Back

ⓘ Makari Mkuu
Makari Mkuu
                                     

ⓘ Makari Mkuu

Makari Mkuu alikuwa mkaapweke na padri wa Misri.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Januari, 19 Januari na 4 Aprili kadiri ya madhehebu.

                                     

1. Maisha

Mzaliwa wa Misri Kusini, aliwahi kufanya biashara ya chumvi, akaoa, lakini mke wake akafa mapema.

Mwaka 330 hivi akawa mfuasi wa Antoni Mkuu jangwani.

Huko alikataa upadrisho akahamia pengine aliposingiziwa vibaya.

Hapo alihamia kwenye jumuia ya bonde la Sketes leo Wadi El Natrun alipokubali kupewa upadri na kuwa kiongozi wa kiroho wa wamonaki. Kati ya wanafunzi wake wa miaka 356-384 kuna Sisoe, Isaya, Aio, Mose Mwethiopia, Pafnusi, Zakaria, Teodoro wa Ferme.

Hivyo monasteri yake ilichangia sana ustawi wa umonaki ikadumu hai hadi leo.

Miaka 373-375 askofu Mwario Lusio wa Aleksandria alimpeleka uhamishoni kwa imani yake.

Kama alivyowafundisha wengine, aliishi kwa Mungu tu katika sala, akajulikana kwa hekima yake.

                                     

2. Marejeo mengine

 • Plested, Marcus, 2004. The Macarian Legacy: The Place of Macarius-Symeon in the Eastern Christian Tradition. Oxford: OUP
 • Mason, AJ trans., 1921, Fifty Spiritual Homilies of St Macarius the Egyptian, London: SPCK
 • Maloney, GA, SJ trans., 1992, Pseudo-Macarius. The Fifty Spiritual Homilies and the Great Letter, CWS, New York: Paulist Press
                                     

3. Viungo vya nje

 • Schaff-Herzog Encyclopedia of Religious Knowledge, 1914: "Macarius the Egyptian"
 • Macarius the Great Select Resources, Bilingual Anthology
 • Greek Opera Omnia by Migne Patrologia Graeca with Analytical Indexes
 • Great Macarius work in Greek and English
 • Spiritual Homilies 1-5, 6-11, 12-22
 • Wesley Center Online Archived Februari 29, 2008 at the Wayback Machine.
                                     
 • Makari wa Aleksandria 300 hivi - 395 alikuwa mmonaki maarufu katika jangwa la Nitria. Alikuwa kijana zaidi kidogo kuliko Makari Mkuu ndiyo sababu anaitwa
 • Filadelfia, Ponsyano wa Spoleto, Mario, Martha, Audifas na Abako, Makari mkuu Makari wa Aleksandria, Basiano wa Lodi, Liberata na Faustina, Yohane wa
 • wamonaki na hatimaye jangwani Misri karibu na Makari Mkuu Walikuwa wa kwanza kufariki huko Skete na Makari alijenga kanisa la kwanza huko jangwani pale
 • Pafnusi wa Tebe alikuwa mmonaki mfuasi wa Antoni Mkuu na wa Makari Mkuu halafu askofu wa mji fulani wa Thebaid kaskazini Misri mwanzoni mwa karne ya
 • Pafnusi Mkaapweke alikuwa padri mmonaki wa Misri, mwanafunzi wa Makari Mkuu katika karne ya 4. Alikuwa hatoki chumbani, isipokuwa kwa kushiriki Liturujia
 • Makari wa Yerusalemu alifariki 335 hivi alikuwa askofu wa Yerusalemu kuanzia mwaka 312 hadi kifo chake. Alishiriki Mtaguso wa kwanza wa Nisea 325 na
 • Bikira Maria Kukingiwa dhambi ya asili, lakini pia kumbukumbu za watakatifu Makari wa Aleksandria, Papa Eutikiani, Eukari wa Trier, Patapi wa Thebe, Romariki
 • huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Kayo na Aleksanda, Vikta wa Afrika, Makari wa Yerusalemu, Papa Simplicio, Droktovei, Atala wa Bobbio, John Ogilvie