Back

ⓘ Kazi
                                               

Symphony No. 5 (Beethoven)

Symphony No. 5 in C minor, Op. 67 ni jina la kutaja simfoni iliyotungwa na mtunzi wa Opera kutoka nchini Ujerumani, Ludwig van Beethoven. Hii ni simfoni ya 5 katika simfoni zake tisa. Ilitungwa kati ya 1804 na 1808. Hii ni moja kati ya Simfoni maarufu zaidi katika kazi za muziki wa classical. Simfoni ina miendo au mitindo minne: ya kufungulia sonata allegro, ya polepole andante, ya haraka scherzo ambayo hii inaongoza hadi mwisho wa simfoni. Kwa mara ya kwanza simfoni hii ilitumbuizwa mjini Vienna katika tamasha lililofanyika katika ukumbi wa Theater an der Wien mnamo 1808. Simfoni yake Nam ...

                                               

Aya Tarek

Aya Tarek ni msanii kutoka jiji la Alexandria nchini Misri. Sanaa zake zimehusiana na sanaa za mitaani au graffiti na upakaji rangi. Japokuwa sanaa za mitaani nchini Misri zilipata umaarufu mkubwa wa kimataifa baada ya mapinduzi ya Misri ya mwaka 2011, Tarek alianza kuchangia sanaa za mitaani kwenye kuta za jiji la Alexandria mnamo mwaka 2008, alipokuwa na miaka 18. Tarek pia alianza kutoa michoro ya ndani ambayo ilimfanya ajihisi amechukuliwa kama msanii mwenye uwezo mkubwa sana. Japokuwa alikuwa mara kwa mara akiongelea kuhusu umuhimu wa sanaa za mitaani kwamba ilimfikia yeyote aliyetaka ...

                                               

Lisa Castel

Lisa Castel alizaliwa Decemba 22 1955 huko Quela, Malanje Province,ni Mwanahabri na Mwandishi wa nchini Angola. Kulingana na Luís Kandjimbo, Castel ni mwana kikundi wa waandishi wa kike wa kisasa huko Angola kama vile Ana Paula Tavares, Amélia da Lomba Ana de Santana, ambaye anamtaja kama "Kizazi cha kutokuwa na uhakika" "Geração das Incertezas", waandishi ambao kwa kawaida huonyesha uchungu katika kazi zao, wakionyesha kukatishwa tamaa na hali ya kisiasa na kijamii nchini humo. Castel amefanya kazi kwa "Jornal de Angola" na jarida "Archote. Yeye ndiye mwandishi wa mkusanyiko wa mashairi " ...

                                               

Dutu sanisi

Dutu sanisi au dutu sintetiki ni dutu zinazoundwa na binadamu kwa mbinu za kikemia kwenye maabara au viwanda, tofauti na dutu asilia kama ubao au mwamba. Dutu sanisi hupatikana ama kwa kuiga kazi inayotekelezwa kiasili, mfano kukuza fuwele katika maabara na kuzigandaniza ili kuzalisha almasi sintetiki, ama kwa kuunganisha molekuli na kujenga polima kama aina mbalimbali za plastiki. Malighafi katika uzalishaji wa dutu sanisi mara nyingi hupatikana kiasili kama vile mafuta ya petroli. Elementi sintetiki ni elementi za kikemia zinazoundwa katika maabara kwa njia za kifizikia.

                                               

Nyandu Tozzy

Hamidu Salim Chambuso ni msanii wa muziki wa rap kutoka nchini Tanzania, Nyandu alianza muziki mwishoni mwa miaka ya 1990, amewahi kufanya kazi na wasanii wakubwa wa Tanzania akiwa ni pamoja na Profesa Jay, Soggy Doggy Hunter, Unique Sisters, Taff B., Young Dee mara mbili katika "Nimekasirika 2012 na "Double Double" 2017, Fid Q, Dudu Baya, Chin Bees, Mr. Blue akiwa kama mwanachama mwenza katika kundi la B.O.B Click. Katika kazi yake ya muziki, amewahi kuwa sehemu ya kundi la muziki la "New Jack Family" kabla ya hapo alikuwa na akina Slim ambaye alikuwa kiongozi wa kundi la CBM Crew. Baaday ...

