Back

ⓘ Maisha
                                               

The O.C.

The O.C. ni kipindi cha Marekani kilichohusu maisha ya vijana iliyoonyeshwa kuanzia 5 Agosti 2003 hadi 22 Februari 2007 kwenye Stesheni ya Fox Broadcasting Company. Kipindi hiki, kilichobuniwa na Josh Schwartz, kinahusu maisha ya kundi la vijana na familia zao wanapoishi mtaani Newport Beach kwenye mji wa Orange County, California. The O.C. imeonyeshwa kwenye zaidi ya nchi 50 kote duniani na ilikuwa mojawapo ya vipindi maarufu mnamo 2003. The O.C. ilivutia watazamaji milioni 9.7 katika msimu wake wa kwanza, lakini watazamaji walianza kupungua katika misimu iliyofuatia.

                                               

Furaha

Furaha ni mojawapo kati ya maono ya msingi, pamoja na pendo, hamu, chuki, hofu, huzuni na hasira. Furaha inapatikana pale ambapo umepata kile ulichokipenda na ulichokuwa na hamu nacho. Neno hili tunaweza kutumia katika hali tofautitofauti. Wapo ambao watalitumia kama jina ila wengine ni hali ya kuwa na amani juu ya ufanyaji wa tendo fulani kwa kuwa hauwezi ukafanya kitu kwa furaha bila ya kuridhia mwenyewe au kuwa na amani nacho. Kwa kufanya hivyo unaweza ukafanya vibaya na kuharibu kabisa. Lakini kama umeridhia nacho, unaweza kufanya kitu hicho kwa umakini na kwa usahihi na unaweza kupend ...

                                     

ⓘ Maisha

Maisha ni muda ambao kiumbe hai anajaliwa kuishi. Ni hali tofauti kabisa na uzima wa milele, kwa kuwa uhai wake una mwanzo na mwisho.

Hasa mwisho unasababisha maswali: kama kila chenye mwanzo kina mwisho, ya nini kuwepo kwake? Kukosa lengo, kuwepo bure, kutokuwa na maana kunamfanya mtu ajisikie mnyonge, pengine akate tamaa ya kuishi, la sivyo ajitose kufurahia mazuri yanayopatikana maishani, lakini bila uwezo wa kuondoa moyoni ule utupu wa maana unaomtia huzuni ya dhati.

Ndiyo sababu maana ya maisha ni mojawapo kati ya masuala makuu ya binadamu duniani: hawezi kukwepa maswali ya kutoka moyoni mwake kuhusu thamani, madhumuni na umuhimu wa maisha yake.

Suala hilo linaweza kujitokeza kwake katika maswali mengi tofauti yanayohusiana, kama vile: "mbona tumekuwepo?"; "maisha yanahusu nini?" na "nini maana ya hayo yote? Binadamu anajiuliza maswali kama hayo hasa anapokabiliana na kifo, kwa mfano msiba wa ndugu au rafiki.

Hilo limekuwa suala kuu la udadisi wa sayansi, falsafa na dini tangu zamani. Hivyo kumekuwa na idadi kubwa ya majibu kutoka asili mbalimbali kadiri ya itikadi na utamaduni.

                                     

1. Marejeo

 • Heraclitus, Fragments, James Hilton, forward, Brooks Hexton, translator, Penguin Classics, 2003, ISBN 0-14-243765-4, ISBN 978-0-14-243765-0
 • Terry Eagleton, The Meaning of Life, Oxford University Press, 2007, ISBN 0-19-921070-5 ISBN 978-0-19-921070-1
 • Alvin Thalheimer, The Meaning of the Terms: Existence and Reality. Princeton University Press, 1920
 • Bryan Magee, The Story of Philosophy, Dorling Kindersley Lond. 1998, ISBN 0-7513-0590-1
 • Antoine Arnauld and Pierre Nicole Logic, or the Art of Thinking, known as the Port-Royal Logic, translated J. Buroker, Cambridge 1996
 • John Stuart Mill, A System of Logic, 8th edition 1908* Plato, The Republic, translated by Desmond Lee, Penguin Classics, 2003, ISBN 0-14-044914-0, ISBN 978-0-14-044914-3
 • C. J. F. Williams, What is Existence?, Oxford University Press, 1981
 • Michael J. Loux, Ockhams Theory Of Terms translation of book I of the Summa Logicae c-1327
 • Aristotle, The Metaphysics, translated by Hugh Lawson-Tancred, Penguin Classics, 1999, ISBN 0-14-044619-2, ISBN 978-0-14-044619-7
                                     

2. Viungo vya nje

 • The Concept of Existence: History and Definitions from Leading Philosophers
 • Kigezo:Cite SEP
 • "A Treatise on Book Titles" is a work by Sayf al-Din al-Amidi, in Arabic, about "original" and "mental existence". It dates from 1805.