Back

ⓘ Mtaala
Mtaala
                                     

ⓘ Mtaala

Mtaala ni mpangilio wa mambo ambayo mwanafunzi anatarajiwa kusaidiwa kujua hatua kwa hatua.

Mtaala unaweza kupanga hata ushirikiano unaotarajiwa kati ya mwalimu na wanafunzi wake ili kufikia shabaha za shule au chuo.

Nchi nyingi zina mitaala iliyopangwa kikamilifu kwa ngazi zote za elimu.

Baadhi inamuachia mwalimu nafasi kubwa zaidi ya kuona mwenyewe la kufundisha kadiri ya mahitaji ya wanafunzi wake.

Ofisi ya Kimataifa ya Elimu chini ya UNESCO ndiyo yenye jukumu hasa la kupitia mitaala na utekelezaji wake duniani kote.

                                     

1. Mtaala na falsafa ya nchi

Mitaala ni jumla ya mipango na uzoefu ulioratibiwa kwa ajili ya mafunzo ya aina fulani yenye malengo maalumu kwa wanafunzi. Mipango hiyo inaweza kuwa ni mambo, matendo na uzoefu wa aina yoyote ile ambayo wanafunzi wanapata chini ya uongozi na usimamizi wa shule. Hutegemea falsafa ya nchi na siasa inayoiongoza.

Mfano: nchini Tanzania falsafa ya nchi ni: Ujamaa na Kujitegemea kutokana na siasa iliyokuwa ikiongoza chini ya Mwalimu Julius K. Nyerere. Falsafa ya elimu ni: Elimu ya Kujitegemea inatokana na falsafa ya nchi. Madhumuni/Malengo Makuu ya Elimu nchini yameanishwa katika Sera ya Elimu ya Taifa na katika mihtasari ya masomokwa kila ngazi

Bila mwongozo wa falsafa ya nchi na madhumuni ya elimu kitaifa wakuza mitaala watakosa mwelekeo maalumu wa ukuzaji mitaala. Hivyo ina hatari ya kufanya mtaala uwe mkusanyiko wa mambo yasiyokuwa na mwelekeo maalumu kitaifa. Madhara yake ni watumiaji kukosa mwelekeo na msimamo maalumu unaolingana na mwelekeo wa kitaifa.

                                     

2. Sifa za mtaala

 • Kwa kawaida mtaala huzingatia taaluma maarifa ufundishaji matendo na kujifunza uzoefu katika kiwango au ngazi fulani ya elimu.
 • Muda utakaotumika kufundisha mtaala huo, kwa mfano miaka miwili saba na minne mitatu mitano n.k)
 • Pia mtaala lazima uonyeshe walengwa wa mtaala aina ya wanafunzi watakaotumia mtaala huo, kwa mfano chekechea, watoto wa shule za msingi na sekondari na walemavu
 • Sifa za walimu watakaofundisha mtaala huo mfano walimu wenye daraja A stashahada na shahada.
 • Vifaa vitakavyotumika kufundishia walengwa na njia na mbinu zitakazotumika kupima maendeleo ya wanafunzi na ubora wa mtaala.

Kwa hiyo mtaala ni jumla ya mpango uliondaliwa kwa ajili ya kufundishia na kujifunza kwa lengo la kuwapatia walegwa maarifa,stadi na mielekeo mbalimbali. Nguzo kuu ya mtaala ni muhtasari ambayo hutumika katika kutekeleza mtaala huo.

Muhtasari: Ni mkusanyiko wa mada zinazokusudiwa ili kukamilisha kiwango fulani cha elimu, kazi au mafunzo maalumu.Katika shughuri za wakuza ukuzaji mitaala, wakuza mitaala wanapaswa kuongozwa na malengo makuu ya elimu yanayowekwa kitaifa.

