Back

ⓘ Rais
                                               

Photographic Convention of the United Kingdom

Photographic Convention of the United Kingdom ilianzishwa mwaka 1886 na mkataba wake wa kwanza ulifanyika katika mji wa Derby, England mwezi Agosti mwaka huo. Wajumbe waanzilishi walikuwa mchanganyiko wa wapiga picha hodari na matajiri. Wapiga picha mashuhuri waliokuwepo katika mkutano wa kwanza ni pamoja na William England, principal mpiga picha na London Stereoscopic Company; Richard Keene, ambaye baadaye akawa mwanachama wa The Brotherhood of the Linked Ring na Alfred Seaman ambao alianzisha idadi kubwa ya studio huko Midlands na Kusini mwa Uingereza.Pictorialist aliyeongoza alikuwa Hen ...

Rais
                                     

ⓘ Rais

Rais ni cheo cha mkuu wa nchi katika serikali ya jamhuri, na pengine mkuu wa taasisi fulani.

Rais wa nchi huwa anachaguliwa ama na wananchi wote au na bunge. Katika nchi kadhaa kuna pia mkutano maalumu unaoitishwa kwa uchaguzi wa rais pekee, kama vile Marekani au Ujerumani.

Kuna aina mbili za rais kufuatana na katiba za nchi mbalimbali:

  • rais kama mkuu wa nchi asiyeshughulikia mambo ya serikali, jinsi ilivyo Ujerumani au Uhindi serikali ya kibunge
  • rais kama mkuu wa serikali, jinsi ilivyo Marekani na pia katika nchi nyingi za Afrika serikali ya kiraisi.

Katika muundo wa serikali ya kibunge shughuli za serikali zinasimamiwa na waziri mkuu. Madaraka ya rais katika muundo huo hufanana na madaraka ya mfalme wa kikatiba isipokuwa hayupo kama rais kwa muda wa maisha yake kama mfalme.

Katika nchi chache, yaani Uswisi, San Marino na Uruguay, kazi za rais hazitekelezwi na mtu mmoja bali na kamati ya viongozi kwa ujumla, kama Halmashauri ya Shirikisho ya Uswisi.