Back

ⓘ Milango ya fahamu
Milango ya fahamu
                                     

ⓘ Milango ya fahamu

Milango ya fahamu ni ogani za mwili zinazoturuhusu kujua mazingira yetu. Mifano yake ni macho na masikio. Ni njia asili ya kutambua mtazamo au hisia.

Kibiolojia inaelezwa kuwa ogani yenye uwezo wa kupokea habari za nje ya mwili, kama vile nuru, sauti, halijoto, mwendo, harufu au ladha, na kuzibadilisha katika mishtuko ya umeme inayofikishwa kwa njia ya mfumo wa neva hadi ubongo.

Kama milango ya fahamu imeharibika, tunasema mtu ni kipofu, bubu au kiziwi, ana matatizo kuelewa mazingira yake sawa na jinsi wanavyoweza watu wengine.

Milango ya fahamu ni muhimu sana kwa Viumbe hai kutokana na kwamba inasadia kiumbe hai katika shughuli zake za kila siku, hasa katika kufatuta mahitaji muhimu kwa Kiingereza yanaitwa Basic needs.

                                     

1. Fahamu zetu

Mara nyingi watu hutaja fahamu tano ambazo ni:

 • Kuonja ni fahamu ya ladha kupitia ulimi
 • Kusikia ni fahamu ya sauti kupitia masikio
 • Mguso ni fahamu ya nyuso za vitu kupitia ngozi, hasa ya mkono
 • Kuona ni fahamu ya nuru kupitia macho
 • Kunusa ni fahamu ya harufu kupitia pua

Hali halisi kuna fahamu zaidi:

 • Fahamu ya maumivu
 • Fahamu ya joto - baridi
 • Fahamu ya uwiano inayotuwezesha kusimama, kutofautisha juu na chini
 • Fahamu ya mwili wetu inayotuwezesha kugusa pua wakati macho yamefungwa
                                     

2. Mfumo wa kibiolojia ya fahamu zetu

Ogani mbalimbali za mwili ziko tayari kupokea vichocheo kutoka mazingira yetu.

Neva katika ogani husika zina uwezo wa kupokea vichocheo vya nje vinavyotafsiriwa katika ubongo kwa fahamu mbalimbali

 • vichocheo vya halijoto vinavyotuwezesha kutofautisha joto na baridi
 • vichocheo vya athari hatari vinavyotafsiriwa na ubongo kwa maumivu au kichefuchefu
 • vichocheo vya nuru vinavyotuwezesha kuona
 • vichocheo vya shinikizo na mwendo
 • vichocheo vya kikemia vinavyotuwezesha kuonja na kunusa

Wanyama pia wana ogani zinazowawezesha kutambua:

 • vichocheo vya mnururisho sumakuumeme nje ya nuru ya kawaida, kwa mfano nyuki hutambua mawimbi ya urujuanimno yasiyoonekana na binadamu
 • vichocheo vya umeme
 • vichocheo vya kusumaku kwa mfano ndege wanaohamahama mbali kila mwaka kwa kufuata uga wa sumaku wa dunia
                                     
 • tofauti na kiwiliwili. Maumbile ya kichwa yametokea kwa njia ya mageuko ya uhai. Katika mchakato huu milango ya fahamu mdomo na kitovu cha neva zilianza
 • kuvifahamu kupitia milango ya fahamu tu. Mifano Upepo mkali umetokea kaskazini mwa bahari ya Hindi Kumetokea na wizi katika nyumba ya jirani Wivu ukizidi
 • na joto. Binadamu ana milango ya fahamu kwa ajili mnurirsho huo kama vile macho kwa nuru na neva kenye ngozi kwa joto. Mifano ya mnururisho isiyoonekana
 • wimbi katika midia ulipo. Kwa macho ya fiziolojia na saikolojia sauti ni mapokezi ya wimbisauti kwa milango ya fahamu hasa sikio na utambuzi wake katika
 • Masafa ya mawimbi hutofautiana sana. Mawimbi marefu yanayoweza kutambuliwa na milango ya fahamu ya binadamu ni sauti ya besi yenye masafa ya mita 21
 • zaidi, uhalisia unajumlisha hata mambo yasiyofikiwa na milango ya fahamu vifaa na mawazo ya binadamu. Wanafalsafa, wanahisabati, wanasayansi na wengineo
 • pia popo ya Desmodus rotundus hujo Amerika Kusini mwenye mlango wa fahamu wa kutambua windo lake. Kua pia aina za wadudu wenye milango fahamu za pekee
 • microwave, mawimbi ya redio ambazo zinatofautiana na nuru kwa idadi ya marudio yake na hazitambuliwi kwa macho au milango ya fahamu isipokuwa joto linalotambuliwa
 • wake katika mafundisho juu ya tabia za vitu vyenyewe. Plato aliona ya kwamba ujuzi wote tunaopata kupitia milango ya fahamu hukosa uhakika, si kamili
 • mwendo wa mifupa sikivu unapokelewa na mishipa ya fahamu ya sikio la ndani ukibadilishwa kwa mishtuko ya umeme inayopita kwenye neva hadi ubongo. Chumba
 • yasiyoonekana kwetu, maana hatuna milango ya fahamu kwake. Lakini zimegunduliwa na sayansi ya kisasa na kutumiwa kwa njia ya teknolojia mbalimbali. Kimsingi