Back

ⓘ Agano
Agano
                                     

ⓘ Agano

Agano ni neno lenye maana nzito katika dini mbalimbali, hasa zile zinazofuata imani ya Abrahamu kwa Mungu mmoja.

Upekee wake ni kwamba agano hilo si kati ya pande mbili zilizo sawa, kama yale kati ya watu, bali ni Mungu anayelianzisha na kupanga masharti, akimhimiza binadamu kukubali na kuwa mwaminifu.

                                     

1. Jina

Agano ni tafsiri ya kawaida ya neno la Kiebrania ברית, bərîṯ au berith.

Katika Biblia ya Kiebrania linatumika mara 264.

Tafsiri ya Kigiriki katika Septuaginta na katika Agano Jipya ni διαθήκη, diatheke, ambalo lina maana ya wasia pia ndiyo sababu katika Kilatini tunakuta Testamentum.

                                     

2. Uyahudi

Wazo la agano ni la msingi kwa Wayahudi, nao wanaona lile alilofanya Mungu na Musa kwenye mlima Sinai linawahusu wao, wakati kwa mataifa mengine lipo lile alilolifanya na Noah.

                                     

3. Ukristo

Ukristo unakiri kwamba Mungu alifanya maagano mengine na binadamu, lakini hatimaye alianzisha "Agano Jipya" na la milele katika damu ya Yesu Kristo iliyomwagwa kwa ondoleo la dhambi za watu wote watakaomuamini.