Back

ⓘ Boda bodaBoda boda
                                     

ⓘ Boda boda

boda ni neno la kutaja baisikeli inayotumiwa kubeba abiria katika Afrika ya Mashariki au "baisikeli ya teksi". Linaweza kumtaja pia dereva wa baisikeli hii.

Asili yake ni kati ya Wajaluo wa eneo la mpakani kati ya Kenya na Uganda karibu na ziwa Viktoria. Inasemekana asili yake ilikuwa huduma ya kubeba abiria kati ya mipaka ya Kenya na Uganda mjini Busia. Hivyo neno la Kiingereza la "border" = "boda" lilikuwa chanzo cha jina "boda-boda" Lakini huduma imeenea sehemu mbalimbali kama vile pwani ya Kenya Mombasa, Malindi na pia katika Uganda.

Baisikeli ya kawaida inayotakiwa imara hubadilishwa kwa kuweka kiti kirefu kama cha pikipiki.

                                     

1. Pikipiki badala ya baisikeli

Uganda imeona mabadiliko ambapo pikipiki zinachukua nafasi za boda katika kazi ya kubeba abiria. Kuna makadirio kuhusu mwaka 2004 ya kuwa watu 200.000 Uganda walikuwa madereva wa boda ya baisikeli na 90.000 wa boda ya pikipiki.

                                     

2. Ajali

Baada ya wengi kuacha baiskeli na kukimbilia pikipiki kwa ajili ya boda boda, kumekuwa na ongezeko kubla la ajali barabarani. Karibu kila siku watu wanafariki kwa ajali za namna hiyo.

Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →