Back

ⓘ Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes
Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes
                                     

ⓘ Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes

Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes ni jina la kitabu kinachoelezea maisha na harakati zilizokuwa zinafanywa na hayati Abdulwahid Sykes katika kupigania uhuru wa Tanganyika kutoka mikononi mwa wakoloni katika miaka ya 1950. Harakati ambazo katika historia ya Tanzania leo hii haijawekwa wala kugusiwa. Kitabu kinaelezea historia iliyofichwa kuhusu Waislamu dhidi ya ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika.

                                     

1. Muhtasari wa kitabu

Wakati wa utawala wa Julius Nyerere kama rais wa Tanzania mambo matatu yalikuwa mwiko kuelezea: kuwa historia ya kudai uhuru wa Tanganyika ilianza kabla yake; kuwa Waislamu ndio waliokuwa katika mstari wa mbele katika harakati za kupambana na wakoloni; kuwa kutokana na historia ya kudai uhuru Waislamu walikuwa na kinyongo na serikali kwa kutothamini mchango wao na kutotekeleza ahadi iliyowekwa wakati wa kudai uhuru.

Mwandishi ameelezea na kufanya utafiti wa kina katika masuala hayo yote. Kupitia maisha ya marehemu Abdulwahid Sykes na kumbukumbu za baba yake Kleist Sykes, mwandishi anamfunulia msomaji majina na juhudi za wazalendo wa mwanzo waliopambana na wakoloni na kumkutanisha na waasisi na viongozi wa kisiasa katika African Association mnamo miaka ya 1920.

Hali kadhalika kitabu kinaelezea michango chanya na adimu kuhusu wazalendo na viongozi vijana walioanzisha TANU mwaka 1954 kudai uhuru wa Tanganyika chini ya uongozi wa Julius Nyerere. Katika kufanya hivi, kitabu kimewatoa hofu wale waliokuwa wakidhani ya kwamba kuandika historia inayopingana na "historia rasmi" ni kukosa uzalendo na mapenzi kwa nchi yao.

                                     

2. Tazama pia

 • John Rupia
 • Dossa Aziz
 • Titi Mohamed
 • Sheikh Amir Bin Juma
 • Zubeir Mtemvu
 • Ali Mshamu
 • TANU
 • Sheikh Suleiman Takadir
 • Ally Sykes
 • Abdulwahid Sykes
 • Tewa Said Tewa
                                     

3. Viungo vya nje

 • Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes katika Google books
 • Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes katika Worldcat
 • Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes katika JamiiForums
 • Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes katika Elibary