Back

ⓘ Huruma




Huruma
                                     

ⓘ Huruma

Huruma ina maana ya wema ulio tayari kusaidia na kusamehe.

Sifa hiyo kwanza ni wa "Mungu" kadiri ya dini mbalimbali, zikiwemo Uyahudi, Ukristo na Uislamu.

Katika karne ya 20, iliyojaa ukatili wa vita vingi, sifa hiyo imezingatiwa zaidi katika ibada kwa Huruma ya Mungu.

Kutokana na imani hiyo, binadamu pia anapaswa kuwa na huruma na kutekeleza matendo ya huruma ya kiroho na ya kimwili.

Hata katika jamii, huruma inahitajika katika mahusiano yoyote pamoja na haki.

Yesu alitangaza Math 5:7, "Heri wenye huruma, maana hao watapata huruma" kutoka kwa Mungu.

Mara nyingi Liturujia inamlilia Mungu awe na huruma.