Back

ⓘ Kirgizia
Kirgizia
                                     

ⓘ Kirgizia

Kirgizia pia Kirgizstan, Kirigizistani au Kigistani ; kwa Kikirgizi: Кыргызстан Kyrghyzstan ; kwa Kirusi: Киргизия Kirgizia) ni nchi ya Asia ya Kati.

Imepakana na Kazakhstan, Uzbekistan, Tajikistan na China.

                                     

1. Historia

Hadi mwaka 1991 Kirgizia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyet, ikijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kikirgizi".

Ilipata uhuru wake katika mwendo wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti.

Kabla ya uhuru yalitokea mabadiliko katika uongozi wa chama cha kikomunisti. Viongozi wapya waliotafuta njia bila udikteta mkali walishika uongozi na rais Askar Akayev alirudishwa madarakani katika uchaguzi wa kwanza na wa pili.

Lakini uchaguzi wa mwaka 2005 ulionekana haukuwa huru, hivyo hasira ya wananchi ikalipuka katika mapinduzi. Uchaguzi mpya ukamteua mpinzani wa awali Kurmanbek Bakiyev.

                                     

2. Mgawanyo kiutawala

Hii ni orodha ya mikoa ya Kirgizia pamoja na makao makuu yake:

 • Mkoa wa Naryn
 • Bishkek mji
 • Mkoa wa Batken
 • Mkoa wa Chuy Bishkek
 • Mkoa wa Osh Mjini mji
 • Mkoa wa Issyk Kul Karakol
 • Mkoa wa Talas
 • Mkoa wa Jalal-Abad Jalal-Abad
 • Mkoa wa Osh
                                     

3. Wakazi

Idadi ya wakazi ilihesabiwa 2005 kuwa watu 5.264.000. Takriban 72.6 % kati yao ni Wakirgizi wenyewe, ambao ni jamii ya Waturuki halafu kuna Wauzbeki 14.4 % hasa kusini na Warusi 6.4 % hasa kaskazini, mbali na makundi madogo zaidi.

Lugha ya kawaida ni Kikirgizi, ambacho ni lugha rasmi pamoja na Kirusi. Angalia pia orodha ya lugha za Kirgizia.

Takriban 64% ni Waislamu, lakini kuna uhuru wa dini. Wakristo wako hasa katika ya wakazi wenye asili ya Ulaya, wakiwemo kwanza Waorthodoksi, halafu Waprotestanti na Wakatoliki wachache.

                                     

4. Marejeo

 • Kyrgyzstan: The Growth and Influence of Islam in the Nations of Asia and Central Asia by Daniel E. Harmon
 • Kyrgyzstan: Central Asias Island of Democracy? by John Anderson
 • Odyssey Guide: Kyrgyz Republic by Ceri Fairclough, Rowan Stewart and Susie Weldon
 • Politics of Language in the Ex-Soviet Muslim States: Azerbaijan, Uzbekistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Turkmenistan and Tajikistan by Jacob M. Landau and Barbara Kellner-Heinkele. Ann Arbor, University of Michigan Press, 2001. ISBN 978-0-472-11226-5
 • Kyrgyzstan: Traditions of Nomads by V. Kadyrov, Rarity Ltd., Bishkek, 2005. ISBN 9967-424-42-7
 • Lonely Planet Guide: Central Asia by Paul Clammer, Michael Kohn and Bradley Mayhew
 • Historical Dictionary of Kyrgyzstan by Rafis Abazov
                                     

5. Viungo vya nje

Serikali
 • Laws of the Kyrgyz Republic
 • Tovuti rasmi ya serikali
 • President of Kyrgyzstan official site
 • Parliament of Kyrgyzstan official site
General information
 • Kigezo:Wikivoyage-inline
 • Kyrgyzstan entry at The World Factbook
 • Kyrgyz Publishing and Bibliography Archived Aprili 5, 2010 at the Wayback Machine.
 • Kyrgyzstan at UCB Libraries GovPubs
 • Country Profile from BBC News
 • Key Development Forecasts for Kyrgyzstan from International Futures
Ramani Wikimedia Atlas of Kyrgyzstan
                                     
 • Historia ya Kirgizia inahusu eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya Kirgizia Hadi mwaka 1991 Kirgizia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyet, ikijulikana kwa
 • Kirgiz Sovyettik Sotsialistik Respublikasi Leo hii imekuwa nchi huru ya Kirgizia Ilikuwa jamhuri kubwa ya saba yenye eneo la 198, 500 km² ndani ya Umoja
 • nchini Kirgizia Uchina, Afghanistan, Urusi, Uturuki na Uzbekistan inayozungumzwa na Wakirgizi. Kikirgizi ni lugha rasmi katika nchi za Kirgizia Mwaka
 • Bishkek Bichkiek ni mji mkuu wa Kirgizia Ina wakazi 900, 000 2005 Mji ulianzishwa kama kituo cha misafara kwenye barabara ya hariri kati ya China
 • yake kipo katika Milima ya Tian Shan huko Kirgizia na mashariki mwa Uzbekistan. Mto wenyewe unaanza Kirgizia katika bonde la Ferghana ambako matawimto
 • Jengish Chokusu ni mlima wenye kimo cha m 7, 439 juu ya usawa wa bahari. Uko kati ya China na Kirgizia Orodha ya milima
 • Uhuru Peak Pamir ni mlima wenye kimo cha m 7, 134 juu ya usawa wa bahari. Uko kati ya Tajikistan na Kirgizia kwenye milima ya Pamir. Orodha ya milima
 • rasmi katika Urusi na pia katika nchi jirani za Belarus, Kazakhstan na Kirgizia Wasemaji wa Kirusi wako katika nchi zote zilizokuwa sehemu ya Umoja wa
 • MV au mv ni kifupi cha: Kodi ya IATA ya Manas Air, Kirgizia Kodi ya ISO 3166 - 1 ya nchi ya Maldivi
 • Шарипович Шарип уулу Жээнбеков alizaliwa 16 Novemba 1958 ni mwanasiasa wa Kirgizia kwa sasa Rais wa nchi. Alianza kazi rasmi tarehe 24 Novemba 2017. Awali
 • GI au gi ni kifupi cha: Kodi ya IATA ya Itek Air, Kirgizia Kodi ya ISO 3166 - 1 ya nchi ya Gibraltar