Back

ⓘ Kolumbani
Kolumbani
                                     

ⓘ Kolumbani

Kolumbani abati alikuwa mmonaki mmisionari kutoka Ireland, maarufu kwa kuanzisha monasteri nyingi na kueneza Ukristo wa Kiselti katika nchi mbalimbali za Ulaya bara, ukiwa pamoja na kanuni kali ya kitawa, malipizi, na maungamo ya binafsi kwa padri.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, hasa siku ya kifo chake, tarehe 23 Novemba.

                                     

1. Sala zake

Ee Kristo Bwana, utujalie daima maji haya yawe ndani mwetu pia chemchemi ya maji hai yanayobubujikia uzima wa milele!

Kwa hakika naomba jambo kubwa; nani asiyejua?

Lakini wewe, mfalme wa utukufu, unajua kuzawadisha makuu, tena umeahidi makuu.

Hakuna kilicho kikuu kuliko wewe: lakini umejizawadisha kwetu na kujitoa kafara kwa ajili yetu.

Kwa hiyo tunakuomba utujulishe tunachopenda, kwa kuwa hatutafuti chochote nje yako.

Kwetu wewe ni yote: uhai wetu, mwanga wetu, wokovu wetu, chakula chetu, kinywaji chetu, Mungu wetu.

Ee Yesu wetu, nakuomba uivuvie mioyo yetu kwa mvumo wa Roho wako na kuzichoma roho zetu kwa upendo wako ili kila mmojawetu aweze kusema kwa ukweli wote: Unijulishe mpenzi wa roho yangu; kwa kuwa nimejeruhiwa na upendo wako.

Ee Bwana, natamani madonda hayo yatiwe ndani mwangu.

Heri yake roho iliyochomwa na upendo! Yenyewe itatafuta chemchemi na kuinywea.

Kwa kuinywea ataionea kiu daima.

Kwa kutuliza kiu yake atatamani kwa ari yule anayemuonea kiu daima, ingawa anamnywa mfululizo.

Hivyo kwa roho upendo ni kiu inayotafuta kwa hamu, ni jeraha linaloponya.

Ee Kristo, Mwokozi wetu mwema sana, tafadhali uwashe taa zetu: ziangaze mfululizo katika hekalu lako na kudumishwa daima na wewe, mwanga wa milele; pembe zenye giza za roho zetu ziangazwe, na giza lolote la ulimwengu lifukuzwe mbali nasi.

Basi, Yesu wangu, uijalie taa yangu mwanga wako, ili kwa uangavu wake nifunguliwe patakatifu pa mbinguni, patakatifu pa patakatifu ambapo chini ya makuba yake makuu panakuwa na wewe, kuhani wa milele wa sadaka ya kudumu.

Unijalie nikutazame, nikukazie macho na kukutamani wewe tu; nikupende wewe tu na kukungojea wewe tu kwa hamu motomoto kabisa.

Katika kutazama kwa upendo hamu yangu izimike ndani mwako na mbele yako taa yangu iangaze na kuwaka mfululizo.

Tafadhali, Mwokozi wetu mpendwa, ujionyeshe kwetu tunaopiga hodi, ili, kwa kukufahamu, tukupende wewe tu, tukutamani wewe tu, tukufikirie mfululizo wewe tu, na kutafakari usiku na mchana maneno yako.

Tafadhali utumiminie upendo mkubwa ambao unakufaa wewe uliye Mungu na unastahili kupewa, ili upendo wako uenee katika nafsi yetu yote na kutufanya wako kabisa.

Hivyo hatutaweza kupenda chochote nje ya wewe uliye wa milele, na upendo wetu hautaweza kuzimwa na maji mengi ya uwingu huu, ya dunia hii na ya bahari hii, kama ilivyoandikwa, Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo.

Hayo yatimie hata kwetu kwa neema yako, Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye upewe utukufu milele na milele. Amina.

                                     

2. Maandishi yake

 • San Colombano. Le opere, a cura di Inos Biffi e Aldo Granata, Jaca Book, Milano 2001.
 • San Colombano, Lettere e poesie, Abbazia San Benedetto, Milano 1998. ISBN 9788887796360
 • San Colombano abate, Istruzioni e regola dei monaci, Abbazia San Benedetto, Milano 1997.
                                     

3. Viungo vya nje

 • Kifaransa Jean Markale, Le periple de Saint Colomban, Geneve 2001. ISBN 2825706922
 • M. Stokes, Six Months in the Appennines in Search of the Irish Saints in Italy, London 1892.
 • Kifaransa Abbè Martin, Saint Colomban, Paris 1905.
 • St. Columban, Abbot and Confessor Archived Septemba 19, 2012 at the Wayback Machine. – St. Columban Parish, Loveland, Ohio
 • About the Knights of St. Columbanus Archived Machi 21, 2008 at the Wayback Machine.
 • T. Concannon, The life of St.Columban, Catholic T. Society of Ireland, Dublino 1915.
 • Life of St. Columban, English translation
 • Knights of St. Columbanus
                                     
 • 627 alikuwa mmonaki kutoka Ufaransa wa leo anayetajwa kama mfuasi wa Kolumbani Baada ya kufukuzwa nchini 612 walianzisha monasteri mpya huko Bobbio
 • XV 1904 - Coleman Hawkins, mwanamuziki kutoka Marekani 615 - Mtakatifu Kolumbani abati mmisionari kutoka Eire 1011 - Reizei, mfalme mkuu wa Japani 967 - 969
 • aliachiwa na Filiberti wa Tournus monasteri yake iliyofuata kanuni ya Mt. Kolumbani akaiongoza kama abati hadi kifo chake. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa
 • alikuwa abati wa pili wa Luxeuil kuanzia mwaka 611, akimrithi mwalimu wake Kolumbani baada ya kuwa mkuu wa chuo cha monasteri. Tangu kale anaheshimiwa na
 • Ufaransa, 698 hivi alikuwa mmonaki wa Kanisa Katoliki, mwanafunzi wa Kolumbani Pamoja na Momelini alianzisha monasteri iliyovutia miito mingi akafanya
 • 685 696 alikuwa mmonaki wa Kanisa Katoliki, aliyeunganisha desturi za Kolumbani na za Benedikto kwa monasteri ambazo alizianzisha na kuziongoza. Aliuawa
 • 18 Januari 625 alikuwa mmonaki wa Ukristo wa Kiselti, mwanafunzi wa Kolumbani na kaka wa Gall. Alifanya nao kazi kubwa ya kueneza imani na umonaki huko