Back

ⓘ Jamii:Uzoroasta
                                               

Uzoroasta

Uzoroasta ni dini na falsafa inayopata jina lake kutoka nabii wake Zoroasta au Zarathustra, ambayo iliathiri imani ya Uyahudi na ya dini zilizotokana na Uyahudi. Wazoroasta wanaamini katika ulimwengu na Mungu apitaye fikira, Ahura Mazda, ambaye ibada zote zinaelekezwa kwake. Kiumbe cha Ahura Mazda ni asha, ukweli na mpango, ambaye anazozana na kinyume chake, druj, uongo na machafuko. Kwa sababu binadamu ana hiari, watu lazima wawe na uwajibikaji kwa maadili wanayoyachagua. Kwa kutumia hiari, watu lazima wawe na jukumu tendaji katika mgogoro wa dunia nzima, na mawazo mema, maneno mema na ma ...

                                               

Zoroasta

Zoroasta, pia Zarathustra alikuwa mwanzilishaji wa dini ya Uzoroasta na nabii ya kwanza wa imani hii. Hakuna uhakika wala juu ya mahali wala wakati alipoishi. Leo hii wataalamu wengi wanaamini aliishi katika mashariki ya Uajemi ya Kale. Habari zilihifadhiwa kimdomo kwa muda mrefu na kuandikwa karne baada yake kwa hiyo ni vigumu kujua umri wa habari zake. Wataalamu wamekadiria wakati wa maisha yake kati ya miaka 1800 KK na 600 KK ilhali hakuna uhakika. Jina lake liliandikwa katika maandiko ya kale zaidi kwa umbo la Zarathustra. Kimatifa amejulikana zaidi kwa umbo la Kigiriki yaani Zoroasta ...