Back

ⓘ Mana
Mana
                                     

ⓘ Mana

Mana ni chakula kilichotumiwa na Waisraeli walipotangatanga katika jangwa la Sinai miaka 40 mfululizo baada ya kutolewa na Musa nchini Misri walipokuwa wananyanyaswa.

Habari hizo zinapatikana katika vitabu vingi vya Biblia hasa Kutoka 16:1-36 na Hesabu 11:1-9 na vilevile katika Kurani 5:27.

Pamoja na maelezo mbalimbali yaliyotolewa na wataalamu kuhusu asili ya chakula hicho, kwa imani kilitazamwa kama ishara ya pekee ya Mungu kuwashughulikia watu wake.

Yesu alikitumia hicho pia kujitambulisha ni nani kwa binadamu wote: "Mimi ndimi chakula cha kweli kilichoshuka kutoka mbinguni" Yoh 6.

                                     

1. Fumbuzi za kisayansi

Wanasayansi wamejaribu kufumbua kitu hicho cha mana. Ufumbuzi mmoja ni kwamba mana ni sandarusi ya mchamwino, mti unaomea sana katika Rasi ya Sinai. Sandarusi hii ni tamu na ikiwa imekauka ina rangi ya hudhurungi.

Ufumbuzi mwingine ni kwamba mana ni mchozo wa wadudu kama vidukari na wadudu-gamba, k.m. mdudu-gamba wa mchamwino Trabutina mannipara. Katika hali ya hewa moto na kavu ya Rasi ya Sinai mchozo huo hukauka haraka. Fuwele za mchozo huo ni tamu na zina rangi ya manjano au hudhurungi. Mara nyingi michozo kama huo huitwa mana pia.

                                     

2. Marejeo

 • Heinrich, Clark 2002. Magic Mushrooms in Religion and Alchemy. Rochester, VT: Park Street Press. ISBN 0-89281-997-9.
 • McKenna, Terence 1993. Food of the Gods: The Search for the Original Tree of Knowledge, A Radical History of Plants, Drugs, and Human Evolution. New York, NY: Bantam Books. ISBN 0-553-37130-4.
 • Merkur, Dan 2000. The Mystery of Manna: The Psychedelic Sacrament of the Bible. Rochester, VT: Park Street Press. ISBN 0-89281-772-0.
 • Arthur, James 2000. Mushrooms and Mankind: The Impact of Mushrooms on Human Consciousness and Religion. Escondido, CA: Book Tree. ISBN 1-58509-151-0.
                                     

3. Viungo vya nje

 • Devotion and Use of the Manna of Saint Nicholas
 • chabad.org, The Manna
 • Catholic Encyclopedia, Manna
 • Jewish Encyclopedia, Manna
 • Lycaeum Archived Novemba 14, 2013 at the Wayback Machine., Manna as a mushroom
                                     
 • Kisiwa cha Mana Hawanja ni kisiwa kimojawapo cha mkoa wa Mtwara, nchini Tanzania, ambacho kinapatikana katika Bahari ya Hindi. Orodha ya visiwa vya Tanzania
 • Kwa mana mengine ya jina hili angalia hapa Bukene maana Bukene ni kata ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini katika Mkoa wa Shinyanga, Tanzania yenye msimbo
 • yanapita yale yote ya watakatifu, na mtu aliye na roho yake anakuta humo mana iliyositirika. Lakini inatokea kuwa wengi, kwa kusikia Injili mara nyingi
 • kilichozidi kinatolewa kama mana kitone cha shira chenye ukolezi mkubwa sana wa sukari: honeydew kwa Kiing. Sisimizi wanapenda mana sana lakini hawawezi kunywa
 • chini ya Jimbo Kuu la Kinshasa. Askofu wake ni Donatien Bafuidinsoni Maloko - Mana S.J. Eneo ni la kilometa mraba 100, 000, ambapo kati ya wakazi 1, 150, 000
 • Managua Kinahuatl: Mana - ahuac - kando la maji ni mji mkuu wa Nikaragua pia mji mkubwa wa nchi hii mwenye wakazi milioni 1.3. Mji uko kando la ziwa
 • Boua 4 056 Dogbo 8 634 Gléré 3 536 Gnépasso 12 216 Magnery 6 021 Mana 1131 Côte d Ivoire. Iliwekwa mnamo 22 Julai 2019. RGPH 2014, Répertoire
 • Korongo hawa pia mana ni ndege wa familia ya Gruidae wenye domo fupi na jembamba kuliko lile la korongo wa familia ya Ciconiidae. Spishi nyingi hufanya
 • khalifatu - rasul - i - llah kinachomaanisha Makamu wa mtume wa Allah Mungu Hivyo mana yake ni makamu au mfuasi wa Mtume Muhammad katika nafasi yake kama kiongozi
 • Agano kati yake na Israeli. Inawezekana vilikuwemo pia fimbo la Haruni na mana kidogo, ingawa 2Waf 8: 9 inasema wakati wa Solomoni hivyo havikuwemo. Carew
 • Jeanjos Parfait, alitoa wimbo wake wa kwanza wa kazi yake uitwao Urakoze mana wimbo ambao unazungumza juu ya ndoa kama zawadi kutoka kwa Mungu. Wimbo
 • nyoga. Na hata wadudu - kibibi walanyama hula dutu nyingine pia kama vile mana mbelewele, mbochi, utomvu na kuvu. Wadudu - kibibi hutumika katika uthibiti