Back

ⓘ Mfalme
                                               

Europa (mitholojia)

Europa ni jina la mwanamke katika mitholojia ya Ugiriki. Alikumbukwa kama binti wa mfalme wa Finisia katika Asia ya Magharibi aliyetongozwa na mungu mkuu Zeus na kupelekwa naye hadi kisiwa cha Krete. Jina lake lilikuwa hivyo jina la bara la Europa yaani Ulaya. Katika masimulizi ya Europa Zeus ni mungu mkuu anayezunguka muda wote duniani akitafuta mapenzi na mabinti mazuri wa kibinadamu lakini anahitaji kujificha kwa sababu Hera, mke wake na mungu mkuu wa kike wa Wagiriki alichukia tabia hii. Kwa hiyo Zeus alibadilisha umbo lake mara kwa mara. Alipotaka kumkaribia Europa mzuri aliingia kati ...

                                               

Ra

Nakala hii inahusu mungu Ra au Re wa Misri ya Kale. Kwa elementi ya kikemia yenye kifupi "Ra", angalia Radi. Ra pia: Re alikuwa mmoja wa miungu ya Misri ya Kale. Aliabudiwa hasa kama mungu wa Jua. Wamisri waliona alizaliwa kila asubuhi upande wa mashariki, na kufariki kila usiku upande wa magharibi. Usiku alisafiri kupitia kuzimu. Hii ndiyo sababu upande wa magharibi wa Nile ulijulikana kama "nchi ya wafu". Alichorwa na kichwa cha ndege wa kozi. Alitazamwa kama mkuu au mfalme wa miungu.

                                               

Osiris

Osiris alikuwa mmoja wa miungu ya Misri ya Kale. Katika mitholojia ya Kimisri aliabudiwa kama mungu wa uhai, kifo, mafuriko ya mto Nile, na maisha ya baadaye.

                                               

Benyamini wa Argol

Benyamini wa Argol alikuwa shemasi aliyeteswa na kuuawa kwa sababu ya imani yake katika dhuluma ya mfalme Vararane V. Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki kama mtakatifu mfiadini. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 31 Machi.

                                               

Guntram

Guntram alikuwa mfalme wa Orleans na Burgundy tangu mwaka 561. Alikuwa na tabia mbaya na kutenda dhambi nyingi, lakini imani ilimuongoza kuheshimu Kanisa na viongozi wake, kujenga monasteri na kuhamasisha uinjilishaji, kupatanisha ndugu zake, kusaidia maskini na kuwaombea kwa kufunga mwenyewe. Kwa sababu hiyo tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Machi.

                                               

Wafiadini 120 wa Uajemi

Wafiadini 120 wa Uajemi walikuwa Wakristo, wakiwemo wanaume 111 na wanawake 9, waliouawa kwa kuchomwa hai kwa sababu ya kukataa kumkana Yesu Kristo na kuabudu moto katika dhuluma ya mfalme Sabor II. Tangu kale wanaheshimiwa na Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki kama watakatifu wafiadini. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Aprili.

Mfalme
                                     

ⓘ Mfalme

Mfalme ni mtawala wa kiume juu ya nchi katika utaratibu wa ufalme. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka mzazi wake aliyekuwa mfalme pia. Lakini kuna pia wafalme waliochaguliwa au kuteuliwa kwa namna nyingine hasa kama mfalme aliyetangulia alikufa bila mrithi.

Utawala wa kifalme ilikuwa hali ya kawaida katika nchi nyingi za dunia kwa muda mrefu.

Mwanamke anayeshika nafasi ya mfalme huitwa "malkia".

Kama cheo kinaendelea katika ukoo mmoja kutoka mababa kwa watoto wao familia hii huitwa nasaba.

                                     

1. Madaraka ya mfalme

Madaraka ya wafalme walitofautiana kati ya nchi na nchi na kati ya kipindi na kipindi cha historia. Mifano ni:

  • Mfalme wa kikatiba imekuwa hali ya kawaida katika karne ya 19 na 20 pale ambako utaratibu wa kifalme umeendelea. Mfalme hatekelezi tena shughuli za serikali. Serikali inachaguliwa na bunge kwenye msingi wa kura wa raia wote jinsi ilivyopangwa katika katiba ya nchi. Nafasi ya mfalme unafanana na ile ya rais katika jamhuri. Kuna tofauti kama mfalme ana athira katika siasa au kama cheo chake ni cha heshima tu na hana uwezo wa kuingilia kati katika kazi za bunge na serikali. Mifano yake ni wafalme wa Skandinavia au pia utaratibu wa Uingereza na nchi za Jumuiya ya Madola zisizo jamhuri. Nafasi ya mfalme iko hasa kama vikundi ndani ya bunga havikubaliani kuhusu serikali mpya na hakuna upande mwenye kura nyingi kabisa.

Wafalme wa nchi kama Moroko na Yordani wana athira kubwa zaidi.

  • Mfalme mwenye mamlaka yote bila kufungwa na katiba alikuwa jambo la kawaida zamani lakini leo hii wamebaki wachache sana. Falme za aina ni Saudia, Omani, Qatar, Uswazi, Brunei na Bhutan inayoandaa katiba kwa mwaka 2008.
  • Mfalme wa sehemu ya taifa tu: mifano yake ni Kabaka wa Buganda au Asantehene wa Ashanti katika Ghana. Wafalme hawa wa jadi bado wanaheshimiwa na kuwa na athira kwa sababu wanatambuliwa na watu wao hata ndani ya jamhuri kubwa zaidi kuliko eneo la kabila au kundi lao.
                                     

2. Wafalme na watawala wengine

Hakuna utaratibu sanifu mtawala gani anastahili kuitwa "mfalme". Kwa kawaida anasimamia eneo au nchi ya kujitegemea lakini wengine huweka pia mashariti kuhusu ukubwa wa eneo lake.

Kwa maeneo fulani kuna vipindi katika historia ambako si rahisi kutofautisha kati ya wafalme na watawala wadogo wengine kama watemi, machifu n.k. Mara nyingi watawala wa Waswahili ambao hawakuwa na mamalaka nje ya eneo dogo la mji wao walijiita Sultani na Wareno waliwaita "reyes" wafalme. Hali hii ililingana na mifano mingine kama kati ya Wagiriki wa Kale ambako vilevile watawala wadogo juu ya miji walitumia cheo cha "mfalme".

Tazama pia: Kaisari, Mtemi