Back

ⓘ Mwalimu
Mwalimu
                                     

ⓘ Mwalimu

Mwalimu ni mtu anayesaidia wengine kupata ujuzi, maarifa na tunu.

Kazi hiyo inaweza kufanywa na yeyote katika nafasi maalumu, kwa mfano mzazi au ndugu akimfundisha mtoto nyumbani, lakini kwa wengine ndiyo njia ya kupata riziki inayomdai karibu kila siku kwa miaka mingi, kwa mfano shuleni. Huko mwalimu anatakiwa kuwa na shahada au stashahada, kadiri ya sheria za nchi na ya ngazi ya elimu inayotolewa.

                                     

1. Majukumu

Majukumu ya mwalimu yanaweza kutofautiana kadiri ya utamaduni husika.

Mara nyingi ni pamoja na kufundisha kusoma na kuandika, kuhesabu, kufanya kazi fulani ya mikono, kushirikiana katika jamii, kufuata dini, kuunda kazi za sanaa.

Kwa kawaida ufundishaji huo unadai mwalimu aandae somo kwa kufuata mtaala fulani, kutoa vipindi na kutathmini maendeleo ya mwanafunzi. Pia ni muhimu atunze nidhamu.

Nje ya madarasa, pengine mwalimu anatakiwa kuongoza wanafunzi wake katika safari za kutembelea mashamba, viwanda, kumbi, makumbusho, n.k.

                                     

2. Sifa zinazohitajika

Ualimu si kazi ngumu sana, kwa sababu unahusika na mambo mengi.

Umoja wa Ulaya umetaja sifa tatu muhimu:

Uwezo wa kushirikiana na wengine Uwezo wa kutumia ujuzi, teknolojia na habari, na Uwezo wa kufanya kazi ndani na pamoja na jamii.

Wataalamu wa sayansi ya elimu wanazidi kukubaliana kwamba mwalimu yeyote anahitaji mambo matatu:

ujuzi vipaji na misimamo.
                                     
  • Ummy Ally Mwalimu alizaliwa 5 Septemba 1973 ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama tawala cha kisiasa Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti Maalum
  • Mwalimu wa Kanisa ni jina la heshima ambalo kwa nadra Kanisa Katoliki linampa mtakatifu ambaye katika maisha, mafundisho na maandishi yake alionyesha
  • Mwalimu Sikujua Mombasa, karne ya 19 - Mombasa, karne ya 19 alikuwa mshairi na mwandishi katika usultani wa Mombasa. Aliandika ushairi na hadithi zake
  • Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Butiama, Mkoa wa Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, 13 Aprili 1922 - London, Uingereza, 14 Oktoba 1999 alikuwa rais wa
  • Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere ni kitabu kilichoandikwa na Peter Bwimbo aliyekuwa mlinzi mkuu wa Mwalimu Julius Nyerere katika kipindi cha kabla ya uhuru
  • Kanuni ya Mwalimu kwa Kilatini Regula Magistri ni kanuni ya kitawa iliyoandikwa na mmonaki asiyejulikana mwanzoni mwa karne ya 6 katika Italia ya kati
  • mzizi wa neno jingine. Mifano zaidi Mimi ni mwalimu Sisi ni walimu Wewe ni mwalimu Ninyi ni walimu Yeye ni mwalimu Wao ni walimu Hizi ni mofimu tegemezi vipande
  • Mzee yupi anaumwa? Miti mingapi imekatwa? Unafanya kazi gani? Chakula kipi ni kitamu? Mwalimu yupi anafundisha vizuri? Lango: Lugha Vivumishi Viwakilishi
  • Edward Wilmot Blyden 1832 - 1912 alikuwa mwalimu mwandishi, balozi na mwanasiasa nchini Liberia. Alizaliwa visiwa vya Karibi. Aliandika kuhusu Muungano