                                     

3. Umuhimu wa kuwa na mtaala

 • Kuelekeza malengo makuu ya elimu katika jamii husika
 • Kuchukua taswira yote ya falsafa ya elimu ya nchi inayohusika.
 • Kuwa dira na mwongozo muhimu kwa walimu katika ufundishaji
 • Kutaja na kuelekeza nyenzo na vifaa vya kufundishia
 • Kuwezesha kurekebisha na kuendeleza elimu
 • Kudhibiti mfumo wa elimu
 • Kuongoza walimu katika ufundishaji ili wasitoke nje ya malengo makuu ya elimu na falsafa ya nchi
 • Kuweka malengo muhimu yaliyo kusudiwakufikia katika ufundishaji
                                     

4. Matumizi ya mtaala

 • Kusaidia walimu na wanafunzi kutambua malengo makuu yanayo kusudiwa kufikiwa katika utoaji wa elimu
 • Kumsaidia mwalimu kutambua na kuchagua njia za kufundishia zinazofaa ili aweze kufikia malengo aliyojiwekea
 • Kufahamisha mwalimu na mwanafunzi kuhusu masomo au mada atakazo fundishwa ili kufikia malengo aliyojiwekea
 • Kumwelekeza mwalimu kuhusu njia atakazopima maendeleo ya wanafunzi na ubora wa mtaala wenyewe.
 • Kumsaidia mwalimu na mwanafunzi kuchagua na kufaragua vifaa vya kufundishia na kujifunzia mada mbalimbali
                                     

5. Aina za mitaala

 • Mtaala usiyo rasmi
 • Mtaala rasmi
 • Mtaala ficho

Mtaala rasmi

Ni mkusanyo wa mambo yote anayopaswa kuyafanya na kuyafahamu mwanafunzi anapokuwa darasani. Au ni mtaala uliopangwa kwa madhumuni ya kumfundisha mwanafunzi katika mfumo rasmi wa elimu.

Mapungufu ya mtaala rasmi

 • Humfanya mwanafunzi ashindwe kufanya mambo yote yaliyo nje ya darasa kama vile ufugaji uvuvi, mila na desturi ya jamii yake.

Mapungufu

 • Mwanafunzi hukosa ujuzi wa maarifa yaani mambo yote yanayofundishwa darasani katika mtaaala rasmi.
                                     

5.1. Aina za mitaala Mtaala rasmi

Ni mkusanyo wa mambo yote anayopaswa kuyafanya na kuyafahamu mwanafunzi anapokuwa darasani. Au ni mtaala uliopangwa kwa madhumuni ya kumfundisha mwanafunzi katika mfumo rasmi wa elimu.

                                     

5.2. Aina za mitaala Sifa za mtaala rasmi

 • Huweka bayana njia ambazo mwalimu atatumia kufundishia
 • Huweka wazi malengo ya kufundisha mtaala
 • Huweka wazi aina ya walengwa
 • Huainisha na kuweka wazi mambo, matendo na uzoefu wa aina yoyote ile ambayo mwanafunzi ataupata chini ya uongozi na usimamizi wa shule yaani taaluma ufundishaji na kujifunza katika kiwango fulani cha elimu
 • Huweka wazi mambo, matendo na uzoefu ambao mwanafunzi ataupata chini ya uongozi wa shule au chuo
 • Huwa na muda maaalumu wa kutekelezwa
 • Huonyesha vifaa vitakavyo tumika kufundishia mtaala
 • Huweka bayana njia za kupima maendeleo ya mwanafunzi
                                     

5.3. Aina za mitaala Faida za mtaala rasmi

 • Kupunguza tofauti zinazoweza kutokea iwapo kila shule au jamii itajitungia mtaala wake
 • Huweka bayana utaratibu wa kutahini na sifa za wale watakaofuzu baada ya kufundishwa na kutahiniwa kwa kuutumia mtaala husika.
 • Kurahisisha kuandaa vifaa vya kujifunzia
 • Kurahisisha ufuatiliaji na upimaji wa maendeleo ya wanafunzi
                                     

