Back

ⓘ Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Antiokia
                                     

ⓘ Liturujia ya Antiokia

Liturujia ya Antiokia, inayoitwa pia Liturujia ya Siria, ni jina la taratibu za ibada ya Wakristo ambayo ina asili yake katika mji wa Antiokia wa Siria ambao katika karne ya 1 ulikuwa kituo kikuu cha umisionari wa Kanisa, halafu ukawa na shule ya teolojia muhimu kama ile shindani ya Aleksandria.

Wanaotumia liturujia hiyo ni hasa Kanisa la Kiorthodoksi la Siria na madhehebu yenye uhusiano naye kihistoria hasa matawi ya Kanisa la Kiorthodoksi la Kisiria la Malankara kutoka India, na yale yaliyotokana nalo, yakiwa pamoja na Kanisa Katoliki la Kisiria na Kanisa Katoliki la Kimalankara. Kwa kiasi kikubwa liturujia hiyo ni pia ya Kanisa la Wamaroni.

                                     

1. Historia

Liturujia hiyo ilitokana hasa na ile ya Kigiriki iliyotumiwa kwanza na Patriarki wa mji huo kama Ignas wa Antiokia mwanzoni mwa karne ya 2, lakini, baada ya farakano la mwaka 451 lililofuata Mtaguso wa Kalsedonia, ilitafsiriwa katika lugha ya Kiaramu, iliyokuwa ya kawaida zaidi katika maeneo yote ya kandokando.

Matini ya Kiaramu ya zamani zaidi yaliyobaki hadi leo ni ya karne ya 5 Yanatunza kumbukumbu muhimu kuhusu liturujia ilivyokuwa wakati huo, nazo zinatusaidia kufuatilia mabadiliko yaliyofanyika baadaye.

Kuanzia anafora ya awali, iliyotafsiriwa kutoka ile ya Kigiriki ya Mt. Yakobo, zilitungwa nyingine nyingi, si chini ya 39.

Wakatoliki ndio waliofanya utafiti bora zaidi juu ya liturujia hiyo, wakitoa vitabu rasmi ili kupunguza fujo iliyojitokeza pengine kati ya Waorthodoksi wa Mashariki. Kati ya anafora hizo zote, wanazitumia saba tu.

Pengine masomo ya Biblia yanafanyika kwa Kiarabu, lugha ya kawaida ya waamini wengi huko Mashariki ya Kati. Lakini waamini wengi zaidi wanaishi India kusini.

                                     

2. Marejeo

 • Wainwright, Geoffrey; Karen Beth Westerfield Tucker 2006. The Oxford History of Christian Worship. Oxford University Press. ISBN 0-19-513886-4. Retrieved on April 5, 2010.
 • King, Archdale 2007. The Rites of Eastern Christendom 1. Gorgias Press LLC. ISBN 1-59333-391-9. Retrieved on April 5, 2010.
 • Chupungco, Anscar J. 1997. Handbook for Liturgical Studies. Liturgical Press. ISBN 0-8146-6161-0. Retrieved on April 5, 2010.
                                     

3. Viungo vya nje

 • Documentary film about Syriac Christians Archived Septemba 25, 2010 at the Wayback Machine.
 • Noohro "The Light" Weekly Bulletin
 • Shroro: The Syriac Christian Digest
 • Syrian Liturgy description and photos
 • Syriac Music Online
                                     
 • Liturujia ya Kilatini ni aina ya liturujia ya Ukristo iliyoenea upande wa magharibi wa Dola la Roma ambapo ilitumika lugha ya Kilatini. Liturujia hiyo
 • Liturujia ya Braga ni liturujia maalumu inayotumika tangu karne ya 6 hasa katika jimbo kuu la Braga Ureno Inahusiana na aina nyingine za liturujia
 • Liturujia ya Roma ni liturujia iliyoenea katika sehemu kubwa ya Kanisa Katoliki, kutoka makao yake makuu, Roma Italia Kwa asili yake ni liturujia ya
 • Liturujia ya Milano ni liturujia maalumu ambayo inatumika katika sehemu kubwa ya jimbo kuu la Milano na katika parokia kadhaa za majimbo ya kandokando
 • Liturujia ya Toledo au liturujia ya Kimozarabu, yaani ya kati ya Waarabu ni liturujia ya pekee inayotumika hasa katika jimbo la Toledo Hispania pamoja
 • Liturujia ya Lyon kwa Kilatini: ritus Lugdunensis ni liturujia mojawapo ya Kanisa la Kilatini ambayo imeendelea kutumika katika jimbo kuu la Lyon Ufaransa
 • zote. Liturujia hiyo ilianza kwa kufuata liturujia ya Siria, kwa kuwa kabla ya mwaka 381 Mashariki ya Kati ilikuwa chini ya Kanisa la Antiokia Mwaka
 • Liturujia ya Roma isiyo ya kawaida ni taratibu za ibada zinavyotumika katika Kanisa Katoliki kufuatana na mapokeo ya Roma jinsi yalivyokuwa mwaka 1962
 • Liturujia ya Vipindi ni sala rasmi ya Kanisa kama inavyoadhimishwa katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo, lakini ni jina hasa la mpangilio unaofuatwa
 • kusali ulistawi kuanzia Antiokia ukaenea kwanza Mashariki halafu Mashariki hasa katika karne IV. Mfano wa litania fupi katika liturujia ni Mwanakondoo wa Mungu