Back

ⓘ Utiifu
Utiifu
                                     

ⓘ Utiifu

Utiifu, katika maisha ya binadamu, ni aina ya "mwenendo ambayo mtu anafuata maelekezo au maagizo ya wazi aliyopewa na mwenye mamlaka".

Ni tofauti na mtu kufuata athari ya wenzake au mkondo wa umati.

Kimaadili utiifu unaweza kutazamwa kwa namna mbalimbali, chanya au hasi, hasa kulingana na uadilifu au uovu wa agizo lenyewe, kwa mfano lile la Hitler kuhusu mauaji ya kimbari ya Wayahudi.

                                     

1. Katika jamii

Utamaduni wa nchi nyingi unatazama utiifu kama adili; hasa jamii kwa kawaida inadai watoto waheshimu na kutii wazazi wao na wazee wengine, lakini pengine watumishi na watumwa walidaiwa kutii mabwana wao, na watu wa rangi fulani kutii wale wa rangi nyingine.

Mbali ya hayo, wananchi wanatarajiwa kutii watawala halali, na wanadini kumtii Mungu.

                                     

2. Katika dini

Utiifu ni muhimu katika dini mbalimbali. Hasa Uislamu unaufanya kiini cha imani neno Islam linamaanisha "kukubali, kusalimu amri".

Katika Ukristo, ni hasa watawa wanaowajibika kuishi kwa utiifu katika jumuia zao ili kutimiza kwa umoja mapenzi ya Mungu.

Mbali ya hao, kielelezo cha Wakristo wote ni Yesu Kristo, aliyesifiwa kwa kumtii Mungu Baba hata kufa - kufa msalabani Fil 2:1-18.

Kwa Kigiriki, lugha ya Agano Jipya, utiifu ni sawa na usikivu wa Neno la Mungu, hivyo Mtume Paulo alisisitiza utiifu wa imani.

                                     

3. Viungo vya nje

  • Science Aid: Obedience High school level Psychology
  • "Obedience, Consumerism, and Climate Change" by Yosef Brody, Ph.D.
  • Catholic Encyclopedia article on obedience