Back

ⓘ Kuhara
Kuhara
                                     

ⓘ Kuhara

Kuhara au kuendesha ni hali ya kupata choo chepesi au cha majimaji angalau mara tatu kwa siku. Kwa kawaida hudumu kwa siku chache na inaweza kusababisha upungufu wa maji mwilini kwa sababu ya ukosefu wa maji. Ishara za upungufu wa maji mwilini kwa kawaida huanza na ukosefu wa kunyooka kwa kawaida kwa ngozi na mabadiliko katika tabia za mtu. Hii inaweza kuendelea na kusababisha upungufu wa mkojo, upungufu wa rangi ya ngozi, a mpigo wa haraka wa moyo, na upungufu wa mwitikio inapoendelea kuwa mbaya zaidi. Hata hivyo, huenda kinyesi chepesi lakini kisicho cha majimaji katika watoto wanaonyonya, kikawa cha kawaida.

Sababu kuu ya maambukizo ya matumbo huwa ni kwa sababu ya kvirusi, bakteria, kimelea, au hali inayojulikana kama gastroenteritis. Maambukizo haya kwa kawaida hupatikana kutokana na chakula au maji ambayo yameambukizwa na kinyesi, au moja kwa moja kutoka kwa mtu mwingine ambaye ameambukizwa. Huenda ikagawanywa kwa aina tatu: kuhara maji kwa muda mfupi, kuhara damu kwa muda mfupi, na ukiwa utadumu kwa zaidi ya wiki mbili, kuhara kunaoendelea. Kuhara maji kwa muda mfupi huenda kukasababishwa na maambukizo ya kipindupindu. Ikiwa kuna damu inajulikana kama kuhara. Kuna sababu kadhaa zisizo za kuambukizwa ambazo zinaweza pia kusababisha kuhara ikiwa ni pamoja na: hyperthyroidism, kutovumilia laktosi, ugonjwa wa kuvimba matumbo, baadhi ya dawa, na ugonjwa wa matumbo yanayowashwakati ya sababu nyingine. Katika visa vingi uchunguzi wa kinyesi hauhitajiki ili kuthibitisha sababu halisi.

Unaweza kuzuia kuhara kunaoweza kuambukizwa kwa usafi ulioboreshwa, maji masafi ya kunywa, na kunawa mikono. Kunyonyesha kwa angalau miezi sita kunapendekezwa hata pia chanjo dhidi ya rotavirus. Dawa ya maji ya kunywa ORS, ambayo ni maji masafi yenye viwango vinavyofaa vya chumvi na sukari, ndio matitabu yanayopendekezwa. Tembe za Zinki zinapendekezwa pia. Matibabu haya yamekadiriwa kuwa yamewaokoa watoto milioni 50 kati ya miaka 25 iliyopita. Wakati watu wanahara inapendekezwa kwamba waendelee kula chakula chenye afya na watoto waendelee kunyonya. Ikiwa ORS ya kuuzwa hazipatikani, suluhisho za nyumbani zinaweza kutumiwa. Kwa wale wanoendesha sana, maji ya kudungwa ndani ya venayanaweza kuhitajika. Hata hivyo, katika visa vingi, inaweza kudhibitiwa vizuri kwa maji mdomoni. Viua wadudu, ijapokuwa haitumiwi sana, inaweza kupendekezwa katika visa vichache kama wale wanaohara damu na wana joto jingi, kuhara kunaotokana na kusafiri, na wale wanaopata bakteria au vimelea fulani katika kinyesi chao. Loperamide inaweza kusaidia kupunguza kuhara lakini haipendekezwi kwa wale wenye maradhi makali.

Karibu visa bilioni 1.7 hadi 5 za kuhara hufanyika kila mwaka. Vimekita mizizi sana katika nchi zinazokua, ambapo watoto wadogo wanahara karibu mara tatu kwa mwaka. Duniani kote, hadi 2012, ilikuwa sababu ya pili kuu ya watoto kufariki wakiwa chini ya miaka 5 milioni 0.76 au 11%. Matukio ya mara kwa mara ya kuhara huwa sababu kuu ya utapiamlo na sababu kuu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano. Matatizo mengine ya muda mrefu ambayo yanaweza kutokea ni pamoja na ukuaji duni wa kimwili na kiakili.

                                     
 • wa kuhara uliojulikana kama kuhara damu au kuharisha damu ni maradhi yanayotokana na machafuko ya ini na hasa matumbo ambayo inasababisha kuhara ambapo
 • katika faila Nematoda anayeishi katika sikamu ya watu. Anaweza kusababisha kuhara na damu, na anemia, katika watoto hasa. Minyoo - mjeledi wana sehemu nyembamba
 • dafu hutumika pia kama dawa, kwa mfano kwa mtu mwenye kisukari, tumbo la kuhara au upungufu wa homoni, hususan zile zinazotengenezwa na kongosho kwa ajili
 • kunyweka, au kutumika kama losheni au kuogea. Gome hutumiwa kama dawa ya kuhara na matumizi ya ukoma. Mchemsho wa gome hutumiwa kutibu kikohozi na kutuliza
 • na tamu na mbegu nyeusi. Majani hutumika kama chai ili kutibu mafua na kuhara damu, na pia husaidia mfumo wa umeng enyaji wa chakula. Mizizi ya mstafeli
 • mwembamba. Bakteria hizo ambazo huitwa vibriocholerae huweza kusababisha kuhara sana na kutapika sana pamoja na homa kali. Maambukizi hutokea hasa kupitia
 • dubwana: Pithovirus sibericum Kundi II Parvovirus B19 Kundi III Virusi vya kuhara Rotavirus B Kundi IV Virusi vya rubella Kundi V Virusi vya mafua: Hantavirus
 • tumbo na kichomi, kichefuchefu na kutapika kunaweza kuanza siku ya tatu. Kuhara huweza kuendelea kwa wiki. Wikimedia Commons ina media kuhusu: Marburg virus
 • Uswisi, wakiunganishwa na hasa kutokana na malaria, shida za kupumua au kuhara - magonjwa ambayo yanaweza kukingwa. Hili suala huleta madhara makubwa hasa
 • zaidi ya ukambi hutokea kwa takriban asilimia 30 na yanaweza kujumuisha kuhara upofu, inflamesheni ya ubongo, na nimonia miongoni mwa mengine. Rubela
 • inahusu tumbo gastro - pamoja na chango entero - na kusababisha kuhara kutapika, maumivu ya tumbo na kupata kiharusi. Ingawa haihusiani na mafua