5.4. Aina za mitaala Mapungufu ya mtaala rasmi

 • Humfanya mwanafunzi ashindwe kufanya mambo yote yaliyo nje ya darasa kama vile ufugaji uvuvi, mila na desturi ya jamii yake.
                                     

5.5. Aina za mitaala Sifa za mtaala usio rasmi

 • Mada au mambo anayofundishwa zinalenga kumpatia mwanafunzi maarifa na stadi za kutatua matatizo aliyo nayo kwa wakari ule
 • Hutokana na jamii au mazingira anayoishi mwanafunzi
 • Hukazia maarifa na stadi zinazo lenga kutatua matatizo yanayokabili jamii husika
 • Mwanafunzi anaweza kupata maarifa na stadi bila kuwa chini ya usimamizi wa shule au chuo.
 • Kwa kawaida haupangwi na kuratibiwa na njia kwa njia zilizo rasmi
 • Unaweza ukakoma mara matatizo yanapomalizika
                                     

5.6. Aina za mitaala Mapungufu

 • Mwanafunzi hukosa ujuzi wa maarifa yaani mambo yote yanayofundishwa darasani katika mtaaala rasmi.
                                     

5.7. Aina za mitaala Mtaala ficho

Mtaala huu unajumuisha matendo yote yanayosaidia ujifunzaji usiokusudiwa au usioratibiwa. Kwa mfano ujifunzaji wa utii kwa mamlaka, kuwahi/kujali muda, usafiri nakadhalika. Yaani unajumuisha mambo yote ambayo hayaonekani kwenye muhtasari wa shule kama sehemu ya mtaala.

                                     

6. Vipengele vya mtaala

Katika mtaala vipengele vilivyo muhimu ni vitano ambavyo hufanya kazi kwa ushirikiano na kwa kutegemeana:

 • Maudhui
 • Malengo ya mtaala
 • Njia za kufundishia
 • Zana
 • Tathmini

Vipengele hivi vitano hufanya kazi kwa ushirikiano na kwa kutegemeana kama viungo vya mwili wa binadamu. Ni vigumu kuvitenganisha ila kwa faida ya kujifunza na kuelewa kwa undani, tutavitazama kimoja katika maelezo.

                                     

7. Malengo ya mtaala

Malengo ni matokeo au matarajio yanayotarajiwa kupatikana kutokana na mpango/programu fulani. Mtaala wowote ule lazima uwe na malengo. Katika uwanja wa elimu, malengo ya mtaala ni mabadiliko ya tabia na mwenendo wyanayotarajiwa kupatikana kwa wanafunzi baada ya kupata programu fulani ya mafunzo.

                                     

7.1. Malengo ya mtaala Umuhimu wa malengo ya mtaala

Malengo kama kipengele cha msingi cha mtaala yana umuhimu mkubwa kwani:

 • Huwa ni msingi wa malengo katika ngazi/kiwango vyote vya elimu-elimu ya msingi, sekondari na vyuo
 • Huwa ni msingi wa vipengele vingine vyote viine vya maudhui ya mtaala
 • Huwa ni msingi wa shughuri za kazi za wakuza mitaala. Wakaguzi na walimu, wanafunzi na watawala wa elimu.
                                     

7.2. Malengo ya mtaala Malengo ya jumla na malengo mahususi

Malengo ya jumla ni matarajio au mabadiliko kitabia ambayo tunatarajia kuyaona kwa mtu ambae amepata elimu.Malengo ya jumla ni malengo na madhumuni ya elimu kitaifa yaliyokusudiwakutimizwa na program mbalimbaliza mafunzokatika viwango mbalimbali vya elimu. Kimsingi malengo haya yanatokana na sera ya elimu katika nchi husika.

