Back

ⓘ Maendeleo
                                               

Maendeleo Vijijini

Angalia: Makala inatoa ufafanuzi wa Vijijini maendeleo. Tazama USDA Maendeleo Vijijini kwa Shirika la Maendeleo Vijijini la Idara ya Kilimo Marekani USDA RD. Vijijini maendeleo kwa jumla hutumika kuashiria matendo na juhudi zilizochukuliwa ili kuboresha hali ya maisha katika vitongoji zisizo Mjini, vijijini, na vijiji vilivyo mbali Jumuiya hizo zinaweza kuelezewa kwa uwiano wa wenyeji kwa nafasi iliyowazi. Shughuli za kilimo zinaweza kuwa maarufu katika kesi hii ambapo shughuli za kiuchumi zinahusiana na sekta ya uzalishaji wa vyakula na malighafi.

                                               

Bongiwe Dhlomo-Mautloa

Bongiwe au Bongi Dhlomo-Mautloa ni raia wa Afrika ya Kusini mwenye asili ya Kizulu na hujishughulisha katika uchapishaji na usimamizi wa kazi za sanaa. Pia ni mwanaharakati. Amesoma shule ya mtakatifu Chad iliyopo Ladysmith, KwaZulu-Natal, na shule ya seminari ya Inanda. Alijifunza uchapishaji akiwa "Rorkes Drift Art and Craft Centre" ambapo alipata stashahada ya sanaa. Alifanya kazi katika kituo cha Sanaa cha African Art Centre huko Durban mwaka 1980- 1983 kisha kufanya kazi katika jumba la maonyesho ya Sanaa la Grassroots katika mji huo wa Durban. Kabla ya kuhamia jiji la Johannesburg, a ...

                                               

ARPANET

Advanced Research Projects Agency Network ulikuwa ndio mfumo wa kwanza wa intaneti kutumika, na mfumo wa kwanza kutumia TCP/IP protokali za kimuunganiko baina ya vifaa viwili vya kielektroniki. Misemo yote hii ndiyo inayotumika kiufundi katika kuielezea intaneti. ARPANET ilianzishwa na Advanced Research Projects Agency ARPA ya Marekani inayojihusisha na mambo ya kiusalama ya nchi hiyo. Katika harakati za kuendeleza mawazo ya J. C. R. Licklider, Bob Taylor ndiyo yaliyopelekea kuzinduliwa kwa mradi huu wa ARPANET mnamo mwaka 1966 na kuwezesha kompyuta mbalimbali kuwasiliana. Taylor alimteuwa ...

Maendeleo
                                     

ⓘ Maendeleo

Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia hapa Maendeleo

Maendeleo ni mabadiliko yanayoonekana kuboresha hali ya binadamu.

Hali hiyo inajitokeza katika nyanja mbalimbali za maisha na kulisha mawazo mengi.

Upande wa sayansi yanahusika na ongezeko la ujuzi kutokana na utafiti na mabadilishano ya matokeo yake.

Upande wa historia yanahusishwa na utambuzi wa kwamba ulimwengu unaweza kuboreshwa zaidi na zaidi kutokana na mchango wa sayansi, teknolojia, uhuru n.k.

Upande wa jamii yanahusishwa na tarajio la kwamba binadamu anaweza kupata hali bora zaidi na zaidi katika mafungamano, siasa, uchumi n.k.

Upande wa falsafa yanahusishwa na tumaini au hakika ya kuwa hali ya binadamu itazidi kuwa bora. Kinyume chake, wengine wanaonyesha kwamba vipindi vya ustawi vinafuatwa na vingine ambapo maendeleo hayatokei, sanasana ni kurudi nyuma.

Kwa jumla, ni muhimu kutambua kwamba si kila badiliko linaleta maendeleo, au walau maendeleo ya upande mmoja yanaweza yakaendana na hali yu kurudi nyuma upande mwingine.

Mara nyingi inatajwa teknolojia ambayo ikitumika vibaya inaweza kuharibu maadili, uchumi n.k. hata kuangamiza kabisa uhai k.mf. mabomu ya nyuklia.

Itafaa daima kukumbuka kaulimbiu ya Julius K. Nyerere: "Maendeleo ni watu, si vitu". Wengine wanauliza, "Maendeleo ya watu ni yapi? Na maendeleo ya vitu ni yapi?"