Back

ⓘ Kuwait
Kuwait
                                     

ⓘ Kuwait

Historia ya Kuwait ilianza kama utemi mdogo chini ya familia ya Al-Sabah iliyokuwa chini ya Sultani wa Uturuki aliyetawala nchi jirani ya Irak hadi vita kuu ya kwanza ya dunia.

Tangu kuingia kwa Waingereza katika nchi za ghuba, mwaka 1899 watawala wa Kuwait walijiweka chini ya ulinzi wa Uingereza kwa sababu waliuona afadhali kuliko ukuu wa Uturuki.

Waingereza walitetea hali yake ya pekee dhidi ya Waosmani na baadaye dhidi ya Saudia.

Baada ya kuporomoka wa dola la Uturuki Kuwait iliendelea kama nchi lindwa chini ya Uingereza hadi kupata uhuru wake tarehe 19 Juni 1961.

Katika miaka iliyofuata Kuwait iliona madai ya Irak ya kuwa tangu zamani Kuwait ni mkoa wake uliotengwa na ukoloni.

Tarehe 2 Agosti 1990 dikteta wa Irak Saddam Hussein alivamia Kuwait na kuiteka. Katika vita ya pili ya ghuba Marekani pamoja na nchi nyingine ilishambulia jeshi la Irak katika Kuwait na kurudisha serikali ya Emir al Sabah.

                                     

1. Watu

Kati ya wakazi 4.044.500 asilimia 30 pekee ni wananchi au Wakuwait wenyewe. Wengine wote ni watu waliokuja kufanya kazi na kuishi hapo. Pamoja na wahamiaji kutoka nchi jirani, 60% ya wakazi ni Waarabu. Zaidi ya 30% tena wana asili ya India au nchi nyingine za Asia. Waafrika ni 76.698.

Lugha rasmi ni Kiarabu; wananchi wanakiongea kwa lahaja maalumu. Kiingereza pia kinatumika hasa, hasa katika biashara.

Upande wa dini, wananchi karibu wote ni Waislamu, hasa Wasuni 70%, lakini pia Washia 30%. Ndiyo dini rasmi. Wakristo ni zaidi ya 10%, lakini karibu wote ni wahamiaji. Wahindu kutoka India ni wengi zaidi kidogo karibu 15%. Wabuddha ni 2%.

                                     

2. Uchumi

Nchi ni tajiri kutokana na wingi wa mafuta ya petroli yaliyopo chini ya ardhi yake. Akiba zake ni kama 10% za akiba za dunia yote. Kabla ya kupatikana kwa mafuta mwaka 1938 nchi ilikuwa maskini lakini sasa ni kati ya nchi tajiri zaidi duniani.

Kabla ya kugunduliwa kwa mafuta palikuwa na kilimo kidogo sana, halafu ufugaji na hasa uvuvi baharini.

                                     
 • Jiji la Kuwait au Kuwait City Kiarabu: madinat - al - Kuwait - مدينة الكويت ni mji mkuu wa nchi ya Kuwait mwenye wakazi 32.000 mjini penyewe na takriban
 • Historia ya Kuwait inahusu eneo ambalo leo linaunda ufalme wa Kuwait Historia ya Kuwait ilianza kama utemi mdogo chini ya familia ya Al - Sabah iliyokuwa
 • Watani alkuwait au Taifa langu Kuwait ni wimbo wa taifa la Kuwait وطني الكويت سلمت للمجد وعلى جبينك طالع السعد وطني الكويت وطني الكويت وطني الكويت سلمت
 • Inaanza kwenye Mlango wa Hormuz na kuendelea hadi mwisho wake upande wa Kuwait na mdomo wa Shatt al Arab. Ni kawaida ya kuiita ghuba ya Uajemi lakini katika
 • Armenia Bahrain Kupro Sinai rasi Misri Palestina Iran Iraq Israel Jordan Kuwait Lebanon Oman Pakistan Baluch pekee Qatar Saudia Syria Falme za Kiarabu
 • الصباح 16 Juni 1929 - 29 Septemba 2020 alikuwa Emir wa Kuwait na Kamanda wa Vikosi vya Jeshi vya Kuwait Aliapishwa tarehe 29 Januari 2006 baada ya kuthibitishwa
 • ni nchi kubwa kati ya nchi za Bara Arabu. Imepakana na Yordani, Iraq, Kuwait Qatar, Bahrain, Falme za Kiarabu, Oman na Yemen. Kuna pwani ya Ghuba la
 • KW au kw ni kifupi cha: Kodi ya IATA ya Kelowna Flightcraft, Kanada Kodi ya ISO 639 - 1 ya lugha ya Kernewek Kodi ya ISO 3166 - 1 ya nchi ya Kuwait
 • pamoja na sehemu ya jangwa la Shamu na ya milima ya Zagros. Imepakana na Kuwait Saudia, Yordani, Syria, Uturuki na Uajemi. Kuna pwani fupi kwenye Ghuba
 • OK au ok ni kifupi cha: Kodi ya IATA ya CSA Czech Airlines, Czech Republic Kodi ya ICAO ya Kuwait Jimbo la Oklahoma, Marekani O.K. Okay
 • KU au ku ni kifupi cha: Kodi ya IATA ya Kuwait Airways Kodi ya ISO 639 - 1 ya lugha ya Kodi ya ISO 3166 - 1 ya nchi ya
 • Airport Nigeria Kano - Mallam Aminu Kano International Airport Kuwait Kuwait City - Kuwait International Airport Jordan Amman - Queen Alia International
 • dikteta Manuel Noriega na kwenye vita dhidi ya Irak iliyowahi kushambulia Kuwait Mwana wake George Walker aliingia pia katika siasa akaendelea kuwa rais