Baadhi ya malengo ya kitaifa ni

 • Kukuza ari ya Watanzania ili wapende kuthamini utamaduni, mila na desturi za nchi
 • Kuendelezana kukuza ndani ya Watanzania moyo wa kujiamini na tabia ya kisayansi, uelewa wao na kuuheshimu.
 • kuongoza kuendeleza na kukuza vitu na uwezo wa watanzania ili waweze kutumia rasilimali zilizopo kuleta maendeleo yao binafsi na kwa Taifa zima
                                     

7.3. Malengo ya mtaala Sifa za malengo ya jumla

 • Huchukua muda mrefukukamilika. Mfano hadi mwisho wa programu
 • Huchukua vitendo kama kujua, kufahamu n.k.
 • Siyorahisi kuyapima kwa sababu hayako wazi
                                     

7.4. Malengo ya mtaala Malengo mahususi

Malengo mahususi ya mtaala hutokana na malengo ya jumla. Haya ni malengo yaliyokusudiwa kutimizwa na programu mbalimbali za mafunzo katika viwango mbalimbali vya elimu.

Ni kutokana na malengo mahususi kila kiwango cha ngazi fulani ya elimu ndiyo yanapatikana mahususi yanayowaongoza walimu katika kuandaa maazimio yao wanayofundishia darasani.

Maudhui haya ndio yawezayo kumuongoza mwalimu kutoa maarifa na stadi ambazo zinaweza kubadili tabia ya mwanafunzi ambayo inaweza kupimika.

Kwa mfano tunapofundisha somo la Hisabati,tunatarajia kuona mabadiliko fulani katika tabia ya mtoto kutokana na kujifunza somo zima au mada fulani. Mabadiliko hayo yanaweza yakawa maarifa,stadi au mwelekeo mwanafunzi anaouonyesha kutokana na kujifunza somo la Hisabati ambao hakuwa nao kabla ya kujifunza somo hilo.

Tunaweza kugawa malengo mahususi katika Nyanja tatu ambazo ni

 • Stadi
 • Utambuzi
 • Mwelekeo


                                     

7.5. Malengo ya mtaala Sifa za malengo mahususi

 • Ni rahisi kupima kufanikiwa au kutofanikiwa kwake
 • Huumia vitendo kama fafanua,taja,eleza n.k.
 • Ni malengo yaliowazi
 • Hutumia muda mfupi wa ukamilishaji wake
                                     

8.1. Maudhui Misingi/vigezo vya kuchagua maudhui ya mtaala

 • Mvuto: Maudhui yafaayo ni yaleyenye kuvutia na yenye kuamsha ari ya mwanafunzi ya kupenda kufahamu maudhui hayo.
 • Umuhimu: Maudhui yanayopewa kipaumbele ni yale yanayolingana hali halisi ya mausha ya jamii, uchumi wan chi inayohusika. Ni yale yenye umuhimu katika maisha ya walengwa.
 • Muda na idadi ya maada: Maudhui yazingatie muda wa program husika. Maudhui yanapoandaliwa huwakatika mfumo wamada kubwa na mada ndogo, kulingana na mfululizo huu unatakiwa uwe unaanzia na mada rahisina kuendelea hadi zile ngumu. Mpangilio wa aina hiyo ni muhimu kwani huhusishaujifunzaji na ufundishaji kulingana na umri wa wanafunzi.
 • Kufundishika: Maudhui yawe na uwezo wa kufunzika/kufundishika yaani yaendane na uwezo wa walengwa.
 • Njia na mbinu: Maudhui yazingatie mbinu na njia za kujifunzia na kufundishia
 • Uthabiti: Uwezo wa maudhui katika kutimiza malengo ya masomo katika kiwango husika.


                                     

9. Njia na mbinu

Ili kuweza kufanikisha tando zima la ufundishaji katika kufanikisha maudhui na malengo ya somo mwalimu hutumia vitendo mbalimbali vijulikanavyo kama njia. Na njia peke yake haiwezikufanikisha somo lazima isaidiwe na mbinu. Mbinu ni stadi maalumu inayobainisha ni jinsi gani ya kufundishia/kujifunzia itakvyowezeshwa katika tendo la kufundisha na kujifunza. Njia ni namna mwalimu anavyowasilisha mada katika mchakato mzima wa kufundisha.

