Back

ⓘ Maporomoko ya maji
Maporomoko ya maji
                                     

ⓘ Maporomoko ya maji

Kwa matumizi mengine ya jina angalia maporomoko

Maporomoko ya maji ni mahali ambako maji yanatelemka juu ya kona kwenye mtelemko na kuelekea chini. Kwa kawaida ni sehemu ya njia ya mto au kijito pale ambako maji yanatelemka juu ya ukingo wa mwamba. Lakini inaweza kutokea pia kwenye ukingo wa barafuto pale ambako maji ya myeyuko yanatelemka.

                                     

1. Kutokea na kubadilika kwa maporomoko ya maji

Maporomoko ya maji hutokea kwa kawaida katika sehemu za juu ya njia ya mto. Hapa mtelemko kwa jumla ni mkubwa zaidi na mwendo wa maji haraka zaidi. Kwa hiyo nguvu ya maji ni kubwa zaidi kiasi inaweza kuchimba lalio hadi imekuwa mfereji kama korongo mrefu.

Pale ambako mwendo wa maji ni juu ya mwamba mgumu mmomonyoko hutokea polepole tu. Pale yanapofikia mahali ambako mwamba mgumu wa juu unakwisha nguvu ya maji yakitelemka kwenye ukingo inachimba lalio ya chini. Chini ya ukingo hutokea dimbwi yenye kizingia cha maji. Maji yanayozunguko humo pamoja na mawe na mchanga ndani yake yanasuguana kwenye ukuta wa mwamba. Kwa njia upeno au nusu pango hutokea. Kama kuna mwamba laini chini ya takaba ya mwamba mgumu wa juu upanuzi wa pango unaendelea haraka zaidi. Baada ya muda upeno unakatika na kuanguka.

Kwa njia hii ukingo wa maporomoko unarudi nyuma na kurudisha njia ya korongo nyuma. Kasi ya harakati inategemea na tabia za mwamba unaopatikana. Kuna maporomoko yanayorudi nyuma mita na nusu kila mwaka.

Baada ya muda wa kutosha wakati mwingine miaka mamillioni nguvu ya maji umeondoa mwamba wa kutosha hali hakuna maporomoko tena na ngazi katika njia imekuwa mtelemko tu.

                                     
  • Maporomoko ya Maji Materuni ni moja ya maporomoko ya maji katika Mto Mware kata ya Uru Mashariki, Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania
  • Maporomoko ya Iguazu ni idadi ya maporomoko ya maji kwenye mto Iguazu ambayo yanapatikana kwenye mpaka wa Argentina na Brazil. Kuna maporomoko 275 ya
  • ya mtelemko wa ghafla. Mara nyingi jina hilo linatumiwa pia kutaja mahali ambako maporomoko ya maji hutokea au yalitokea. Maporomoko ya maji Kata ya Maporomoko
  • Maporomoko ya Niagara Niagara Falls ni mfululizo wa maporomoko ya maji kwenye mto Niagara yaliyopo mpakani mwa Kanada na Marekani kati ya Ziwa Erie
  • Maporomoko ya Kalambo yanatokana na mto Kalambo ambao ni mpaka wa Tanzania na Zambia. Maporomoko ya maji haya ukiachilia kuwa ni ya pili baada ya yale
  • Maporomoko ya Huangguoshu ni mojawapo ya maporomoko maarufu yenye maajabu zaidi duniani. Maporomo ya Huangguoshu yanapatikana bara la Asia nchini China:
  • Victoria Falls au Maporomoko ya Viktoria Mosi - oa - Tunya ni maporomoko ya mto Zambezi mpakani mwa Zambia na Zimbabwe. Mto Zambezi wenye upana wa mita
  • maji kama mito vinatumika katika usafirishaji wa magogo Hutumika katika uzalishaji wa umeme maji hutumika kuzalisha umeme kutokana na maporomoko ya maji
  • kati ya mito ya mkoa wa Kilimanjaro Tanzania Kaskazini Mashariki Unapitia Materuni halafu una maporomoko ya maji Mito ya Tanzania Orodha ya mito ya mkoa