Back

ⓘ Ufahamu
                                     

ⓘ Ufahamu

Ufahamu ni dhana inayorejelea kujua na kuielewa jambo kwa usahihi na kuweza kulielezea upya kwa usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi.

Ufahamu wa mtu waweza kupimwa katika kusikiliza jambo au katika kusoma.

                                     

1. Kusikiliza

Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe.

                                     

1.1. Kusikiliza Mambo ya kuzingatia katika ufahamu wa kusikiliza

Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:

 • Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa
 • Kuelewa sintaksia muundo wa maneno ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa.
 • Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza

Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafutayo:

 • Kuwa makini na kuelekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia kila anachokisema.
 • Msomaji anatakiwa kuandika baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya muhimu ili kumasidia kukumbuka hapo baadae.
 • Kuwa makini na ishara mbambali za mwili kama vile kurusha mikono, kutingisha kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho. Ishara hizi huwa zinachangia kwa kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.
 • Kutilia maanani vidokezo vya maana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza jambo jipya, anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.
                                     

2.1. Kusoma Kusoma kimyakimya

Katika usomaji huu, msomaji hufumba kinywa na kupitisha macho katika kila mstari harakaharaka. Macho hayo huunganisha neno lililotangulia na lile linalofuata. Ubongo wake huchambua mambo muimu yanayojitokeza, huku akiyahifadhi kichwani.

Mtu akijizoeza kusoma kimya, ananufaika ifuatavyo:

 • Hukwepa kuzingatia kanuni za matamshi
 • Hupata nafasi ya kupima mwendo wake na kiasi cha welewa
 • Hujiepusha na lawama ya kusumbua wengine
 • Huweza kusoma maandishi mengi kuliko ambavyo angesoma kwa sauti
                                     

2.2. Kusoma Kusoma kwa sauti

Kusoma kwa sauti ni namna ya kuyaangalia maandishi na kuyatamka kwa sauti inayosikika.

Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa Kusoma. Kuna vipengele viwili vinavyounda mchakato wa ufahamu wa kusoma:

Uelewa wa msamiati na Uelewa wa matini

Ili kuilelewa habari/matini ni lazima msomaji awe na uwezo wa kuelewa msamiati uliotumika katika matini hiyo. Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka vilevile matini yote haitaeleweka.

Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:

 • Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa zina maneno ya kisanaa hivyo ni muhimu msomaji kubaini maana ya maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, hii itamsaidia kuelewa vyema maana ya mwandishi.
 • Vilevile msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele anachokisoma inampasa akielewe vizuri.
 • Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za uakifishi, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo hatazingatia alama za uakifishaji anaweza kupotosha maana ya mwandishi.
 • Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu inatakiwa ajiulize, Je, kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini mwake basi itakuwa rahisi kwake kuielewa habari hiyo.

Kwa kuzingatia haya yote msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari aliyoisoma na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma.                                     

2.3. Kusoma kusoma kwa burudani

Huu ni usomaji ambao lengo lake kuu huwa ni kujiburudisha tu. Katika usomaji wa aina hii, msomaji hujisomea zaidi magazeti, majarida na vitabu tofauti na vile vinavyotumika darasani.

Mambo ya Kuzingatiwa katika Ufahamu wa Kusoma kwa Burudani

Wakati mwingine si lazima msomaji awe na vitabu vyote ambavyo anahitaji kuvisoma au magazeti na majarida. Inapotokea hivyo, msomaji anaweza kwenda maktaba kuazima kitabu nachokihitaji.

Ingawa lengo la msomaji huwa ni kujiburudisha tu, lakini pia hujiongezea maarifa. Hii ni kwa sababu, magazeti, majarida na vitabu sambamba na kutuamia lugha sanifu huelezea mambo mabalimbali yanayoihusu jamii.

Hivyo msomaji kutokana na kusoma vitabu na majarida mbalimbali hujiongezea kiwango cha welewa wa lugha na mambo mengine ya kijamii yanayojadiliwa humo.

Ni jambo zuri kwa msomaji kujijengea tabia ya kujipima ili aweze kuelewa kiwango cha maarifa aliyopata katika kujisomea. Kujipima huku kunaweza kufanywa kwa kujiundia utaratibu wa kuweka kumbukumbu ya vitu au makala zilizosomwa na kufanya ufupisho wa kila makala.

                                     
 • Aina za ufahamu zilizo kuu ni tatu: ufahamu wa kusoma, ufahamu wa kusikiliza na ufahamu wa kuona. Ufahamu wa kusoma: hapa mtu hupata ufahamu wa jambo fulani
 • Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba kwa Kiingereza Fertility Awareness kifupi FA unahusu mbinu zinazotumika kutambua wakati mwanamke anapoweza kushika
 • mang amuzi ya maisha yakiwa pamoja na kusoma, kusikia au kutenda. Pia huhusisha ufahamu na uelewa, hususani wa ukweli, kama ulivyofundishwa au kuthibitishwa na
 • kufikiri, kuelewa, kuwasiliana, kujifunza, kupanga na kutatua matatizo. Ni ufahamu uliomo katika ubongo wa binadamu, unaoweza hata kutofautisha jambo kwa
 • Msamiati ni maneno magumu yanayotumika katika ufahamu au kifungu cha habari fulani. Kwa kawaida msamiati huwa unafafanuliwa kwa kusoma kifungu cha habari
 • na nguvu kuwa na mali kuwa na nguvu ya kufanya jambo darasani kuwa na ufahamu wa kuelewa masomo ni kipawa binafsi anaweza akawa nayo mwingine, na mwingine
 • daktari kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza misingi ya kisaikolojia ya ufahamu Mwaka wa 2000, pamoja na Paul Greengard na Arvid Carlsson, alikuwa mshindi
 • au hata hapo watakapoamua kuachia madaraka. i. Awe na ufahamu Kiongozi ni lazima awe na ufahamu mkubwa juu ya taasisi anayoiongoza, malengo yake, mazingira
 • na kuchanganyikiwa akilini, kujisikia kama karibu na kupotea, ufahamu au kupotea ufahamu kweli, au kiuu kikali. Kama anemia imeendelea watu weupeweupe
 • kuelewa vizuri kinachotokea wakati viungo havifanyi kazi kawaida. Kwa mfano, ufahamu wa jinsi kazi ya tezi ya thairoidi imesaidia katika kutibu rovu. Uchunguzi
 • kuratibu silika yake kuhusu uzazi ili uendane na uwajibikaji. Ubalehe Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba Uzazi wa mpango Uzazi wa mpango kwa njia asilia