pia shule.

Leo hii matumizi ya neno yamebadilika, kwa maana ya "kitabu" hupatikana tu katika matini zenye Kiswahili cha zamani na kama mahali au taasisi ya elimu kwa jumla, neno "shule, skuli" limechukua nafasi pana zaidi.

                                     

2. Viwango vya vyuo

Jina la "Chuo" linaweza kutaja taasisi zinazotoa elimu kwa ngazi tofauti sana. Hii itategemea na muundo wa elimu katika nchi mbalimbali.

 • Chuo cha ufundi stadi, kwa mfano useremala, mara nyingi kitafundisha wanafunzi waliotoka shule ya msingi na kuwafundisha ufundi fulani kama useremala, yaani matumizi ya vifaa vya fani hii na kuwawezesha kutengeneza fenicha au kushughulikia kazi zinazohusu matumizi ya ubao katika ujenzi.
 • Chuo cha uganga kinapokea watu waliomaliza shule ya sekondari na kuwapa elimu wa kuwa msaidizi wa mwuguzi au daktari aliyesoma tiba kwenye chuo kikuu "medical assistant".
 • Vyuo vingine vinaweza kuwapeleka wanafunzi wao hadi ngazi ya diploma au hata bachelor.
 • Katika nchi kadhaa chuo kinatoa elimu ya juu lakini katika fani moja tu, tofauti na chuo kikuu kinachofundisha fani mbalimbali na pia kuweka uzito kwenye uchunguzi wa kitaalamu, si mafundisho pekee.
                                     

3. Wanafunzi na walimu

Watu wanaoingia katika chuo kwa shabaha ya kujifunza huitwa wanafunzi, pia wanachuo au wanazuoni. Wale wanaotoa elimu huitwa walimu, kwenye ngazi za juu zaidi wanaweza kuitwa pia profesa au wakufunzi.

                                     

4. Vyuo nchini Tanzania

Nchini Tanzania vyuo huratibiwa na tume ya vyuo vikuu nchini humo inayoitwa TCU Tanzania commission for university. Tume ya vyuo vikuu Tanzania imeonyesha orodha ya vyuo nchini Tanzania kwamba mpaka mnamo waka 2019 Tanzania ilikua tayari na vyuo zaidi ya hamsini 50, Orodha ya vyuo vilivo idhinishwa ta tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania bofya hapa.

                                     
 • Chuo Kikuu ni taasisi ya elimu ya ngazi ya juu ambako wanafunzi wanafundishwa na wataalamu wa fani mbalimbali ambao hufundisha pamoja na kuendesha uchunguzi
 • Chuo Kikuu cha Dar es Salaam CKD kiingereza: University of Dar es Salaam ni chuo kikuu cha kwanza nchini Tanzania chenye kauli mbinu inayosema Hekima
 • Chuo Kikuu cha Nairobi UoN ni chuo kikuu kikubwa zaidi nchini Kenya. Ingawa historia yake kama taasisi ya elimu ilianza 1956, hakikufanya kuwa chuo
 • Chuo Kikuu cha Kenyatta 0704 143 990 kwa Kiingereza: Kenyatta University kilichoko katika mji wa Nairobi, Kenya, ndicho chuo kikuu cha umma cha pili
 • Chuo Kikuu cha Oxford kwa kifupi Oxford ni chuo kikuu cha utafiti nchini Ufalme wa Muungano, kilichoanzishwa mnamo mwaka 1096 katika Oxford, England
 • Chuo Kikuu cha Strathmore ni chuo cha kibinafsi mjini Nairobi, Kenya. Chuo cha Strathmore kilianzishwa mwaka wa 1961, kama chuo cha kiwango cha sita kinachofunza
 • Chuo Kikuu cha Kyambogo ni chuo kikuu cha umma nchini Uganda. Kilianzishwa mwaka wa 2001 kama chuo kikuu cha tatu cha umma nchini Uganda. Kampasi ya chuo
 • Chuo Kikuu cha Göttingen ni chuo kikuu nchini Ujerumani, kilichoanzishwa mnamo mwaka 1734 katika Göttingen, Saksonia Chini. Tovuti rasmi ya Chuo Kikuu
 • Chuo Kikuu cha Cambridge ni chuo kikuu nchini Ufalme wa Muungano, kilichoanzishwa mnamo mwaka 1209 katika Cambridge, England. Tovuti rasmi ya Chuo Kikuu
 • Chuo Kikuu cha Princeton huhesabiwa kati ya vyuo vikuu bora nchini Marekani. Kiko katika jimbo la New Jersey. Kilianzishwa mwaka 1746 kwa jina la College