Kuna njia mbili zinazoweza kutumika katika swala zima la kujifunzia na kujifunza:

 • Njia isiyo shirikishi
 • Njia shirikishi
                                     

9.1. Njia na mbinu Misingi ya kuchagua njia/mbinu

 • Mwalimu: Uwezo mwalimu katika kutumia nji/mbinu ujuzi na utaalamu wake.
 • Maudhui: Hali ya somo lenyewe na maarifa ambayo mwanafunzi wanafunzi wanatakiwa wayapate hivyo maudhui yanatakiwa yafundishike.
 • Malengo: Nini malengo ya wanafunzi wanatakiwa kufanikisha nini katika maisha yao? Njia/mbiu lazima zifanikishe malengo yaliokusudiwa.
 • Hali ya mwanafunzi: Umri wa mwanafunzi, kukomaa na kutokomaa kiakili, mazingira yao hivyo njia/mbinu ziendane na hali za walengwa.
                                     

10. Vifaa vya mtaala

Mtaala una vifaa vyake maalumu ambavyo vinatakiwa vitumike kwa usahihi ili kutekeleza mtaala kwa ufanisi. Vifaa hivyo ni:

 • Muhtasari
 • Vitabu vya kiada
 • Kiongozi cha mwalimu
 • Kitabu cha mwalimu na rejea
 • Vitabu vya ziada
                                     

10.1. Vifaa vya mtaala Muhtasari

Muhtasari ni mwongozo unaotaja kwa kifupi tu mambo yote yanayotakiwa yafundishwe katika mwaka mzima katika darasa fukani au kwa miaka kadhaa kwa kila darasa kwa mmpangilio maalumu.

                                     

10.2. Vifaa vya mtaala Muundo wa muhtasari

Muhtasari una sehemu kuu mbili:

 • Majedwali ya kutumia kufundishia: Hii ni sehemu ambayo huwa na maudhui ya somo husika yanayotakiwa kufundishwa kila mwaka. Majedwali ya kufundishia yana vipengele vikuu vilivyopangwa katika safukama ifuatavyo.
 • Utangulizi: Hii ni sehemu ambayohuelekeza sababu za kuwepo kwa muhtasari huo, muundo wake, malengo ya elimu katika kiwango husika na malengo ya kufundisha somo hilo katika kiwango hicho.
                                     

10.3. Vifaa vya mtaala Vipengele vya muhtasari

 • Vifaa /zana za kujifunzia na kufundishia
 • Mapendekezo ya njia za kufundishia na kujifunzia
 • Lengo la kufundishia mada hiyo
 • Mada kuu na mada ndogo
                                     

10.4. Vifaa vya mtaala Matumizi ya muhtasari

 • Kuongoza waandishi wa kitabu cha kiada,kiongozi cha mwalimu na vitabu vya rejea
 • Kutathmini mtaala baada ya kipindi maalumu cha matumizi ya muhtasari huo.
 • Kumwongoza mwalimu kuandaa maazimio ya kazi na maandalio ya masomo
 • Kuandalia mwongozo wa upimaji wa maendeleo ya wanafunzi kwa mwaka au kwa kipindi cha miaka kadhaa
 • Kuelekeza njia zifaazo katika kufundisha na kujifunzia
                                     

10.5. Vifaa vya mtaala Kitabu cha kiada

Ni kitabu ambacho kinafafanua mada zote za muhtasari kwa ukamilifu. Kitabu hiki ndicho kinachobeba maudhui ya somo kwa ukamilifu.Mfano vitabu malimbali vya masomo vilivyomo mashuleni.

