Back

ⓘ Papa
                                               

Jimbo Katoliki la Zanzibar

Jimbo Katoliki la Zanzibar ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, likienea katika visiwa vya Unguja na Pemba vya Tanzania visiwani, jumla kilometa mraba 2.332. Makao makuu yake ni katika mji wa Zanzibar na linahusiana na Jimbo kuu la Dar-es-Salaam. Kanisa kuu limewekwa wakfu kwa heshima ya. Askofu wa jimbo ni Augustine Ndeliakyama Shao, C.S.Sp.

                                               

Paulo wa Narbonne

Kadiri ya wanahistoria Wakristo. chini ya kaisari Decius 250 BK, Papa Fabian alituma maaskofu 7 kutoka Roma kwenda Gallia Ufaransa wa leo wakahubiri Injili: Grasyano huko Tours, Trofimo huko Arles, Paulo huko Narbonne, Saturnini huko Toulouse, Denis huko Paris, Austremoni huko Clermont na Martial huko Limoges. Tangu kale Paulo anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini ingawa hakuuawa kwa ajili ya imani wakati wa dhuluma ya kaisari Decius. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Machi.

                                               

Nikola Owen

Nikola Owen, S.J. alikuwa bradha Mjesuiti aliyesaidia sana kudumisha imani Katoliki nchini Uingereza. Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius IX mwaka 1929 na mtakatifu mwaka 1976 na Papa Paulo VI. Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe ya kifodini chake.

                                               

Benedikta Cambiagio Frassinello

Benedikta Cambiagio Frassinello alikuwa mwanamke wa Italia kaskazini ambaye, baada ya kuolewa, alishika maisha ya kitawa pamoja na mume wake na hatimaye alianzisha shirika la Masista Wabenedikto wa Maongozi ya Mungu kwa ajili ya malezi ya wasichana. Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 10 Mei 1987 na mtakatifu tarehe 19 Mei 2002. Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 21 Machi.

                                               

Prokopi wa Sazava

Prokopi wa Sazava alikuwa padri kanoni, halafu kwa kuacha mke na mtoto akawa mmonaki Mbenedikto, mkaapweke na hatimaye abati wa monasteri aliyoianzisha Sazava. Tarehe 2 Juni 1204 alitangazwa na Papa Inosenti III kuwa mtakatifu. Sikukuu yake ni tarehe 25 Machi.

                                               

Lusia Filippini

Lusia Filippini alikuwa mwanamke wa Italia ya kati ambaye, kwa msaada wa kardinali Marcantonio Barbarigo, alianzisha shirika la Walimu wa Kikristo kwa ajili ya malezi ya wasichana. Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 13 Juni 1926 na mtakatifu tarehe 22 Juni 1930. Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Machi.

Papa
                                     

ⓘ Papa

Kwa samaki anayeitwa kwa Kiswahili "papa" tazama papa samaki

Papa ni cheo cha kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote. Cheo hicho kinategemea kile cha askofu wa Roma.

                                     

1. Asili

Kiasili neno la Kilatini "Papa" linamaanisha "Baba", nalo likawa cheo kutokana na nia ya kumtaja askofu wa Roma kwa heshima ya pekee. Msingi wa heshima hiyo ni imani ya Wakatoliki kuwa askofu wa Roma ni mwandamizi wa Petro, mkuu wa mitume wa Yesu.

Wakatoliki huamini ya kwamba Petro alipewa na Yesu kazi ya kuongoza Kanisa lote kwa niaba yake na ya kwamba jukumu hilo linaendelea kati ya waandamizi wa Petro kwenye kiti cha askofu wa Roma ambacho kwa heshima kinaitwa Ukulu mtakatifu.

                                     

2. Historia

Upapa ni kati ya vyeo vya zamani zaidi duniani na umeathiri sana historia ya binadamu kwa miaka karibu 2000.Athari hiyo iliweza kuwa nzuri au mbaya, kadiri ya matendo ya mhusika.

Kwa muda mrefu mamlaka ya Papa upande wa siasa, hasa juu ya mikoa ya Italia ya Kati, ilisababisha nchi nyingine na koo tajiri za Roma zijiingize katika uchaguzi ili kupitisha watu wao, hata wasiofaa. Upande mwingine, Mapapa waliathiriwa na utamaduni na mazingira ya nyakati zao, hasa tapo la Renaissance, kiasi cha kuzama katika anasa.

Baada ya Dola la Papa kutekwa na Ufalme wa Italia 1860-1870, Mapapa wameweza kushughulikia zaidi mambo ya kiroho na kujitokeza kwa ubora.Kwa miaka ya karibuni inatosha kumfikiria Papa Yohane Paulo II na mchango wake katika kuangusha ukomunisti katika Ulaya Mashariki.

