Back

ⓘ Ujuzi
Ujuzi
                                     

ⓘ Ujuzi

Ujuzi maana yake ni kufahamu, kujua na kuelewa hali, habari na maelezo yanayohusu mazingira tunapoishi. Tunapata ujuzi kwa maarifa yetu au kwa njia ya kufundishwa tukitazama, kutambua, kulinganisha na kutafakari yale tuliyoona na kujifunza.

Kimsingi tunaona tofauti kati ya ujuzi na rai au hoja tupu. Rai na hoja zinakuja pamoja na hisia na maarifa ambayo mara nyingi haikutafakariwa kimakini. Kinyume chake ujuzi ni yale tunayoona kuwa yana kiwango kikubwa cha uhakika baada ya kujadiliwa na watu wengi katika mchakato unaoeleweka. Lakini kila ujuzi una kiwango cha kukosa uhakika kwa sababu uwezekano wa makosa katika kuelewa uhalisia unabaki kila wakati.

Katika falsafa, elimu ya jinsi ya kupata ujuzi huitwa epistomolojia. Mwanafalsafa Plato alieleza ujuzi kuwa "rai ya kweli yenye msingi mzuri" kwa Kiingereza "justified true belief".

                                     
 • Idadi ni jumla ya viumbehai, vitu au mambo yanayohesabika. Ujuzi wa idadi ni muhimu katika fani nyingi, kwa mfano takwimu. Ndiyo sababu tangu zamani nchi
 • ujuzi au maarifa aliyonayo binadamu katika kufanya jambo fulani. Katika kueleza dhana ya ufundi tunamhusisha binadamu zaidi, kwani ndiye mwenye ujuzi
 • upande wowote. Nadharia inaweza kuwa jumla ya ujuzi ambao unaweza au usiweze kuambatana na mafunzo ya kimatendo. Kuunda nadharia ni kutengeneza ujuzi
 • inayotumiwa kujitoa katika shida ama kuweza kupata kitu, kwa kutumia elimu au ujuzi Ujuzi huo unaweza ukawa wa kuzaliwa nao au ukatokana na mang amuzi ya maisha
 • katika taaluma fulani. Mtaalamu anaaminika katika fani yake kama chanzo cha ujuzi au maarifa. Utaalamu huo unaweza kutegemea elimu, lakini pengine pia malezi
 • kuongeza maarifa ya elimu, ikiwa ni pamoja na ujuzi wa wanadamu, utamaduni na jamii, na matumizi ya hisa hii ya ujuzi wa kuunda maombi mapya. Inatumika kuanzisha
 • jinsi binadamu anavyokabili maisha katika mazingira yake. Hiyo inajumlisha ujuzi imani, sanaa, maadili, sheria, desturi n.k. ambavyo mtu anajipatia kama
 • Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani. Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.
 • Mwanahisabati ni mtaalamu anayetumia ujuzi mpana wa hisabati katika kazi yake, ili kutatua mafumbo ya kihisabati. Archimedes, 287 KK hivi 212 KK Muhammad
 • yanayotoka kwenye makubwa. Ujuzi wa kisasa kutokana na utafiti wa DNA ndani ya seli za viumbehai unaendelea kuongeza ujuzi wetu kwa hiyo katika mengi
 • majadiliano kuhusu maisha. Mara nyingi majadiliano hufanywa kwenye kikundi cha watu wawili au zaidi ili kutatua jambo au kuongeza ujuzi wa jambo fulani.