Back

ⓘ Sultani
                                               

Osmani I

Osmani I alikuwa mwanzilishaji wa Waosmani aliyeweka msingi kwa Milki ya Osmani iliyoendelea kwa karne sita hadi 1922 katika eneo la Uturuki, Balkani, Shamu na Misri. Chanzo chake ilikuwa kama chifu au mtemi wa kabila la Kiturki mpakani wa Ufalme wa Bizanti katika Anatolia. Awali utemi wake ilikuwa chini ya Waturki Waselchuki lakini baada ya uvamizi wa Wamongolia mnamo 1258 uwezo wa Waselchuki ulipungua na Osman alijitangaza kuwa Sultani wa dola huru mwaka 1299. Aliendelea kuwashambulia hasa Wabizanti kwa msaada wa maghazi wengi waliojiunga naye kutoka nchi mbalimbali za Waislamu kwa kusud ...

                                               

Hamad bin Thuwain wa Zanzibar

Sayyid Hamad bin Thuwaini Al-Buwsaid alikuwa Sultani wa tano wa Zanzibar. Aliongoza Zanzibar kuanzia tarehe 5 Machi 1893 hadi 25 Agosti 1896.

Sultani
                                     

ⓘ Sultani

Neno lenyewe lamaanisha "nguvu", "mamlaka" au "utawala" likawa baadaye kama cheo cha mtawala wa kiislamu mwenye kujitegemea bila kuwa na mwingine juu yake.

                                     

1. Masultani katika historia

Kiasili cheo cha Sultan ilikuwa ngazi moja chini ya Khalifa. Lakini watawala wa Milki ya Osmani waliendelea kujiita "sultani" hata baada ya kupokea cheo cha khalifa pia.

Baadaye cheo cha sultani kilitumiwa katika nch mbalimbali na watawala wa ngazi mbalimbali.

Katika historia ya Uswahilini "sultani" ilikuwa mara nyingi neno lingine kwa chifu mkubwa kama yeye alikuwa Mwislamu.

Katika historia sehemu ya watawala wa Kiislamu walipendelea cheo cha mfalme kar.: malik au Emir / Amir mwenye amri.

                                     

2. Masultani leo

Leo hii kuna nchi mbili zinazotawaliwa na mfalme mwenye cheo cha Sultani ni Omani na Brunei.

Masultani wengine wenye madaraka ni watawala wa majimbo tisa ya shirikisho la Malaysia.

Kuna watawala wa jadi katika nchi mbalimbali wanaoendelea kutumia cheo lakini hawana madaraka tena.

Watawala wa nchi Moroko tangu 1956, Uarabuni wa Saudia, Yordani tangu 1946 wanatumia cheo cha mfalme malik. Nchi za Libya, Misri, Irak na Yemeni zilikuwa na wafalme.

Nchi kama Kuwait na falme za Kiarabu hutawaliwa na watawala wanaorithi cheo lakini wanatumia cheo cha "amiri".

Ali bin Hamud of Zanzibar
                                               

Ali bin Hamud of Zanzibar

Ali bin Hamud alikuwa sultani wa Zanzibar kwa miaka tisa Alitangazwa rasmi kuwa Sultani wa Zanzibar tarehe 20 Julai 1902, siku mbili kabla ya kifo cha baba yake aliyekuwa Sultani wa saba. Kulikuwa na utawala wa muda mfupi mpaka pale alipopata ridhaa ya wengi kuanza uongozi. Alitumikia kiti hicho cha usultani kwa muda mfupi kutokana na maradhi. Tarehe 9 Desemba 1911 Ali alijiuzulu na kuacha kiti hicho kwa shemeji yake Khalifa bin Harub Al-Busaid.

Makaburi ya Masultani, Zanzibar
                                               

Makaburi ya Masultani, Zanzibar

Makaburi ya Masultani yapo kadhaa katika kitongoji cha Forodhani, Zanzibar. Kutokana na mila za nyakati za zamani maeneo ya maziko yalitakiwa kuwa karibu na nyumba. Familia ya sultani ilizikwa haswa karibu na ikulu.

                                               

Bafu za Kisultani, Zanzibar

Bafu za Kisultani, Zanzibar ni bafu ndogo zenye muundo wa bafu za Uajemi zilizojengwa maalumu kwa ajili ya familia ya Sultani wa Zanzibar, Tanzania. Zilijengwa ndani ya moja ya Majumba ya Beit al-Tahin - leo Shule ya Forodhani.

Soko la Darajani, Zanzibar
                                               

Soko la Darajani, Zanzibar

Soko la Darajani ni soko kuu katika Mji Mkongwe, Zanzibar. Pia linajulikana kama Soko la Estella na kwa jina lisilo rasmi Marikiti Kuu. Soko liko katika barabara ya Darajani, katika mazingira ya Kanisa kuu la Kristo la Anglikana. Muundo mkuu wa soko ulijengwa mnamo 1904 na Bomanjee Maneckjee, kwa Sultani Ali bin Hamud. Baadaye ulipanuliwa na kurejeshwa. Soko la Darajani haswa ni soko la chakula, lakini pia kuna maduka yanayouza bidhaa anuwai, kutoka vifaa vya umeme mpaka mavazi.