                                     

3. Majina ya mapapa

Papa huchaguliwa na makardinali wa Kanisa Katoliki baada ya mtangulizi wake kufa au kungatuka. Baada ya kuchaguliwa papa mpya anaweza akajipatia jina jipya. Tangu tarehe 13 Machi 2013 ni Papa Fransisko, ambaye awali aliitwa Jorge Mario Bergoglio, kutoka Argentina.

Majina ya mapapa wengine wa Kanisa Katoliki yanapatikana katika orodha ya mapapa.

                                     

4. Marejeo mengine

 • Dollison, John 1994. Pope-pourri. New York: Simon & Schuster. ISBN 978-0-671-88615-8.
 • Brusher, Joseph S. 1959. Popes Through the Ages. Princeton, N.J: Van Nostrand. OCLC 742355324.
 • Maxwell-Stuart, P. G. 1997. Chronicle of the Popes: The Reign-by-Reign Record of the Papacy from St. Peter to the Present. London: Thames and Hudson. ISBN 0-500-01798-0.
 • Norwich, John Julius 2011. The Popes: A History. London: Chatto & Windus. ISBN 978-0-7011-8290-8.
 • Chamberlin, E. R. 1969. The Bad Popes. New York: Dial Press. OCLC 647415773.
                                     

5. Viungo vya nje

 • The Holy See - The Holy Father - website for the past and present Holy Fathers since Papa Leo XIII
 • The Authority of the Pope: Part I Archived Septemba 3, 2011 at the Wayback Machine.
 • Data Base of more than 23.000 documents of the Popes in latin and modern languages
 • The Authority of the Pope: Part II Archived Septemba 4, 2011 at the Wayback Machine.
 • Origins of Peter as Pope Archived Septemba 4, 2011 at the Wayback Machine.
 • Pope Endurance League - Sortable list of Popes
                                     
 • Papa Valentino alikuwa Papa kwa wiki chache tu kuanzia tarehe 1 Septemba 827 hadi kifo chake mwezi Oktoba 827. Alimfuata Papa Eugenio II akafuatwa na
 • Papa Sisinnio alikuwa Papa kwa wiki tatu tu kuanzia tarehe 15 Januari 708 hadi kifo chake tarehe 4 Februari 708. Alimfuata Papa Yohane VII akafuatwa na
 • da Castiglione. Alikuwa mpwa wa Papa Urban III. Alimfuata Papa Gregori IX akafuatwa na Papa Inosenti IV. Kuhusu Papa Celestino IV katika Kamusi Elezo
 • Papa Nikolasi V 15 Novemba 1397 24 Machi 1455 alikuwa Papa kuanzia tarehe 6 Machi 1447 hadi kifo chake. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Tommaso Parentucelli
 • Papa Eugenio II alikuwa Papa kuanzia tarehe 11 Mei 824 hadi kifo chake tarehe 27 Agosti 827. Alimfuata Papa Paskali I akafuatwa na Papa Valentino. Papa
 • Papa Callixtus II alikuwa Papa kuanzia tarehe 1 Februari 1119 hadi kifo chake tarehe 13 Desemba 1124. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Guido wa Vienna. Alimfuata
 • Papa Theodor II alikuwa Papa kwa siku ishirini hadi kifo chake mwezi wa Desemba 897. Jina lake la kuzaliwa pia lilikuwa Theodorus. Alimfuata Papa Romanus
 • Papa Agapeto II alikuwa Papa kuanzia tarehe 10 Mei 946 hadi kifo chake mnamo Oktoba, 955. Jina lake la kuzaliwa halijulikani. Alimfuata Papa Marinus II
 • Papa Celestino II alikuwa Papa kuanzia tarehe 25 Septemba 1143 hadi kifo chake tarehe 8 Machi 1144. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Guido wa Castello. Alimfuata
Rosa Venerini
                                               

Rosa Venerini

Rosa Venerini alikuwa bikira maarufu kwa huduma yake katika malezi ya wasichana. Kwa ajili hiyo alianzisha shule ya kwanza kwa wasichana tu nchini Italia, halafu shirika la masista walimu linalodumu hadi leo. Alipofariki shule zake zilikuwa 40 tayari. Papa Pius XII alimtangaza mwenye heri tarehe 4 Mei 1952, halafu Papa Benedikto XVI akamtangaza mtakatifu tarehe 15 Oktoba 2006. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyoaga dunia.

Stanislaus Kazimierczyk
                                               

Stanislaus Kazimierczyk

Stanislaus Kazimierczyk alikuwa padri kanoni wa Kanisa Katoliki nchini Poland maarufu kwa ibada yake kwa Yesu ekaristi na kwa huruma yake kwa maskini. Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 18 Aprili 1993. Halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 17 Oktoba 2010. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Mei.