                                     

10.6. Vifaa vya mtaala Sifa za kitabu cha kiada

 • Kiwe chenye lugha rahisi inayo eleweka kulingana na kiwango cha mwanafunzi
 • Kiwe na mada zinazopangwa kwa mtiririko wenye mantiki kuanzia mada kuanzia mada rahisi hadi zile ngumu
 • Kiwe na maelekezo na mazoezi yanayomshirikisha mwanafunzi katika kujifunza
 • Kiwe kinaendana na muhtasari pamoja na kiongozi cha mwalimu.
 • Kiwe na maandishi yanayosomeka kwa urahisi ya kuvutia
                                     

10.7. Vifaa vya mtaala Matumizi ya kitabu cha kiada

Mwalimu hukitumia kwa kuelekeza maarifa. Hutumiwa na mwanafunzi pia kwa kujikumbushia na kufanya marudio.

                                     

10.8. Vifaa vya mtaala Uchambuzi wa kitabu cha kiada

Vitabu vingi vya kiada vimeandaliwa katika mitindo tofautitofauti, hivyo ni jukumu la mwalimu w somo pengine akishirikiana na wanafunzi kuchagua kitabu kinachofaa. Ili kuweza kufanya uamuzi wa kitabu kinachofaa huna budi kuchambua kwa kuzingatia mambo yafuatayo: Kwa kiasi gani mada zote za muhtasari zimefafanuliwa kwa ufanisi pamoja na kuzingatia sifa za kitabu cha kiada.

                                     

10.9. Vifaa vya mtaala Kiongozi cha mwalimu

Hiki ni kitabu kinachompa mwalimu maelekezo ya mada ya kufundisha, jinsi ya kuifundisha, maudhui gani yafundishwe na kutumia vifaa au zana gani. Pia kinaitwa kitabu cha mwongozo kwa mwalimu.

                                     

10.10. Vifaa vya mtaala Umuhimu wa kitabu cha mwalimu

 • Humpa mwalimu maudhui na mifano ya ziada kuzidi kumpanua mawazo na upeo.
 • Humsaidia mwalimu kujijengea moyo wa kujiamini na hasa kama si mzoefu wa ufundishaji wa somo hilo
 • Humsaidia mwalimu katika kuandaa somo
 • Humweleza mwalimu jambo la kufanya la kufanya humpa dira au mwelekeo wa ufundishaji
                                     

10.11. Vifaa vya mtaala Dhana ya kitabu cha mwalimu

 • Kinaelezaa jinsi ya kutenda katika hatua zote tangua uandaaji wa somo, ufundishaji hadi upimaji
 • Ni mwongozo ambao unammpa mwalimu ujuzi wa ufundishaji.
 • Ni kitabu kinachotoa maelezo ya kina kuhusu ufundishaji wa somo fulani
                                     

10.12. Vifaa vya mtaala Sifa za kitabu cha mwalimu

 • Kina vitendo vyote ambavyo mwalimu hupaswa kutenda katika hatua za ufundishaji
 • Kinaeleza jinsi ya kutekeleza kazi ya ufundishaji hatua kwa hatua
 • Huweza kutumiwa na mwanafunzi pia
 • Hutoa ufafanuzi wa mada kwa kiwango cha juu zaidi ili kupanua mawazo ya mwalimu na kumuimarisha zaidi kitaaluma.
                                     

10.13. Vifaa vya mtaala Tofauti kati ya kitabu cha mwalimu na kiongozi cha mwalimu

 • Kitabu cha mwalimu humwelekeza hatua za kufuata katika kufundisha somo au kufanya jaribio fulani. Kiongozi cha mwalimu hupendekeza njia na mbinu mbalimbali za kufundisha somo.
 • Kitabu cha mwalimu huweza kutumiwa na mwanafunzi na mwalimu. Kiongozi cha mwalimu hutumiwa na mwalimu tu.
 • Kitabu cha mwalimu huhusika zaidi na mchakato au hatua za utendaji, kam vile utafitijaribio. Kiongozi cha mwalimu huhusika na jinsi ya kufundisha mada za masomo.kwa kawaida hutumika pamoja na kitabu cha kiada.
                                     

