Back

ⓘ Jamii:Teolojia
                                               

Apokrifa

Apokrifa ni jina linalotumika katika Ukristo kuanzia karne ya 5 kutajia vitabu ambavyo madhehebu husika hayavikubali katika Biblia. Hivyo vitabu vilevile vinaweza kuwa vitakatifu kwa madhehebu kadhaa lakini si kwa mengine. Lakini kuna vitabu vingine ambavyo vinatazamwa na Wakristo wote kuwa ni apokrifa, kwa mfano "Maisha ya Adamu na Eva". Maelezo ya undani zaidi yanapatikana katika makala Deuterokanoni kuhusu vitabu maarufu zaidi vinavyokubaliwa na Kanisa Katoliki na wengineo kama Neno la Mungu, lakini si na Waprotestanti wengi.

                                               

Ario

Ario alikuwa padri kutoka Libya aliyefanya kazi huko Alexandria, Misri. Mafundisho yake yalisisitiza kuwa Mungu Baba ni mkuu kuliko Mwana, akipinga imani katika Utatu. Kristolojia yake ilikanushwa na askofu wake, Aleksanda wa Aleksandria, lakini ilienea kote mashariki mwa Dola la Roma na kuvuruga Kanisa Katoliki kiasi cha kudai Kaisari Konstantino I aitishe Mtaguso wa kwanza wa Nisea mwaka 325. Huo mtaguso mkuu wa kwanza, uliokusanya maaskofu wengi hasa wa mashariki, ulikataa hoja zake na kumkiri Mwana kuwa na hali ileile ya Baba. Hata hivyo vurugu ziliendelea hata kudai ufanyike mtaguso w ...

                                               

Babu wa Kanisa

Babu wa Kanisa ni jina la heshima ambalo kuanzia karne IV Kanisa Katoliki limewapatia Wakristo wa kale, wenye utakatifu, elimu na imani sahihi, ambao mafundisho yao yanawezesha kujua mapokeo ya Mitume. Orodha ya kwanza ya mababu wa Kanisa iliandikwa katika Hati ya Gelasi karne VI; baadhi yao waliongezewa jina la Mwalimu wa Kanisa. Muhimu zaidi upande wa Mashariki ni: Atanasi, Basili Mkuu, Gregori wa Nazienzi na Yohane Krisostomo. Upande wa Magharibi ni: Ambrosi, Agostino wa Hippo, Jeromu na Papa Gregori I.

                                               

Baraka

Baraka ni tendo la kumtakia au kumuombea mtu mema, hasa kutoka kwa Mungu. Pengine mtendaji ana mamlaka fulani juu ya yule anayeombewa, hasa katika dini husika. Baraka zinaweza kulenga maisha ya kawaida au mema ya kiroho zaidi utakaso.

                                               

Chuo cha Kikristo cha Aleksandria

Chuo cha Kikristo cha Aleksandria katika karne za kwanza BK kilikuwa kimojawapo kati ya vituo vikuu viwili vya elimu ya Kikristo na kati ya vyuo vya kwanza vilivyofundisha imani ya Kikristo kwa namna ya kitaalamu. Wakati wa Mababu wa Kanisa teolojia na ufafanuzi wa Biblia ya Kikristo vilivyotolewa huko vilitofautiana na Shule ya Antiokia. Majina ya vituo vyote viwili yalitokana na majiji vilipostawi katika Ukristo. Wakati wanateolojia wa Antiokia ya Siria leo nchini Uturuki walifuata zaidi maneno yenyewe ya Biblia, wale wa Aleksandria Misri walipenda zaidi kuifafanua kiroho. Matokeo ya tof ...

                                               

Ekaristi

Jina linatokana na neno la lugha ya Kigiriki εὐχαρίστω eukharisto: "nashukuru" lililotumiwa na Mtume Paulo na Wainjili katika kusimulia karamu hiyo ya mwisho ya Yesu na Mitume wake, na muujiza uliotangulia ambao Yesu alidokeza nia yake ya kushibisha binadamu wote, yaani ule wa kuzidisha mkate na samaki kwa ajili ya umati. Jina linaonyesha mazingira ya sala ya matukio hayo, ambapo Yesu alimuelekea Mungu akimshukuru kwa vyakula na kinywaji alivyoshika mikononi kabla hajawagawia wanafunzi wake. Shukrani ilikuwa msimamo wa msingi wa Yesu kwa Baba maisha yake yote, hasa alipofikia wakati wa kut ...

Hukumu ya mwisho
                                               

Hukumu ya mwisho

Hukumu ya mwisho, Siku ya hukumu au Siku ya Bwana ni sehemu ya imani ya dini za Uzoroasta, Uyahudi, Ukristo na Uislamu. Ni siku ambapo Mungu atahukumu kwa pamoja watu wote walioishi duniani. Fundisho hilo muhimu lilipewa uzito katika sanaa, hasa ya Kikristo, kwa nyimbo na michoro mbalimbali.

Mungu Mwana
                                               

Mungu Mwana

Mungu Mwana kwa Kigiriki Θεός ὁ υἱός, Theos o uios ni nafsi ya pili ya Utatu Mtakatifu wa Mungu pekee. Dogma hiyo ya Ukristo madhehebu yote isipokuwa Wasiosadiki Utatu inamkiri Yesu kuwa Mungu sawa na Mungu Baba na Roho Mtakatifu. Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli inamkiri Mungu Mwana "aliyezaliwa na Baba tangu milele yote", alikuwepo kabla ya kujifanya binadamu tumboni mwa Bikira Maria.

Pantokrator
                                               

Pantokrator

Pantokrator ni aina mojawapo ya michoro ya Yesu Kristo ambayo inalenga kumtangaza kuwa Mwenyezi Mungu. Sababu ni kwamba neno hilo la Kigiriki Παντοκράτωρ lilitumiwa na watafsiri wa kwanza wa Biblia ya Kiebrania kwa ajili ya majina mawili ya Mungu: YHWH Sebaoth Bwana wa majeshi na El Shaddai Mwenyezi Mungu.