Maria Dominika Mazzarello
                                               

Maria Dominika Mazzarello

Maria Dominika Mazzarello alikuwa mtawa wa Piemonte, Italia Kaskazini, mwanzilishi wa Mabinti wa Bikira Maria Msaada wa Wakristo pamoja na Yohane Bosco. Bikira huyo alijitolea maisha yake pamoja na shirika lake hilo kwa malezi ya Kikristo ya wasichana. Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI tarehe 20 Novemba 1938, halafu mtakatifu na Papa Pius XII tarehe 24 Juni 1951. Sikukuu yake hufanyika tarehe 14 Mei.

Viborada
                                               

Viborada

Viborada alikuwa mkaapweke mwenye karama za pekee ambaye hatimaye aliuawa na Wahungari Wapagani. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Tena ndiye wa kwanza kutangazwa na Papa. Hilo lilifanywa na Papa Klementi II mwaka 1047. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Mei.

Fransisko De Geronimo
                                               

Fransisko De Geronimo

Fransisko De Geronimo, S.J. alikuwa padri wa Italia Kusini na mtawa wa Shirika la Yesu maarufu kwa mahubiri yake hasa kwa maskini Alitangazwa mwenyeheri na Papa Pius VII mwaka 1806, halafu mtakatifu na Papa Gregori XVI mwaka 1839. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Mei.

Amato Ronconi
                                               

Amato Ronconi

Amato Ronconi alikuwa Mkristo maarufu kwa kuishi miaka mingi kwa toba na hija. Alijenga makanisa na vituo vya kuhudhumia maskini, ambao aliwagawia mali yake yote. Kwa sababu hizo, wengine wanasema alikuwa Mfransisko wa Utawa wa Tatu. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Hiyo ilithibitishwa kwanza na Papa Pius VI tarehe 17 Aprili 1776, halafu na Papa Fransisko tarehe 23 Novemba 2014. Sikukuu yake ni tarehe 8 Mei.

Severino wa Settempeda
                                               

Severino wa Settempeda

Severino wa Settempeda alikuwa Mkristo ambaye, alipofiwa wazazi wake, aliamua pamoja na ndugu yake Viktorini wa Camerino kuwagawia maskini urithi wao mkubwa na kwenda kuishi upwekeni kwenye Mlima Nero. Papa Vigili alimfanya yeye askofu wa Settempeda na Viktorini askofu wa Camerino Italia ya Kati. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Mei.

Viktorini wa Camerino
                                               

Viktorini wa Camerino

Viktorini wa Camerino alikuwa Mkristo ambaye, alipofiwa wazazi wake, aliamua pamoja na ndugu yake Severino wa Settempeda kuwagawia maskini urithi wao mkubwa na kwenda kuishi upwekeni kwenye Mlima Nero. Papa Vigili alimfanya yeye askofu wa Camerino Italia ya Kati na Severino askofu wa Settempeda. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Juni.

Yosefu Maria Rubio
                                               

Yosefu Maria Rubio

Yosefu Maria Rubio alikuwa padri wa Shirika la Yesu, ambaye anaitwa mtume wa Madrid kwa jinsi alivyotangaza Injili huko, hasa katika mitaa maskini. Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 6 Oktoba 1985 akamtangaza mtakatifu tarehe 4 Mei 2003. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.

Jovenale wa Narni
                                               

Jovenale wa Narni

Jovenale wa Narni anakumbukwa kama askofu wa kwanza wa mji huo. Inasemekana alikuwa na asili ya Afrika Kaskazini akapewa uaskofu na Papa Damaso I. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake

Margerita wa Città di Castello
                                               

Margerita wa Città di Castello

Margerita wa Città di Castello alikuwa bikira kipofu na mlemavu wa viungo tangu kuzaliwa. Baada ya kukataliwa na wazazi na monasteri mbalimbali alijiunga na Utawa wa Tatu wa Dominiko Guzman. Utakatifu wake ulioheshimika tangu kale ulithibitishwa na Papa Fransisko tarehe 24 Aprili 2021. Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe aliyoaga dunia.

Eutropi wa Saintes
                                               

Eutropi wa Saintes

Eutropi wa Saintes alikuwa askofu wa kwanza wa Saintes, Akwitania, leo nchini Ufaransa alikotumwa na Papa akitokea Roma au Persia. Inasemekana aliuawa wakati wa dhuluma ya Dola la Roma dhidi ya Ukristo lakini hakuna hakika. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kwama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Aprili.

                                               

Yohane Grande

Yohane Grande Román, O.H. alikuwa bradha wa shirika la kihospitali la Mt. Yohane wa Mungu nchini Hispania. Kabla ya hapo alikuwa ameanzisha hospitali mwenyewe, ila aliamua kuiunga na shirika hilo mwaka 1574. Alipohudumia wagonjwa wa tauni aliambukizwa akafa. Papa Pius IX alimtangaza kwanza mwenye heri tarehe 13 Novemba 1858, halafu Yohane Paulo II akamtangaza mtakatifu tarehe 2 Juni 1992. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.

Users also searched:

...
...
...