Back

ⓘ Leopold Sedar Senghor
Leopold Sedar Senghor
                                     

ⓘ Leopold Sedar Senghor

Léopold Sédar Senghor alikuwa mshairi, mwanasiasa na hatimaye rais wa kwanza wa Senegal kati ya miaka 1960 na 1980.

Senghor alikuwa Mwafrika wa kwanza aliyechaguliwa kuwa mwanachama wa Académie française. Kabla ya uhuru wa nchi yake aliunda chama cha Umoja wa Kidemokrasia wa Senegal kwa Kifaransa: Bloc démocratique sénégalais; kwa Kiingereza: Senegalese Democratic Bloc. Wengi wanamhesabu kati ya wataalamu Waafrika muhimu zaidi katika karne ya 20.

                                     

1. Maisha

Senghor alizaliwa katika kijiji cha Joal kilichowahi kuwa kati ya vituo vya kwanza vya wafanyabiashara kutoka Ulaya na pia kitovu cha misheni Za Kanisa Katoliki kwenye pwani ya Senegal. Baba yake alikuwa mfanyabiashara mzalendo, mama yake mke wa tatu wa baba na Muislamu.

Alipokuwa na umri wa miaka 8 alianza kusoma shule ya mapadre akaendelea kwenye seminari ya mapadri wa Roho Mtakatifu na baada ya kushauriwa asiendelee na masomo ya upadre alisoma shule ya kawaida.

Alimaliza vema hasa kwa masomo ya Kifaransa na Kilatini akapewa nafasi ya kusoma chuo Ufaransa.

Mwaka 1928 Senghor alikwenda Ufaransa aliposoma lugha na baadaye sarufi ya Kifaransa kwenye Chuo Kikuu cha Paris. Baada ya masomo alipewa nafasi ya kufundisha kwenye vyuo vya Tours na Paris. Mwaka 1932 alipata uraia wa Ufaransa.

Tangu siku zake masomoni alikuwa na urafiki na Aime Cesaire na pamoja naye alibuni hoja ya "negritude" walipotetea kuwepo kwa utamaduni wa "Watu Weusi" kama utamaduni wa pekee na muhimu, tofauti na utamaduni wa Kizungu.

Mwaka 1945, baada ya vita vikuu vya pili na ushindi wa Ufaransa, alijiunga na chama cha kisoshalisti akachaguliwa kuwa mbunge.

Mwaka 1960 alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Senegal akaendela kushika nafasi hiyo hadi mwaka 1980 alipongatuka kwa hiari.

                                     
  • Senegal, 26 Machi 1951 ni mmoja wa washairi wakuu wa Kiafrika. Leopold Sedar Senghor alisema juu yake ndiye mshairi mwenye ujuzi zaidi wa kizazi chake