                                               

Virginia Raffaele

Virginia Raffaele ni binti wa wasanii wawili wa sarakasi, Raffaele alisomea ngoma ya kitambo na kisasa kwenye Chuo cha kitaifa cha Densi cha Roma na mnamo 1999 alihitimu katika Accademia Teatro Integrato iliyoongozwa na Pino Ferrara. Alianza kazi yake kwenye jukwaa, mara nyingi akifanya kazi kama naibu ya wachekeshaji wawili Lillo & Greg kundi ya wawili ya vichekesho baada ya kuanza kama mwandishii kwenye programu ya Rai 2 Quelli che. il Calcio, Alijulikana kwa uigaji wake na ubishi katika Italia 1 show Mai dire Grande Fratello Show. Kisha alionekana kwenye maonyesho mengine kadhaa, pamoja ...

                                               

Washeli

Washeli ni kisahani chembamba chenye tundu katikati. Hutumiwa pamoja na bolti na nati. Kazi yake ni hasa kutandaza mkazo kwenye uso mkubwa zaidi wa kitu kinachoshikiliwa. Washeli hutumiwa pia kuongeza umbali wakati wa kuunganisha vitu viwili. Ni muhimu pia kwa kutenganisha dutu tofauti kama alumini na feleji ya bolti / nati inayoweza kusababisha ulikaji. Washeli kwa kawaida hutengenezwa kwa metali au plastiki. Zile za mpira au plastiki hupunguza mitikisiko. Washeli zenye uso wa meno huongeza mshiko baina ya nati na bolti na kuzuia kufunkuka kwa mshiko.

Kazi
                                     

ⓘ Kazi

Kazi ni sehemu muhimu ya maisha ya binadamu, hivyo ina nafasi kubwa katika anthropolojia, falsafa, teolojia,fizikia na sosholojia.

Inafafanuliwa kama utendaji unatumia nguvu ya akili au ya mwili ili kufikia lengo fulani, ambalo mara nyingi ni faida ya kiuchumi ili kuweza na kuwezesha kuendelea kuishi.

Lakini thamani yake halisi haiishii katika uzalishaji wa vitu, bali inategemea hasa ustawishaji wa utu katika vipawa vyake vyote kulingana na maadili na maisha ya kiroho.

Kwa msingi huo, ni wajibu wa kila mtu aliyefikia ukomavu fulani.

Ni pia mchango muhimu katika jamii na inayostahili kuheshimiwa na kutunzwa na wote kuanzia serikali hadi watu binafsi.

Kwa kuwa ni wajibu, kazi ni vilevile haki ya msingi ya binadamu. Bila kuwa nayo, mtu anaelekea kunyongonyea na kujiona hama maana, hasa kama utovu wa kazi unadumu muda mrefu na kumzuia asiweze kupanga maisha yake, kwa mfano upande wa ndoa na familia, kwa sababu ya kutojitegemea.

Sheria mbalimbali zinaratibu mahusiano kazini, hasa kama kuna mwajiri na mwajiriwa.

                                     

1. Kazi katika Biblia

Biblia inazungumzia maisha halisi ya watu, hivyo haikuweza kuisahau kazi. Toka kitabu cha Mwanzo 1:1-2:4a inaonyesha heshima ya kufanya kazi kwa kumchora Mungu akitenda kazi kama binadamu kwa siku sita, akipumzika ile ya saba.

Ndiye aliyewaagiza Adamu na Eva wafanye kazi katika dunia ili kuistawisha Mwa 2:15.

Baada ya dhambi ya asili waliyoifanya wajibu huo umebaki, ila kama adhabu sasa unachosha Mwa 3:17-19.

Pamoja na hayo, Yesu alikubali kufanya kazi kwa mikono yake kama fundi labda seremala kwa sehemu kubwa kabisa ya maisha yake, alipoishi na familia yake au walau mama yake kijijini Nazareti Mk 6:3.

Mtume Paulo alipinga kwa nguvu uzembe wa waliodai kazi haihitajiki tena kwa sababu eti, ufalme wa Mungu umefika. Aliandika, "Asiyetaka kufanya kazi, asile chakula" 2Thes 3:10. Mwenyewe, pamoja na kuhubiri Injili alikuwa akiendelea na kazi yake ya kushona mahema ili kupata mahitaji yake bila kulemea wengine.

                                               

Tahakiki

Tahakiki ni maelezo yanayoandikwa na mtu yeyote ambayo huchambua na kufafanua kitaaluma kazi fulani ya fasihi ili kuonyesha wazi uzito na udhaifu wa mambo yaliyojadiliwa, pamoja na uhalisia wa mambo na hatimaye namna ya kuboresha kazi hiyo. Mara nyingi tahakiki huwa kitabu kinachochambua kazi mbalimbali za fasihi andishi. Kazi zinazochambuliwa na tahakiki katika kazi ya fasihi ni pamoja na tamthiliya, riwaya au ushairi.