Back

ⓘ Msamaha
Msamaha
                                     

ⓘ Msamaha

Msamaha ni uamuzi wa Mungu au mtu wa kutofuatilia makosa ambayo ametendewa.

Ni kinyume kabisa cha kisasi lakini pia ni tofauti na kutetea, kusahau na kupatana. Kwa kawaida unaendana na ombi la mtu aliyekiri makosa.

Pengine neno msamaha linatumika kwa uamuzi wa rais au mtawala mwingine wa kutoa gerezani baadhi ya watu kabla adhabu yao haijakamilika, hasa katika nafasi ya kuingia madarakani au ya sikukuu nyingine. Vilevile kuhusu ondoleo la deni au wajibu mwingine.

Elimunafsia inaonyesha kwamba utoaji wa msamaha unaleta nafuu kwa mtu anayeutoa, na nafuu hiyo inaweza kuenea kutoka nafsini hata mwilini,

Dini nyingi zinasisitiza umuhimu wa kusamehe wengine kuhusiana na haja ya kusamehewa nao lakini pia na Mungu kutokana na ukosefu unaomuathiri kila binadamu.