Back

ⓘ Jamii:Uyahudi
                                               

Kiyiddish

Kiyiddish ni lugha inayotumiwa na Wayahudi. Ilikuwa lugha kuu ya Wayahudi wengi duniani, hasa katika Ulaya ya Kati na Ulaya ya Mashariki hadi maangamizi makuu dhidi ya Wayahudi wa Ulaya. Tangu maangamizi hayo idadi ya wasemaji imepungua sana, leo kuna takriban wasemaji 600.000 duniani. Ni tofauti na Kiebrania ambayo ni lugha ya kidini ya Wayahudi na lugha rasmi katika nchi ya Israeli, lakini huandikwa kwa herufi za Kiebrania. Asili yake ni Kijerumani cha zamani pamoja na Kiebrania. Ilianzishwa na Wayahudi wa Ujerumani takribani miaka 1.000 iliyopita. Wakati wa mateso dhidi yao katika Vita ...

                                               

Ladino

Ladino ni lugha inayozungumzwa na Wayahudi katika nchi mbalimbali. Ni lugha ya karibu na ikiwa na maneno ya Kiebrania ndani yake. Wasemaji wengi wako Israel, halafu Uturuki, Bulgaria na Marekani. Idadi ya wasemaji inaendelea kupungua; mnamo 1990 walikuwa 150.000 duniani. Asili ya lugha hii ni jumuiya kubwa ya Wayahudi walioishi Hispania hadi karne ya 15. Hadi mwaka 1492 sehemu za Hispania ilitawaliwa na Waarabu. Baada ya kutekwa kwa nchi yote na Wahispania Wakristo walianza kuwa na wasiwasi kuhusu Waarabu Waislamu na pia Wayhudi waliokaa nchini. Matso makali yalifuata na dini zote nje ya U ...

                                               

Mafarisayo

Mafarisayo waliunda madhehebu mojawapo ya Uyahudi ambayo wakati wa Yesu Kristo iliweza kufikia 5% ya Wayahudi wote, lakini ilikuwa na athari kubwa katika jamii yao, kutokana na sifa ya kuwa wanadini hasa. Jina lenyewe lina maana ya waliojitenga ili kushika kiaminifu masharti yote ya Torati ya Musa. Mafarisayo wanajulikana hasa kutokana na Injili ambazo zinawataja kwa kawaida kama wapinzani wa Yesu, ingawa yeye alikuwa anakubaliana nao katika mafundisho mengi ya imani tofauti na yale ya Masadukayo, dhehebu jingine kubwa lililokuwa na wafuasi hasa kati ya makuhani. Mafarisayo walianza mwisho ...

                                               

Masadukayo

Masadukayo waliunda madhehebu muhimu ya dini ya Uyahudi wakati wa Yesu Kristo. Walikuwa na nguvu hasa kati ya makuhani. Ndiyo maana waliishiwa nguvu hekalu la Yerusalemu lilipoangamizwa na Warumi pamoja na mji mzima mwaka 70 B.K. Walikubali Torati ya Musa tu, na kukataa vitabu vingine vyote vya Biblia. Kwa msingi huo, walikataa mafundisho yaliyoletwa na manabii, kama vile juu ya ufufuo wa wafu na uzima wa milele. Katika hilo waligongana na Mafarisayo na Yesu ambaye, kadiri ya Injili, ndio waliohusika zaidi na kifo chake.

                                               

Mitazamo ya Kiyahudi juu ya Yesu

Mitazamo ya Kiyahudi juu ya Yesu ni ya aina mbalimbali, lakini yote haimkubali, la sivyo ingewabidi wahusika wamuamini na kubatizwa badala ya kuendelea na dini yao ambayo viongozi wake walimhukumu ni kafiri anayestahili kuuawa. Kwa kawaida Wayahudi wanamuona Yesu kama mmojawapo kati ya wengi waliojinadi kuwa Masiya katika nyakati mbalimbali za historia ya taifa lao. Yesu anatazamwa kama yule aliyefaulu zaidi kukubalika, na kwa sababu hiyo, kuleta madhara makubwa kuliko wote. Uyahudi haujawahi kumkubali rasmi Masiya yeyote kuwa ametimiza utabiri wa manabii. Zaidi ya hayo, unaona ibada ya Wa ...

                                               

Musa

Musa aliishi miaka 1250 hivi K.K. akawa kiongozi wa Wanaisraeli walipoondoka nchini Misri kukimbilia nchi ya Kanaani. Hasa Torati na vitabu vingine vya Biblia vinasimulia habari zake. Pia Qurani inamtaja katika aya 502. Waisraeli waliishi Misri kama wageni tu zaidi ya miaka mia nne Mdo 7:6-16 wakiongezeka kiasi cha kuwatisha wenyeji wao ambao walianza kuwafanya watumwa mwaka 1300 hivi K.K. Kwa mujibu wa Biblia, katika kuwakomboa utumwani, Mungu alijionyesha mtetezi wa haki za maskini. Pamoja na kushurutishwa kufanya kazi wasizozipenda, ilitolewa amri ya kuua watoto wao wote wa kiume, ingaw ...

Ketubimu
                                               

Ketubimu

Ketubimu ni sehemu ya tatu na ya mwisho ya Biblia ya Kiebrania. Vitabu hivi hugawanywa katika kundi za: vitabu vya hekima kama vile Ayubu, Mhubiri na Mithali. vitabu vya kishairi kama vile Zaburi, Maombolezo na Wimbo Ulio Bora. vitabu vingine kama vile Ruthu, Estha na Danieli. vitabu vya kihistoria kama vile Ezra, Nehemiah na Mambo ya Nyakati.

Wahasidimu
                                               

Wahasidimu

Wahasidimu ni kundi la Wayahudi. Asili yake ni mwamko wa kiroho katika karne ya 18 ambao kutoka Ukraine magharibi ulienea haraka Ulaya Mashariki kote. Israel Ben Eliezer, "Baal Shem Tov", anahesabiwa kuwa mwanzilishi wake. Leo wafuasi wake ni 400.000 hivi, na wengi wao wako Marekani, Israel na Ufalme wa Muungano.

Wazeloti
                                               

Wazeloti

Wazeloti walikuwa Wayahudi wa karne ya 1 BK waliopigania uhuru wa nchi yao kutoka utawala wa Warumi. Walianzishwa na Yuda Mgalilaya na kukoma katika vita vya kwanza vya Kiyahudi. Maarufu kati yao ni Mtume Simoni Lk 6:15; Mdo 1:13.