Back

ⓘ Majira ya baridi
Majira ya baridi
                                     

ⓘ Majira ya baridi

Majira ya baridi ni mojawapo kati ya majira manne ya kanda za wastani, na halijoto yake ni ya baridi kuliko majira mengine. Ni kinyume cha majira ya joto au chaka.

Pengine baridi inakuwa kali sana na kuendana na barafuto: ndiyo maana maeneo mengine ya dunia hayana wakazi wa kudumu, hasa bara la Antaktiki.

Yanafuata majira ya kupuputika majani kwa Kiingereza Fall au Autumn na kutangulia majira ya kuchipua kwa Kiingereza Spring.

Majira hayo yanatokea duniani kwa nyakati tofauti kadiri eneo husika lilivyo kaskazini au kusini kwa ikweta. Hata katika nchi ileile, kwa mfano Kenya, majira ni tofauti upande huu na upande huu wa ikweta.

Majira hayo tofauti hupatikana zaidi katika ukanda wa tropiki.

                                     

1. Wanyama, mimea, binadamu na majira ya baridi

Ili kuhimili ukali wa majira ya baridi, wanyama wengi wana njia mbalimbali za kimaumbile na kitabia.

 • Uhamaji ni mbinu mojawapo inayotumiwa hasa na ndege wakati wa baridi. Hata hivyo, ndege wengi hawahami. Baadhi ya vipepeo pia huhama msimu huu.
 • Wanyama wengine hulala ili kupunguza shughuli metaboli mwilini wakati wa majira ya baridi. Wanyama hao, kama vile vyura, nyoka, na popo huamka msimu huu unapomalizika.
 • Wanyama wengine huhifadhi chakula watakachokula wakati wa majira ya baridi.
 • Wanyama wengine huishi majira ya baridi lakini hujibadilisha kama vile rangi. Rangi ya manyoya hubadilika kuwa nyeupe ili kufanana na theluji. Mifano ya wanyama hawa ni kama vile mbweha wa Aktiki, sungura wa mlimani, n.k.
 • Wanyama wengine wenye manyoya hukuza manyoya yao kama wakati wa baridi; hii inaboresha uwezo wa manyoya kuhifadhi joto.
 • Msimu huu huathiri pia tabia za wanyama. Kwa mfano panya kawaida huishi chini ya theluji.
 • Baadhi ya mimea ya kila mwaka haiwezi kuishi wakati wa baridi. Hata hivyo, mimea mingine ya kila mwaka inahitaji baridi kukamilisha mzunguko wa maisha yao. Baadhi ya mimea ya msimu hufaidika kwa kufunikwa na theluji wakati mimea mikubwa huacha sehemu ya juu kulala huku mizizi yake ikihifadhiwa na theluji.

Binadamu nao hufanya mambo mbalimbali ili kuweza kukabiliana na majira ya baridi.

 • Msaada wa kibinadamu hutolewa kwa mfano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi UNHCR, kama vile usambazaji wa vitu ikiwa ni pamoja na mablanketi, mafuta ya taa, mazulia ya sakafu yanayopasha nyumba joto, n.k.
 • Baadhi ya nyumba za majira ya joto, ambazo zilijengwa kwa ajili ya matumizi ya majira ya joto tu zinahitaji kutunzwa wakati wa majira ya baridi. Wakati wa msimu huu nyumba hizo hutunzwa kwa kufungwa, kuzima maji, umeme, na mistari ya simu, na kulinda vipengele mbalimbali kutokana na theluji kubwa.

Kwa mfano katika eneo la New England, nchini Marekani, familia nyingi tajiri zilizoishi humo wakati wa karne ya 19 zilikuwa na nyumba za majira ya joto milimani ili kuondoka mwanzoni mwa magonjwa kwa homa ya njano na magonjwa mengine ambayo mara nyingi yalijitokeza katika miezi ya majira ya joto.

 • Vifaa vinavyotumiwa wakati wa majira ya baridi kama vile magari, vifaa vya elektroniki, vifaa vya kilimo na umwagiliaji, boti na redio pamoja na vifaa vya kawaida huwezeshwa kutumiwa msimu huu kwa njia mbalimbali kama matumizi ya kemikali maalum.
 • Mabwawa ya samaki yanahitaji hatua kadhaa za ziada ili kuhakikisha kuwa samaki wanaishi vyema wakati wa baridi.
                                     

2. Viungovyanje

 • Jinsi ya kutunza boti
 • Hydraulic pressure in that part of the water last to freeze Archived Aprili 27, 2012 at the Wayback Machine.
 • Umuhimu wa msaada wa kibinadamu wakati wa majira ya baridi
 • Video fupi ya katuni kuhusu sababu za kuwepo kwa majira ya baridi
 • Jinsi ya kuipa nyumba joto wakati wa majira ya baridi
                                     
 • wastani. Yanafuata majira ya baridi kwa Kiingereza winter na kutangulia majira ya joto kwa Kiingereza summer Majira hayo yanatokea duniani kwa
 • Majira ya kupuputika majani kwa Kiingereza Fall au Autumn ni mojawapo kati ya majira manne ya kanda za wastani, na halijoto yake ni ya baridi kiasi
 • Pasifiki. Majira ya joto ni kuanzia Disemba hadi Machi, na majira ya baridi kuanzia Juni hadi Septemba. Nusutufe ya kaskazini Ikweta Tropiki ya Saratani
 • kuongezeka kwa hewa baridi hivyo katika nchi zenye majira baridi mimea huanza kuopoteza majani na kuandaa usingizi. Sikusare ya otomnia inakadiriwa kuwa
 • mfasiri kutoka nchi ya Uswidi. Hasa ameandika mashairi kuhusu majira ya baridi nchini mwake. Mwaka wa 2011 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi. 17 dikter
 • Lituanya. Kuna wakazi 74, 563 mwaka 2009 Mji ulianzishwa 1581. Eneo lake ni 45 km². Majira ya baridi katika Alytus Mto Nemunas Alytus www.alytausgidas.lt
 • Mimea ya nchi ambako jalidi ni hali ya kawaida wakati wa majira ya baridi ina uwezo wa kukauka kabla ya majira ya jalidi kuanza. Katika mazingira ya joto
 • inaweza kufika, kwa hiyo sentigredi C - 40 zimeshapimwa kwenye majira ya baridi lakini majira ya joto sentigredi za C 40 zinawezekana pia. Mwaka 2008 Taklamakan
 • kuanzia Juni hadi Septemba, na majira baridi kuanzia Disemba hadi Machi. Nusutufe ya kusini Ikweta Tropiki ya Saratani Tropiki ya Kaprikoni Duara la Aktiki