Back

ⓘ Mwanamke wa Kwanza
Mwanamke wa Kwanza
                                     

ⓘ Mwanamke wa Kwanza

Mwanamke wa Kwanza ni cheo kisicho rasmi ambacho hupewa mke wa rais au mkuu wa nchi asiye mfalme au Kaisari. Nchini Marekani, mke wa gavana wa jimbo pia huitwa "Mwanamke wa Kwanza".

                                     

1. Asili

Cheo hicho kilitumiwa mara ya kwanza kama "First Lady" nchini Marekani karne ya 19. Ndivyo Rais Zachary Taylor alivyomwita Dolley Madison mwaka wa 1849 wakati wa mazishi yake.