11. Vyanzo vya mitaala

Ni muhimu kujua vyanzo vya mtaala ili kuhakikisha vinahusishwa na kuzingatiwa wakati wa kuandaa mtaala. Vyanzo hivyo ni pamoja na

 • Wazazi
 • Siasa ya nchi
 • Waajiri
 • Wataalamu mbalimbali.
 • Jamii
 • Wanafunzi
 • Walimu
                                     

12. Marejeo

 • TET 1994, Ukuzaji mitaala na Kunasihi.KIUTA DSM

Wizara ya elimu na Utamaduni2005.mpango wa mafunzo ya walimu kazini Daraja la IIIC/B-A: Moduli ya soma la Mitaala. Wizara ya elimu na Utamaduni.

 • TET 2013, Moduli ya kujifunzia somo la ualimu. Taasisi ya Elimu Tanzania DSM. Retrieved on February 05.2014 from Http:www.luwingu.wordpress.com/Mitaala.
                                     
 • mwa tamthiliya zake, inayompa umaarufu zaidi ni Morani, pia riwaya ya Watoto wa Maman tilie ambavyo hutumika sana katika mtaala wa elimu ya Tanzania.
 • sanaa. Kwa kawaida ufundishaji huo unadai mwalimu aandae somo kwa kufuata mtaala fulani, kutoa vipindi na kutathmini maendeleo ya mwanafunzi. Pia ni muhimu
 • viwandani. Ili kuafikia mahitaji ya kazi, shule za upili zilijengwa na mtaala uliolenga maarifa ya kazi za ofisi na za sulubu ukazinduliwa. Hii ilibainika
 • mapana ya masomo maalum yakiwemo mpango wa mafunzo, teknolojia ya elimu, mtaala uliokuzwa, masomo yaliyopangwa, masomo maalumu, sayansi tambuzi na sayansi
 • viwandani. Ili kuafikia mahitaji ya kazi, shule za upili zilijengwa na mtaala uliolenga maarifa ya kazi za ofisi na za sulubu ukazinduliwa. Hii ilibainika
 • mtihani wa Uingereza wa GCSE na mtihani wa International GCE O level. IGCSE mtaala msingi au wa kupanuliwa huchukuliwa katika makundi ya masomo tano: lugha
 • umekanika, Uchoraji, Somo la Umeme, Kifaransa, Muzuki, Kijerumani na biashara. Mtaala huwapa wanafunzi wa huwapa wanafunzi fursa ya kuchagua masomo ambayo yatawafaidi
 • School na Shah Lalji Nagpar Academy. Wanafunzi katika shule hizi kufuata mtaala wa Uingereza. Utalii ni muhimu katika shughuli za kiuchumi Nakuru. Majaliwa
 • kati ya matano yafuatayo: Mtaala wa Kilimo, Mtaala wa Kijumla chaguo la Sanaa au Sayansi Mtaala wa somo la Biashara, Mtaala wa Ufundi Vocational Programme
 • kwanza wa kiafrika wa idara hiyo.Pia aliwahi kuwa mshauri wa ukuzaji wa mtaala haswa wakati chuo kikuu cha Uganda cha Kyambogo, kwa kushirikiana na shirika
 • kutoka kote nchini Kenya. Wanafunzi hushiriki kikamilifu katika shughuli mtaala mwenza na taasisi hii ina vilabu kadhaa. Mifano ni: ICL - NachaguaMaisha
 • daraja la juu, na miaka mitatu masomo ya chuo kikuu Shule zote zilifuata mtaala mmoja. Mwaka wa 1981, kamati iliyoteuliwa na rais kuratibu namna ya kuanzisha
 • za binafsi na za serikali, kuna tofauti katika kiwango cha uhuru katika mtaala wao, wigo wa msaada wa fedha toka kwenye kodi na ufadhili. Matumizi ya elimu