Back

ⓘ Uraibu
Uraibu
                                     

ⓘ Uraibu

Uraibu ni hali inayopatikana wakati roho au mwili unataka mno kuwa na hisia fulani kiasi cha kuwa na matatizo kutekeleza shughuli hadi kufikia tena hisia inayolengwa.

Hisia za aina hii zinaweza kupatikana kutokana

  • au matendo mengine ya kurudiarudia ambayo yanaweza kuwa tofauti sana, kama vile kununua vitu au kuiba
  • kusikia matokeo ya kuingiza pombe au dawa fulani kwenye mwili
  • kujishughulisha mno na michezo ya kompyuta, michezo ya fedha, simu ya mkononi, kutazama televisheni n.k.
  • kusikia matokeo ya kuvuta sigara, bangi au madawa mengine

Uraibu hutazamwa kama ugonjwa au utumwa wa ndani. Katika jamii inaeleweka kwa kawaida kama uraibu wa dawa yaani dutu zinazomfanya mtu kurudia matumizi hata kama inaharibu afya, hali yake katika jamii na hata kuvunja sheria. Hapo ni hasa dawa za kulevya zinazojulikana kuwa zinaunda uraibu.

Lakini matumizi ya kiraibu ya dawa inakuja pamoja na hali ya kiroho inayofanana kabisa na hali ya uraibu wa vitu au matendo mengine.