Back

ⓘ Sayansi
                                               

Kupenyeza kwa ubongo

upenyezi ya ubongo, pia inajulikana kama obliteration sisteni, ni jeraha la upande athari za juu shinikizo ndani ya ubongo ambapo ubongo unahama kutoka katika sehemu yake ya kawaida hususani ubongo katika fuvu la kichwa. Ubongo huweza kuhama na miundo vile kama falksi ya ubongo, tentoriumu serebeli, na hata kwa njia ya tundu liitwalo forameni magnamu katika mwisho wa kitako cha fuvu la kichwa. kujipenyeza kwa ubongo husababishwa na mambo kadhaa ambayo husababisha athari ya molekuli na kuongeza shinikizo ndani ya ubongo: ambayo inajumuisha{2,}kiwewe,kuumia ubongo, kiharusi, au kusababisha u ...

                                               

Mpango wa uzazi kwa kutumia kiraka

Kiraka mimba ni kiraka cha kupitisha dawa kwenye ngozi na hupakwa kwenye ngozi kutoa homoni ya kusanisi,estrogini,{na{/2} projestini homoni ili kuzuia mimba.Kiraka ya kuzuia mimba imeonyeshwa kama enye kuthirika kama kuunganisha dawa ya kuzuia mimba kidonge vyema.kiraka yaweza kuwa vyema katika matumizi ya kawaida Viraka vya mpango wa uzazi vinavyopatikana kwa sasa ni Ortho Evra, ambavyo huuzwa Uingereza na nchi nyingine kwa Janssen-Cilag. viraka hivi ni vifurushi ambavyo vimepakiwa katika masanduku kwa utatu na vinapatikana kwa agizo la daktari pekee. Kirasmi, kiraka mimba mara nyingi huj ...

                                               

Umbra

Umbra ni sehemu ya kivuli penye giza zaidi. Inaweza kuitwa pia kitovu cha kivuli. Jina hilo hutumiwa hasa kutaja aina ya kivuli kinachotokea wakati wa kupatwa kwa Jua au kupatwa kwa Mwezi. Umbra au kitovu cha kivuli hutofautishwa na penumbra au kivuli cha kando, ambako giza linapungua. Wakati wa kupatwa kwa Jua umbra ni eneo jembamba la kilomita kadhaa ambako Jua linafunikwa kabisa na Mwezi ikiwa giza linatokea kwa dakika kadhaa wakati wa mchana. Katika sehemu pana zaidi za penumbra au kivuli cha kando, Jua linaonekana kisehemu; karibu na kanda ya umbra mwanga unapungua lakini kwenye sehem ...

Sayansi
                                     

ⓘ Sayansi

Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa.

Mara nyingi Galileo Galilei anahesabiwa kuwa baba wa sayansi ya kisasa.

                                     

1. Aina za sayansi

Kuna sayansi mbalimbali ambazo huainishwa katika makundi yafuatayo:

Sayansi Asili k.m.

 • Biolojia
 • Jiografia
 • Zoolojia

Sayansi Umbile k.m.

 • Fizikia
 • Kemia
 • Hisabati

Sayansi Jamii k.m.

 • Saikolojia
 • Siasa
 • Akiolojia
 • Elimu

Sayansi Tumizi k.m.

 • Uhandisi
 • Teknolojia

Pia, kuna sayansi zinazohusu mada mbalimbali:

 • Unajimu
 • Tiba
 • Maarifa
                                     

2. Mbinu za kisayansi

Msingi wa sayansi ni vitendo. Vitendo vya kisayansi vina njia zake zinazotumika kuthibitisha kweli za kisayansi.

Namna ya kueleza jambo kisayansi huchimbuka toka nadharia ama udhanifu. Halafu, ili kweli ikubalike, hutoka kwenye udhanifu na kwa kupitia majaribio rasmi, hutengeneza dhana kamili ama nadharia kama ni shauri la kueleza mwenendo na tabia.

Kwa hivyo, asili ya njia ya kisayansi ni mtazamo unaokwenda sambamba na vitendo vinavyochunguzwa. Kutoka mitazamo wanasayansi wanaunda nadharia. Baadaye wanaangalia kama bashiri za nadharia ni kweli. Isipokuwa kweli watakanusha nadharia hiyo. Ikionekana kwamba mara nyingi sana nadharia ilibashiri ukweli, na haijakosea, itakuwa nadharia inayokubalika.

                                     

3. Sura ya kisayansi

Mara chache, maarifa yatokanayo na sayansi yanaweza kupinga hali ya kawaida. Kwa mfano nadharia ya atomu inasema kwamba katika jiwe maada yabisi kuna uvungu dutu tupu, na kwamba atomi zinacheza katika nafasi ndogo katika jiwe ukifananisha na maada kimiminika. Lakini kwa nadharia hii tunaweza kueleza mambo mengi, hata kwa nini tunaweza kusema kwamba jiwe halina uvungu.

                                     

4.1. Historia Sura ya kiutamaduni

Sayansi iliaanza kama udadisi wa mtu mmojammoja; lakini kadiri maarifa yanavyopanuka, inakuwa vigumu kwa mtu mmoja kufanya mchango wa kujitenga. Hivyo jumuiya zimebeba kusudi ambalo hapo mwanzo lilionekana kama ni shauku la mtu mmojammoja kama awali.

Hii hufanya mkururo wa ugunduzi ama uvumbuzi kuwa sehemu ya historia ya sayansi. Majina na sifa kutajwa sambamba na shauri la aliyepelekea.

Sayansi na jamii huenda pamoja katika kuleta mabadiliko, kwa kuwa mabadiliko huletwa na watu wenyewe.

                                     

4.2. Historia Sayansi na siasa za dunia

Katika dunia hii ya leo, maendeleo ya watu hujidhihirisha sana kutokana na jinsi jamii husika ilivyopiga teke katika uwanja huu.

Ingawaje haibainishwi wazi miongoni mwa sura ya mambo ya kidunia, sayansi kwa kweli ni nguvu inayoweza kubadili maisha ya watu kwa wema; lakini katika kilele chake cha mafanikio, vyombo vyenye nguvu za mamlaka na fedha hushikilia baadhi ya matunda yake katika hali ya kibiashara na kiutawala zaidi.

                                     

4.3. Historia Sayansi na maendeleo

Wapo watu pia ambao hutumia sayansi kujaribu kuboresha maisha ya watu wote kwa ujumla. Hivyo sayansi haibakii tu mikononi mwa wenye kushika dau kimifumo, bali changamoto ya wote wenye kutaka kuleta maendeleo ya ujumla.

Hivyo roho ya uchunguzi ndiyo iliyoleta kuzaliwa, kukua na kutapakaa kwa sayansi.