Back

ⓘ Imani sahihi
Imani sahihi
                                     

ⓘ Imani sahihi

Imani sahihi ni msimamo unaokubali mafundisho sanifu ya dini fulani, tofauti na yale ya wachache.

Umuhimu wa jambo hilo unasisitizwa hasa katika dini inayokiri umoja wa Mungu, lakini si katika dini nyingine kama zile za jadi au za miungu mingi.

Katika Ukristo, inamaanisha kwa kawaida kukubali imani kama ilivyofundishwa na mitaguso ya kiekumene katika karne za kwanza za dini hiyo dhidi ya uzushi wa aina mbalimbali.

                                     

1. Historia

Matumizi ya neno hilo yanashuhudiwa kwanza na Codex Iustinianus Mkusanyo wa Justiniani I ya miaka 529-534, inayodai majimbo yote duniani yawekwe chini ya maaskofu waliokubali kanuni ya imani ya mtaguso mkuu wa Nisea

Baada ya farakano la mwaka 1054 kati ya Kanisa la Kilatini na Makanisa ya Mashariki ambayo yalikuwa bado na ushirika na Papa wa Roma, ingawa pande zote mbili ziliendelea kujiona ya Kiorthodoksi na ya Kikatoliki, polepole neno la kwanza limekuwa likitumiwa zaidi na Ukristo wa Mashariki na lile la pili na Ukristo wa Magharibi.